Hivi hawa DSTV wanatuchukuliaje Watanzania?

Hivi hawa DSTV wanatuchukuliaje Watanzania?

Mtanzania utamjua kwa majibu yake ya kitumwa! Mtumwa ndiye ukimuuliza kwa nini hutembei kufurahia maisha kama watu wengine anakumbia ''bwana anakataza''! Bila shaka wewe exposure yako ni sifuri na pia elimu yako imedunda! Biashara haihalalishi wafanyabiashara kufanya watakavyo!
Wanapenda kukubali kuonewa, kukandamizwa na kupunjwa under the name of "hewala bwana wacha tu nifunike kombe mwanaharamu apite".
 
Salaam WanaJF!

Hivi hawa jamaa wa DSTV (Multichoice) wanatuchukuliaje Watanzania!? Kwamba wanatuchukulia tupo vizuri sana kiuchumi, ama wanatuchukulia sisi washamba sana au inakuwaje!?

Kila siku wanafanya kuzichezesha chaneli zao ndani ya DSTV, sio kitu cha ajabu kukuta chaneli yako pendwa imehamishiwa katika kifurushi kingine ambacho ni cha gharama zaidi.

Yaani Kifurushi cha COMPACT ambacho tunalipia Tsh 50000+ kwa mwezi nacho kimeshakuwa useless, chaneli pendwa wamezisogeza kwenye kifurushi cha COMPACT plus ambacho unatakiwa kulipia Tsh 90000+ kwa mwezi.

Huu ni utapeli kwa Watanzania, sijui mnatuchukuliaje DSTV!!?
hamia kwenye king'amuzi ambacho una uwezo nacho
 
Mimi nimelipia Tuesday na S3 ipo kwenye COMPACT
Okay, labda kipindi unalipia bado ilikuwa kwa Compact package, huu uzi nimeupandisha hapa jana (Alhamis), huenda kuna mabadiliko wameyafanya Jumatano au Alhamis!
Nafikiria kulipia hivyohivyo, nikifanya hivyo nitaleta mrejesho hapa.
 
Mtanzania utamjua kwa majibu yake ya kitumwa! Mtumwa ndiye ukimuuliza kwa nini hutembei kufurahia maisha kama watu wengine anakumbia ''bwana anakataza''! Bila shaka wewe exposure yako ni sifuri na pia elimu yako imedunda! Biashara haihalalishi wafanyabiashara kufanya watakavyo!
Yaani acha tu mkongwe, yaani inashangaza sana. Nilijua ni mimi tu nimeliona hili. Mtu anakuambia kirahisi tu "kama unaona gharama hauziwezi tafuta king'amuzi kingine" huko kwenye king'amuzi kingine ni wafanyabiashara pia, nao wakiamua kufanya uhuni? Si nitakuwa nafanya kazi ya kununua ving'amuzi tu kila mara. 😂😂😂😂
 
kipind cha olimpic kile kuna channel wakaziamisha m nalipia kile kifurush cha 31k wakaziamisha channel ad kifurush cha 51k

nikawapigia wakanipa maelezo nikaona siwaelew coz nisharipia then wik mbil mbele ndio wanaamisha channel

nikawapigia tcra wakanipa muongozo niwatumie email hao dstv ya malalamiko yangu then niwa cc na tcra

nikafanya hvyo mbona adi inafika jion wakazirudisha chennel zote

wengne walikua wale zuku faiba nao nimeripia kuja kufunga nipate huduma ya internet ofisin wakawa wananipiga carenda nikaona sio inshu

nikawavutia waya tcra wakanipa maelekezo kama hayo ya mwanzo mbona kesho yake tu wakaja mafund huku wakiwa wamesisitizwa wafanye kazi kwa ubora
 
Dstv wanazingua sana, yaan wanafanya watakavyo, mi nnatumia kfurush cha elf 21, Mara chanel ya wrestling waweke mara watoe, ile ya premer leage mara wa weke mara watoe yaan vululu vululu
 
nunua dishi la free to air wala hautalipia hata senti au nunua decoda ya canal+ bei zao kitonga na unaona ligi zote za ulaya na movies za kutosha kwa 30000 tu ila lugha kifaransa
Yanapatikana wapi
 
Nmelipia trh 29/03/2022
Leo ni tarehe 15 mkongwe, malizia package yako kwanza halafu tutapeana mrejesho baadae, au tuombe kabla ya package yako kuisha wawe wamepokea malalamiko na kuyafanyia kazi.
 
Leo ni tarehe 15 mkongwe, malizia package yako kwanza halafu tutapeana mrejesho baadae, au tuombe kabla ya package yako kuisha wawe wamepokea malalamiko na kuyafanyia kazi.

Mzee acha mbwembwe, we lipia hiyo 51,000 then utatupa mrejesho hapa hapa.
 
King'amuz Cha azamu kipo tafuta bar yakuangalia sinema zako au mpira. Unanunua kitu huwezi kukihudumia channeli zandani karibu 20 mnaangalia bure wezenu wafanyaje biashara tambua hao hawatoi huduma wako biashara zaidi
 
Mzee acha mbwembwe, we lipia hiyo 51,000 then utatupa mrejesho hapa hapa.
Hivi bhachu, umeelewa hata ninachozungumzia? Kabla sijalipia nina kawaida ya kucheki mtandaoni vifurushi vimekaaje, ili kama kuna mabadiliko nijue. Sasa nimecheki nimekuta kifurushi cha Compact hakina channel ya Supersport PL.
Screenshot_20220415-080725.png


Wewe unasema nilipie tu kwasababu kwako ipo, haya nalipia nisipoikuta hiyo channel yangu pendwa inakuwaje? Pia kumbuka wewe umelipia kifurushi muda mrefu, kifurushi chako bado hakijaisha, inawezekana ndio maana bado unaiona hiyo channel.
 
Lakini siku hizi kifurushi kikiisha Al Jazeera unapata na chanel nyingine nyingi tu, ile zile pendwa za muvi hupati
Labda hivyo visimbuzi vingine sio dstv.
Hapa wamekata zote wameacha ile ya matangazo na tbc tuu.

Zile za kibongo kama eatv, clouds, chanel ten na upendo tv nadhani wanakuachia kwa muda tu kama 2weeks hivi.
 
Labda hivyo visimbuzi vingine sio dstv.
Hapa wamekata zote wameacha ile ya matangazo na tbc tuu.

Zile za kibongo kama eatv, clouds, chanel ten na upendo tv nadhani wanakuachia kwa muda tu kama 2weeks hivi.
Basi kwangu ni tofauti, huwa nizikuta zipo kifurushi kikikata
 
Basi kwangu ni tofauti, huwa nizikuta zipo kifurushi kikikata
Ni kawaida ya dstv kifurushi kikikata wanapunguza channel chache chache kwa muda flani.

Huenda wewe huwa unalipia mapema kikikata. Ila ukikaa kitambo kidogo zinafurushwa zote unabaki na tbc na matangazo.
 
Wewe unaonaje mkuu. Maana ukiachana nao hutaingia hizo gharama. Tafuta alternative maisha yaendelee.
Kama ingekuwa wanakubali uwarudishie king'amuzi chao na warudishe pesa ingekuwa vizuri sana, maana kuachana nao maana yake ukatafute kwingine !!
 
Back
Top Bottom