Kuna kaka yangu niliyemfuatia mimi. Miaka ya 1990's mwishoni huku alikuja nayo home. Akawa ananibania kulichezea. Nikim'mind naambiwa mkorofi nalilia kitu sio changu. Ila ndugu zangu wakubwa anawapatia wanachezea wanavyotaka.
Nikimuomba usiku muda amelala nichezee kidogo ananiambia muda umeenda analiweka lipumzike na betri zinaisha chaji sana usiku sababu hakuna jua
Nikaona huyu bwege hanijui huyu nitamkomesha sote tukose. Nikavizia kuona huwa anaficha wapi maana alikuwa hataki nijue baada ya kunikuta siku moja nimelichukua nachezea akaanza ficha kwa tahadhali nisijue anapoweka.
Siku hiyo nikawahi kulala, yeye akiwa sebuleni analichezea na ndugu zetu wakubwa. Me nikajikausha kama nimelala. Muda ukaenda akaingia nikamuona anapanda juu ya kabati anaficha kwenye box. Nikashema shenzi wewe kwisha janja yako kesho utahadithia kima wa kilimani.
Nikalala kwa ugwadu nikisubiria kukuche nimshikishe adabu. Asubuhi ilipofika tukasepa shule ila mimi huwa nawahi kurejea. So nikarudi fasta home, break ya kwanza juu ya kabati. Nikaikuta. Shenzi, nikaichukua nikatafuta screwdriver nikaifungua. Kwa kutumia nail cutter nilikata vidude viwili tu vile vinakuwa vimechomelewa katika motherboard. Kisha nikarudishia kama nilivyoikuta.
Yule bwege alivyorejea baadae akachukua kuiwasha inawaka ila kuna button hazifanyi kazi, ikiwamo ile kubwa na ile ya kupeleka upande wa kushoto. Technically kidude kikawa hakifai.
Akajitia kulalamika akinituhumu kuwa nimeharibu nilimjia juu kama askari wa ffu. Nikamgombeza kuwa wewe hilo takataka lako lini umenipa nichezee si kila siku unaninyima na huwa unaenda nalo shule. Akajidai huwa naiacha nikamwambia sasa mimi ndio huwa nakushikia au unataka kuleta za kuleta?!
Hadi b mkubwa akamkata akasema ila wewe kila siku mdogo wako nasikia analalamika unambania kuchezea leo imeharibika unasema ameharibu yeye na huwa hagusi hata kidogo.
Picha likaisha hivyo nikiwa na ushindi wote tumekosa na yeye hachezei tena likitu lake pumbavu.
Sent using
Jamii Forums mobile app