Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Dah..kwa hili la kusikia harufu....usikute Dar nzima tunaumwa uviko ila hatujijui 🤣🤣🤣🤣🤭
 
Tena pale Makumbusho Stend ndio sitaki kupasikia.
Pananuka utadhani nini. Nusura Nitapike lakini ajabu ni kuwa Mimi pekee ndiye niliyeonekana kukerwa na harufu Ile watu wengine hata hawana habari
Unamanisha Michael Jackson angetua bongo angesemaje khs jiji kunukia?
 
Ndio maana wana darusalama mnapenda kuzibuana mitaro ya maji machafu kumbe mnaishi pahala panukapo na harufu mmeizoea
 
Sijafika huko Mkuu Ila nitaenda.

Maeneo mengi Yananuka hasa Maeneo ya Stend za Daladala.

Kesho nitakuwa na ziara ya Maeneo ya Posta yote, Feri, Upanga, na Kidogo Namanga
Hili wengi watakubishia na wana haki ya kufanya hivyo. Wana haki kwa sababu bila mtu kusafiri nje ya Tanzania na kwenda nchi zilizoendelea utakuwa unadhani Dar kila kitu kipo sawa. Haya uliyoandika kuna watu watadhani ni utani lakini mimi nimeyashuhudia mara nyingi. Ukitoka sehemu kama Ulaya ukifika Dar vitu vifuatavyo ni dhahiri. 1. Harufu mbaya (jiji lote) 2. Watu wachafu kupindukia. 3. Watu, Nyumba, magari na kila kitu viko disorganized.
 
Harufu imekithiri kweli ila sio Dar tu hata Nairobi pananuka kwa kweli

Ila hiyo mitaro naona inafukiwa vingi sio kinyesi tu labda na watu pia maana sio kwa harufu hiyo
 
Sawa Bhana mtu wa DAR. Wewe si ndiye Shemeji YANGU wa Tandale.

Jaribuni kuwa wasafi hata kidogo.

Vijana wadogo mmeathirika kisaikolojia kisa harufu za Chemba za maji taka.

Pumbavu
Ahhahaha
 


Na watu wameathirika kisaikolojia.

Wanahasira na kupayuka payuka tuu
 
Harufu tumeshaizoea sisi, tena ukiziba pua watu wataona unajisikia. Ila usijali, ndani ya muda mfupi na wewe utaizoea Harufu yetu pendwa.

Karibu tena Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…