Hivi hakuna namna bora ya kusherehekea Uhuru bila kuonesha silaha za kivita?

Kuna point katika hoja yako.

Mi nafikiri wanaonyesha hayo mavifaru kama ujumbe kwamba amani tuliyo nayo nchini inatokana na kazi kubwa nyuma ya pazia inayofanywa na majeshi yetu.

Pia kuonyesha kwamba pamoja na kwamba tuna amani lakini mtu yeyote awe wa nje awe wa ndani asimchezee simba sharubu.

Japo kama wangejiongeza zaidi kufikiri wangefanya exhibitions za maana zaidi ya hayo masilaha ya vita.
 
Marekani na Nguvu zote zile za kijeshi hata bunduki hawaonyeshi kwenye gwaride la kumbukumbu ya siku ya uhuru wao 🤣 🤣 Mkubwa ni mkubwa tu, na mkubwa hajaribiwi kwa kushikwa sharubu
Vituko kweli....tunajichimba mikwara wenyewe tena......au akina lisu ndio
 
Tena nashauri Jeshi liwe na kitengo maalum cha silaha za jadi, ambazo zilitumika dhidi ya vita na wakoloni, mikuki, manati, pinde na mishale, mitego mbali mbali, n.k. Kitengo hiki kingekuwa na ladha sana kwenye maonesho kama haya , na si kuonesha mizinga, na makombora. Relevance ya kitengo hiki ni kuwa teknolojia hii ilitumika kuikomboa nchi hii mikononi mwa wakoloni, pia ni kitengo kinachotakiwa kuwepo kwani huko mbeleni kinaweza kuisaidia nchi
 
Infantry bila air cover na air support ni mabata yanayosubiri kupopolewa
Nope wanamove vizuri tu. Isipokuwa kazi itakuwa nzito zaidi. Nanwatapoteza watu wengi zaidi.
Ila ground troops ndio original army. Wakifeli ground troops hao wengine wanafanya kazi bure
 
Bi. Tozo a.k.a Mpemba a.k.a maushungi yumo humu ndani na hakika atapita hapa atasoma kisha atachukua hatua.
 
Sasa yeye ka nchi kapo kama mkoa wa Dar na unaweza kuta hata Dar ni kubwa, kwanini asiagize mengi huku anashinda na kulala Congo kwenye madini? Kwanza atakuwa anaitamani nchi yetu ilivyo kubwa, yeye akipiga mruzi mmoja nchi nzima wanasikia.
Basi tuilinganishe Tz na Israel au Belgium. Maana hizi Nazo ukubwa wake Ni size ya Rwanda.

Au tulinganishe Tz na Russia,USA,China maana hizi Ni kubwa maradufu ya Tz.?
 
Mimi nashukuru wameacha kuonyesha watu wanavunja tofali kwa vichwa.

Badala ya kuonyesha tumeachieve nini kama Taifa ndani ya miaka 60, wao wanaonyesha Masilaha tena yote yametengenezwa nje.

Kwani hakuna achievements ya kuonyesha?
Nami nilitarajia tuoneshwe makuzi ya teknolojia katika kubadilisha maisha ya Watanzania kutoka kilimo cha kutegemea jembe la mkono (wakati tunapata uhuru) kuja kwenye ma planter ya kisasa na ma combine harvester, lkn tunaletewa helikopta za makomandoo. Dah. Msijesema wanatela kwenye Nanenane, huwa hawaleti. Nahudhuria sana hayo maonesho
 
Kwani maandaki hamna we kubali kataa jeshi ni infantry infantry ndo kila kitu jeshini na ndomana askari wote upata mafunzo ya infantry kwanza hayo ndo mafunzo ya awali ya akari mpya hayo Mengine badae....
Umeangalia Vita ya Armenia vs azerbaijan hapo juzi Kati?Mtu kachezea drones mwanzo mwisho,vifaru vimeachwa nyang'anyang'a hakuna cha infantry Wala nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…