Hadi Leo imebaki historia tu?? Like seriously??
Kuna vitu vinatafakarisha.
Sativa ambaye wala hakuwa anafahamika , kitendo cha kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo, alitekwa Dar es Salaam wakampeleka Arusha baadae akapigwa risasi na kutelekezwa mbuga ya Katavi wakiamini ameshakufa na mbuga ile ina mamba basi watakuja kumalizia mzoga , ila alibahatika kupona.
Watu waliendesha kilomita 1000+ kwenda kumuua mtu mmoja ambaye hata hakuwa na hatari yoyote .
Sasa ukivuta picha mawe aliyokua anarusha Polepole mpaka wanawafungia mitandao muda anaongea walimuua kwa mtindo gani na pengine walimpa mateso kiasi gani kabla hawajamuua na walimtupa au nae walimpeleka kuwa chakula cha mamba?
Hadi leo ni miaka 2 tangu Sativa atekwe na hakuna aliyekamatwa na Polepole sasa katimiza mwaka hakuna hatua yoyote , msikilize hapo Sativa akieleza alivyotekwa.
View: https://www.youtube.com/live/5GhS9HSzdrw?si=SgsAHzGZ_78zoHq-