Hivi hamsomi mazingira? No way tutamuona akiwa live tena!

Hadi Leo imebaki historia tu?? Like seriously??

Kuna vitu vinatafakarisha.

Sativa ambaye wala hakuwa anafahamika , kitendo cha kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo, alitekwa Dar es Salaam wakampeleka Arusha baadae akapigwa risasi na kutelekezwa mbuga ya Katavi wakiamini ameshakufa na mbuga ile ina mamba basi watakuja kumalizia mzoga , ila alibahatika kupona.

Watu waliendesha kilomita 1000+ kwenda kumuua mtu mmoja ambaye hata hakuwa na hatari yoyote .

Sasa ukivuta picha mawe aliyokua anarusha Polepole mpaka wanawafungia mitandao muda anaongea walimuua kwa mtindo gani na pengine walimpa mateso kiasi gani kabla hawajamuua na walimtupa au nae walimpeleka kuwa chakula cha mamba?

Hadi leo ni miaka 2 tangu Sativa atekwe na hakuna aliyekamatwa na Polepole sasa katimiza mwaka hakuna hatua yoyote , msikilize hapo Sativa akieleza alivyotekwa.


View: https://www.youtube.com/live/5GhS9HSzdrw?si=SgsAHzGZ_78zoHq-
 
NIMEITAFUTA HII MAKALA SANA...Sasa wewe Britanicca ni bora ulitake radhi ili jukwaa kabisa
 
😢😢😭😭
 
😢😢😭😭

Na ndio kimetokea kwa Twaha , kama tusipomuona ndani ya siku tatu toka sasa hawa vibaka ndio watakuwa wamempoteza kwa mtindo huo.

Walifeli kwa Mshabaha na Maria kuwavusha border sasa naona wanataka wawamalizie kwa kushikirikiana na majambazi wa Kenya.
 
Inasikitisha sana, 😢😭
 
Dah ila watanzania tunaperekeshwa aisee

Hivi kuna kipindi watu walikuwa wananyimwa huduma ya internet kisa polepole anaongea 💔

I don't know what happened to my beautiful mamaland
 
Sasa hapo huyo ni kiongozi au ni uozo? Kama anaingizwa chaka kiboya namna hiyo kwenye jambo obvious kama hilo vipi kuhusu mikataba yenye complexities kibao za cooperate laws, international laws, binding agreements na mambo mengine kibao ya kitaaluma si ndiyo anapotezwa kabisa.
 
Huko naomba usiongee!, ni madudu matupu!, ila huko naomba kumtetea kwasababu ni professional ya watu, mtu ukiwa sio professional fulani, hutegemewi kujua complex issues ya professional husika, utategemea wasaidizi wako ambao ni ma pro.

Nimetokea kosomea sheria, LL.B yangu pale UDSM, pale ni sheria kweli!, ila huku serikalini kuna wanasheria vilaza wa ajabu, wanafanya madudu ya ajabu ya kisheria, simlaumu Mama, ila nawalaumu waalimu wangu watatu walionifundisha pale UDSM kisha wakaingia serikalini, kitu cha ajabu sana ni nao pia baada ya kuingia serikali, wakawa vilaza wa ajabu!.
  1. Mama amechukua nchi, akaikuta ina katiba ilionajisiwa kwa kuchomekewa ubatili, mtu asiye mwanasheria hawezi kuujua ubatili wa katiba na sheria bila msaada wa wanasheria. Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
  2. Wasaidizi wake sheria wanajua NEC ni zao la katiba, huwezi kuivunja NEC na kuunda INEC kwa mabadiliko ya kawaida ya sheria bali ni kwa mabadiliko madogo ya katiba. Hili halikufanyika!.
  3. Sheria ya uchaguzi mama aliyoikuta ina ubatili, ambao uliishabatilishwa na mahakama kuu ya Tanzania, mama akatungiwa sheria mpya yenye ubatili ule ule!,
  4. Kitu cha ajabu ni muswada huo batili, umetungwa wakati profesa wangu mmoja mzuri sana ndio waziri wa sheria, profesa wangu mwingine ni katibu mkuu, profesa wangu mwingine ni jaji mkuu, na mwalimu wangu mwingine Daktari ni Spika wa Bunge, na madudu hayo yakapita mikononi mwao! Barua Wazi ya Mwanafunzi kwa Walimu Wake Wawili. 1 ni kwa Dean wake, na 2. TA wa Kipindi chake c Kwanza. Please Watendeni Watanzania Haki Hii!.
  5. Mwanasheria mahiri aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya sheria, japo aliujua ukweli, akaufungia macho, akijua ndio anamtendea mema mama, akikatiliwa mbali kurejea bungeni!.
  6. Dada yangu, ambaye ni mwanasheria nguli, mbobezi na mbobevu, alijua ndio anakibeba chama chake, naye kwenye usipika wakamchinjia baharini sasa ni back bencher!.
P
 
Vitu vingine vinahitaji tu commonsense kufahamu kuwa mambo hayako sawa, kuwa haki haitendeki, kuwa katiba haifuatwi na kuwa raia wanataka serikali iliyochaguliwa kihalali, kuwa ili tuheshimike internationally lazima tujiheshimu sisi wenyewe kwanza, kuwa kusifiwa na chawa huku tukiendelea kuharibu hakulisaidii taifa hivyo basi tatizo linaanzia kwenye mfumo mzima, vetting, the current TISS pia ni tatizo kubwa mno kwani uozo wote unaoendelea wangekuwa ni wazalendo kwa taifa usingekuwa ukitokea.
Rais mwenye nia njema kwa mustakabali wa taifa hawezi kuua raia recklessly na kusababisha mpasuko usio wa lazima akibaki kutegemea kuteka, kubambikia kesi na kuua kila anayekuwa na mawazo mbadala. Nchi inaongozwa na majangili, mafisadi na sadly ni watu ambao hawana nia njema kwa taifa zaidi ya kujali maslahi yao binafsi na ya close associates.
As a nation, we're doomed.
 
Huu mkeka alichana yanga
 
Kuna angle namzimia sana mama! She teaches us lessons and we don't learn! Wewe unamshughulikia mtu huku anaandaliwa mwingine wa kukushughulikia wewe!

She will change this country for good.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…