HIVI HAYA MADUDE BADO YAPO ??

Tunakoment hapahapa mwaya ....plus rede kombolela na madange
Sent using Jamii Forums mobile app
Kombolea nimecheza sana kwa jirani kulikuwa na jirani yangu sa kipindi cha likizo watoto wa shangazi, mjomba wanaenda kama likizo kwa huyu jirani yangu sasa kulikuwa na vitoto vya kike vizuri haha, nilivila sana mnacheza mkichoka kila mmoja anaenda kujificha na wake wee.. utoto raha sana
 
Secondary [emoji16][emoji16]ulchelewa mkuu..ilo la primary, seco unanaza na gameboy,gameboy advance na sp,unasogea sega pale by unaanza advance unajua atleast ps 2,sikuhizi ps 4
Sent using Brain
Hom mzee alikuwa hataki kusikia mambo ya game, akikunyaka, hom bro alikuwa na pc siku mzee kalifuma alii pasulia ukutani, mda wote kama huna kazi uwe na kitabu na siyo pc
 
Kipindi hamna simu za mikononi nilinunuliwa kiredio(hakina spika) kidogo kina hilo dude sasa nikichomeka headset nacheza hilo dude huku nakula masongi hunambii kitu.
 
Kuna kaka yangu niliyemfuatia mimi. Miaka ya 1990's mwishoni huku alikuja nayo home. Akawa ananibania kulichezea. Nikim'mind naambiwa mkorofi nalilia kitu sio changu. Ila ndugu zangu wakubwa anawapatia wanachezea wanavyotaka.

Nikimuomba usiku muda amelala nichezee kidogo ananiambia muda umeenda analiweka lipumzike na betri zinaisha chaji sana usiku sababu hakuna jua


Nikaona huyu bwege hanijui huyu nitamkomesha sote tukose. Nikavizia kuona huwa anaficha wapi maana alikuwa hataki nijue baada ya kunikuta siku moja nimelichukua nachezea akaanza ficha kwa tahadhali nisijue anapoweka.

Siku hiyo nikawahi kulala, yeye akiwa sebuleni analichezea na ndugu zetu wakubwa. Me nikajikausha kama nimelala. Muda ukaenda akaingia nikamuona anapanda juu ya kabati anaficha kwenye box. Nikashema shenzi wewe kwisha janja yako kesho utahadithia kima wa kilimani.

Nikalala kwa ugwadu nikisubiria kukuche nimshikishe adabu. Asubuhi ilipofika tukasepa shule ila mimi huwa nawahi kurejea. So nikarudi fasta home, break ya kwanza juu ya kabati. Nikaikuta. Shenzi, nikaichukua nikatafuta screwdriver nikaifungua. Kwa kutumia nail cutter nilikata vidude viwili tu vile vinakuwa vimechomelewa katika motherboard. Kisha nikarudishia kama nilivyoikuta.

Yule bwege alivyorejea baadae akachukua kuiwasha inawaka ila kuna button hazifanyi kazi, ikiwamo ile kubwa na ile ya kupeleka upande wa kushoto. Technically kidude kikawa hakifai.

Akajitia kulalamika akinituhumu kuwa nimeharibu nilimjia juu kama askari wa ffu. Nikamgombeza kuwa wewe hilo takataka lako lini umenipa nichezee si kila siku unaninyima na huwa unaenda nalo shule. Akajidai huwa naiacha nikamwambia sasa mimi ndio huwa nakushikia au unataka kuleta za kuleta?!

Hadi b mkubwa akamkata akasema ila wewe kila siku mdogo wako nasikia analalamika unambania kuchezea leo imeharibika unasema ameharibu yeye na huwa hagusi hata kidogo.

Picha likaisha hivyo nikiwa na ushindi wote tumekosa na yeye hachezei tena likitu lake pumbavu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha, hii family feud ilikuwa ni kibokooo.
 
dah aisee hili dude ni shida zaidi ya mchezo wa ku bet
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] mkuu mlikuwa mnafatana kuzaliwa sio?
 
Tuliokulia tunacheza hivi tunakomenti wapi?View attachment 1061362
😃😃Dah mlikuwa mnalembua mnaporusha jiwe juu na kulisubiri lishuke.
Malcom Lumumba ilikuweje mtoto wa kike alikupita kwenye hii game,wakati enzi hizo lilikuwa habari ya mjini,nakumbuka kuna jamaa alikuwa anakodisha kwa 200 sasa mzee akanikuta nakesha nalo usiku silali,ikabidi aninunulie,mitaa yetu ilikuwa buku jero tuu.
 
Kipindi hiki hili dude limenikuta mkubwa kidogo, nilikuwa napambana na mambo ya masomo bwana. Japo Game nimecheza sana ila siyo hili Brick Game na msauti wake mbayaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…