Hivi hawa masai wanaotembea wakiuza dawa ni za kweli au matapeli?

Hivi hawa masai wanaotembea wakiuza dawa ni za kweli au matapeli?

Mcqueenen

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
6,843
Reaction score
11,702
Hola Amigos,
Jana nmekutana na mmasaai anatembea akiuza dawa mbalimbali kwenye kigunia, alikuwa ameshikilia kama kimenu cha dawa alizonazo na bei zake, ukikutana naye haongei sana anakupa kipeperushi tu.

Baadhi ya dawa nlizoziona kwenye menu
Mkongo puturu-10,000
Mkuyati-15,000
Dawa ya mapenzi(kutongozea)-25,000
Nk. Nk. magonjwa mengine…

Hivi hizi dawa za hawa jamaa zina ukweli wowte au ni utapeli tu mjini?
 
Unaonaje ungenunua hizo dawa, as a part of your research.

Then ukaja na majibu?
 
Wanazo dawa mpaka za kuongeza nguvu za kiume, tena unakunywa palepale wanakozitembeza kwenye galoni na kikombe. Swali, wanajuaje hizo dawa zina kemikali zinazotakiwa kuimarisha mwili, au ni kunywa uchafu na sumu? Wengine wanauza mpaka mavi ya tembo kabisa, lile tofali la duara alilotoa tembo likiwa limejaa vipande vya mitimiti, wengine huwa tunalitumia kuwashia moto na hata kupikia chakula kama kuni
 
Ila hizi dawa za kienyeji zingine zinatia shaka utendaji kazi wake mwilini. Kuna mkojo wa binadamu uliovunda unatumika kuoshea vidonda kichwani na upele. Kuna pia mavi ya nyoka na wanyama wengine bila kusahau mafuta ya nyama zao hutumika kama dawa za kienyeji. Uchafu mtupu
 
Kwahiyo wewe akili ya kufikiri huna? Mpaka dawa ya kutongozea serious?
watu wanapewa mpaka dawa za kupendwa na wapenzi wao. Unakuta mtu anatembea na ka mzizi akitamani mtua anakatoa alikokahifadhi anaanza kukatafunatafuna
 
Dadadadeki maasai ni kabila la hovyo sana tumewapa Imani hadi wameamua kukufuru hio imani.
 
Hahaha

Anakuambia nna kijiti sijui jani, ukikitafuna tu kila dem ukimtongoza
Hachomoi

Ova
Kwahiyo wewe akili ya kufikiri huna? Mpaka dawa ya kutongozea serious?
Wakuu,

Hizo dawa zipo. Ila si dawa asili, bali ni ya kiganga. Tuseme ni hirizi inatenengenezwa na Waganga.

Siyo kijiti, hapo wanakupiga tu. Ni dawa ya kujipaka kwenye paji la uso na mikononi pale unapokuwa na uhakika wa kushikana mikono na mhusika.

Ni uchawi wa kumkamata unayemtaka. Na hizo dawa si rahisi kila mtu kuwa nayo. Maana ni ghali huko na hawatoi kwa sababu zinachochea sana chuki ndani ya jamii.

Hao wanawapiga hela tu. Ila haimaanishi hakuna.
 
Dadadadeki maasai ni kabila la hovyo sana tumewapa Imani hadi wameamua kukufuru hio imani.
Mkuu,

Sema wauza dawa. Kuhusisha kabila zima kwa sababu ya watu kadhaa si jambo jema.

Jiulize, hiyo imani imekujaje? Maana yake hapo kabla walikuwa wanatoa dawa na zinafanya kazi barabara.

Dunia imebadilika kutoka kutoa toba na badala yake kuvuna hela kutoka kwa wahitaji. Nao wakaingiwa na tamaa ya pesa na wingi wa wahitaji wakaanza kuuza dawa za hovyo.
 
Dadadadeki maasai ni kabila la hovyo sana tumewapa Imani hadi wameamua kukufuru hio imani.
Wamasai ni kabila linaloenzi tamaduni zao sio inferior kama makabila mengine yanayorubunika na tamaduni za kigeni.

Ni kabila pekee ambalo linaishi kwa kufuata kanuni za makundi katika jamii.

Kila kundi la umri Lina majukumu yake maalum.

Madawa yapo mengi sana na yanatibu ila kuyapata Kuna namna Huwa yanapatikana.

Madawa huufanya mwili kuwa imara na usiopata madhara ya magonjwa madogo madogo kila mara.
 
Mjini hakuna shamba wala pori, Shamba ni kichwa chako mwenyewe alisikika mlevi mmoja akisema
 
Back
Top Bottom