Kifo hichi bado kina maswali mengi sana, pamoja na hayo Masanja hana tatizo kutangaza msamaha. Hiyo ni silaha kubwa kuliko zote, ameziba mengi kwa kutangaza haradharani kuwa pamoja na mke wake.
Hakuna ubaya wowote, iwe kweli ama si kweli bado ushindi upo kwa Masanja.
Mungu amsaidie Masanja na mke wake wapite salama katika kipindi hichi kigumu kwao.
Tuelewe kumpenda mke wako na Dunia yote ikajua hakuna ubaya wowote, Wala sio ushamba. Shida yetu tunaona kumpenda mke/mume ni vibaya.
Tumejazwa mitazamo hasi na jamii zetu, mwanaume unaishi na mke wako kama unaishi na jambazi, nikiwa na maana kila kitu umeweka Siri hadi hisia.
Mke wako hajui akaunti yako ya bank, mke hajui mshahara wako, mke hajui nyumba zako ulizojenga kwa Siri.
Mke wako hajui kama unampenda au humpendi! Kila kitu kwako Siri Siri.
Siku yakikupata wengine wanafaidi watoto wako na mke wako wanabaki wanateseka.
Shetani anajua nguvu iliopo katika kushikana vyema na mwenzi wako wa maisha, ndio maana elimu nyingi potofu zinasambazwa kwa Kasi kubwa.
Elimu yeyote iliyo nje au inayopingana na neno la Mungu hiyo elimu sio sahihi.
Penda mke wako, penda mume wako, siku akikuumiza Hilo litabaki kwake mwenyewe ila wewe utakuwa huna hatia.
Tuache kuishi na wenzi wetu kama maadui wetu bila sababu yeyote.
Asante sana.