Hivi hawa ambao kila siku wanaporomosha Maghorofa ya Kupangisha DSM hali hii ngumu hawaioni au watapangisha Kuku?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Katika Watanzania 500 badi 457 wanalia hali mbaya ya Uchumi a.k.a Vyuma Vimekaza halafu hapo hapo tena kuwa Watu wanathubutu kabisa Kujenga Maghorofa makubwa makubwa ya Kupangisha ( Apartments ) hivi humo wanategemea Kupangisha Binadamu au labda wataweka tu pengine ' Mifugo ' yao kama Kuku, Bata, Mbuzi na pengine hata Ng'ombe?

Kazi ipo hakyanani!

Nawasilisha.
 

Mkuu kwa waliokuwa nazo toka mwanzo wataendelea kuwa nazo hakuna kilichobadilika kwao na watu watapanga vilevile ila rate imeshuka ya upangaji tofauti nazamani mkuu Hali mbaya kwa tabaka la Kati na lachini kabisa sio kwa tabaka lajuu
 
Ukifuatilia kwa kina utagundua kuwa biashara zimedoda, watu hawana pa kuwekeza, maana ukiweka bank unaweza jikuta zimebebwa bila maelezo kwa kisingizio cha kujipatia fedha kwa njia isiyohalali au wakasema unatakayisha fedha, sehemu sahihk na salama akbayo matajiri wengi wanaona bora wahifadhi pesa zao no kwenye majengo, wakiizika pesa hapo itakuwa salama kuliko benki, fuatilia utaona ni matajiri wengi wanajenga nyumba sasa, si kwamba wanapenda ila ni mbinu mpya ya kuhifadhi pesa.
 
Apartments nyingi zinapangishwa na watu wa nje, wafanyakazi wa balozi, wafanyakazi (leaders) wa makampuni makubwa na wahindi.
 

Kuna Mzee mmoja ametokewa na hiki hiki ulichokisema hapa, sasa ni mwaka wa pili huu tayari jina lake la Ubatizo wa Kudumu la ' Marehemu ' linaanza Kuzoeleka.
 
wateja wapo kaka.. nilienda sehemu tabata kumsindikiza ndugu yangu.. apartment kodi laki 5 kwa mwezi... na tukaambiwa tumechelewa zimejaaa

Tafadhali nifikishie ' Shikamoo ' yangu kwa hao ' Wapangaji ' wa Tsh 500,000/= kwa Mwezi na hasa kwa usawa huu wa JPM.
 
Hakika hali ni ngumu hata hao wanao panga kwenye hizo apartments kodi sio sawa na ila ya awamu ya JK awamu hii imeshuka
 
Si wote wanamaisha magumu,wengine kwa sasa wanamaisha mazuri kuna wengine vyeo vyao vimepanda na maslai pia yameongezeka; kuna 'principle' anapoumia mtu, ujue mwingine ananufaika;katika hali ya kawaida hakuna kazi ya kujitolea,lazima itakuwa na faida kwa kiasi fulani.
 
Fedha inashuka thamani, Biashara hazifanyiki... Purchasing power imeshuka..

Sehemu pekee ya kuhifadhi Fedha either ikabaki kwenye value yake au kuongezeka ni kwenye real estates.. Hata asipopata wateja sasahv atakuwa na running cost ndogo tu za kutunza jengo lake lakini fedha yake itakuwa iko sehemu salama
 
Kuna rafiki yangu kaajiriwa mwaka huu mwanzoni juzi amenunua Passo nikampigia kumpa hongera nikamwambia "Kaka naona mambo siyo magumu kabisa" akajibu "Nasikia sikia tu watu wanadai maisha magumu ila mi siamini" alinifurahisha sana.
Sasa Paso ni gari ya kuiongelea mbele ya wanaume hadharani?

Huyo jamaa yako ana akili kubwa ametafuta access ya kufika kazini kwa wakati na asipate adha wakati wa kurudi kazini. Baada ya hapo huwezi kukaa na wanaume kuiongelea Passo.
 
Long term investment. The Rich makes money when the economy is on the up AND when the economy is on the nosedive!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…