Hivi HESLB waliongeza mikopo kimya kimya kwa baadhi ya wanafunzi?

Mwenyezi Mungu anijalie uzima na afya tele ili nije kuwasomesha watoto wangu kwa fedha zangu za mfukoni, na siyo kwa kutegemea hii Bodi ya Mikopo, ambayo kimsingi ni jipu kwa wale wanufaika waliofanikiwa kurejesha mkopo.

Maana kubambikiwa deni ni nje nje. Sitokubali kuona watoto wangu wakifanyiwa huu ujinga.

Yaani unaandikiwa mkopo wa kulipa, unalipa mpaka deni linaisha! Halafu baadaye unaletewa makato mengine kutoka kusikojulikana, na kutakiwa kulipa tena!
 
Kwani wakati wa JPM hilo tatizo halikuwepo?
 
Dogo mwanzo alipata asilimia 58,

Now kaongezewa Ana 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…