Hivi HESLB waliongeza mikopo kimya kimya kwa baadhi ya wanafunzi?

Hivi HESLB waliongeza mikopo kimya kimya kwa baadhi ya wanafunzi?

Mwenyezi Mungu anijalie uzima na afya tele ili nije kuwasomesha watoto wangu kwa fedha zangu za mfukoni, na siyo kwa kutegemea hii Bodi ya Mikopo, ambayo kimsingi ni jipu kwa wale wanufaika waliofanikiwa kurejesha mkopo.

Maana kubambikiwa deni ni nje nje. Sitokubali kuona watoto wangu wakifanyiwa huu ujinga.

Yaani unaandikiwa mkopo wa kulipa, unalipa mpaka deni linaisha! Halafu baadaye unaletewa makato mengine kutoka kusikojulikana, na kutakiwa kulipa tena!
 
Kwanza niseme kabisa hatutachoka kudai pesa yetu halali inayotokana na madai ya kurejeshewa kiasi kilichozidishwa kwenye makato wakati wa urejeshaji wa deni la mkopo pindi tukamilishapo urejeshaji deni lote.

Hawa wahuni wa Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu wamekuwa na kawaida ya kuendelea kuwakata wanufaika kupitia mishahara hata baada ya kukamilika kwa marejesho.

Ukikamilisha kujisajiri kwenye Akaunti yao ya Loan Refund wanakwambia subiri ndani ya siku 90 kumbe hiyo ni lugha tu ya kukuondoa ofisini kwao. Ukifuatilia baada ya siku 90 kupita wanaendelea kukuzungusha.

Ukifika pale ofisi zao za Dar au za kanda mnajikuta wenye tatizo hilo mko wengi sana. Ukiwapigia namba yao ya mawasiliano hata siku moja haipokelewi. Prof Mkenda jaribu kuwapigia uone. Hivi hata hili tumkumbuke jamani marehemu JPM?
Kwani wakati wa JPM hilo tatizo halikuwepo?
 
Dogo mwanzo alipata asilimia 58,

Now kaongezewa Ana 100
 
Back
Top Bottom