Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Uwepo wa vitu gani nisivyo viona wala kuvihisi?Kaka una amini uwepo wa vitu usivyo viona kwa macho ? Wala kuvihisi ?
Sijawahi kukataa uwepo wa Mungu kwa sababu sijamuona wala kumuhisi, unaelewa hilo?
Unaelewa kwamba nakataa uwepo wa Mungu kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, si kwa sababu sijamuona kwa macho wala kumuhisi.
Unaelewa hilo?
Unaelewa kwamba swali lako kwangu ni irrelevant?
Kwa sababu naweza kukuambia nakubali nyumba yangu ipo nyumbani, wakati mimi nipo kazini siioni sasa hivi.
Lakini, kukubali huku hakuna contradiction.
Kinacho matter si kwamba kitu kinaonekana au hakionekani, naweza kukihisi au siwezi kukihisi.
Kinachomatter ni, jambo lina logical consistency? Lina contradiction?
Mungu wako hana logical consistency, ana contradiction.
Habari za kama anaonekana na kuhisika kwangu si muhimu, sijapinga Mungu kwa sababu sijamuona, unanihoji kwa hoja ambayo sijawahi kuitaja.
Unataka kuleta pingamizi ambalo simo humo.
Mimisi wale wanaosema siamini Mungu yupo mpaka uniletee nimuone hapa.
Nakwambia sikubali Mungu yupo, kwa sababu dhana ya kuwapo kwake inajipinga yenyewe hata kabla sijasema lolote.
Unaelewa tofauti hapo?