Hivi hii kanuni ya biashara ni kweli mwenye duka hakupi kitu bila hela asubuhi mpaka auze kwanza?

Hivi hii kanuni ya biashara ni kweli mwenye duka hakupi kitu bila hela asubuhi mpaka auze kwanza?

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Habari.

Mi mwenzenu sijui nikoje haya maimani ya ajabu ajabu yananipa shida sana huku duniani yaani huwa hata siwazagi haya mambo.

Sàsa mimi nina ela yangu msimbazi safi nahitaji kitu kwenye duka chenji hana na mimi kutembea na hela ndogo ndogo siwezi namwambia mwenye duka nasi nipe bidhaa takuletea badae hela anasema siwezi kukupa bado sijauza biashara itadoda.

Hebu wajuzi mje mtujuze hii formula ya biashara ni kweli inafanya kazi hawa wenzetu wa maduka.??!
 
Hii si kanuni bali ni imani na imani siyo lazima iwe sahihi, ni sahihi kwa yule anayeamini tu ndio maana kwa mfano asiyeamini uchawi hauwezi kumdhuru. Biashara ni sayansi mimi sioni uhusiano wowote wa kufeli au kufanikiwa biashara na imani za namna hii, ni kupoteza muda tu kuanza kuzifikiria. Wenye biashara wapo wanaoamini hizi imani na hata wateja pia wapo wanaoamini.
 
Nasikia kumbe hata wahindi wana hii imani ukienda kukopa asubuhi anakufukuza tena kwa hasira.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Kuna Duka zamani nikiwa mtoto nikaambiwa kanunue chumvi lakini usiseme chumvi hawatakupa..
Nilishangaa Sana eti sema dawa ya mboga...
Nikasema chumvi Kwa kusudi ..jamaa walini mind Sana dukani... walinipa shingo upande
 
Kuna wale dukani ana droo za kutosha na vipochi hata viwili lakini hela unampa anaenda tumbukiza kwenye ndoo....hii nchi ngumu sana
 
Kwanini uje ukope kwangu kwani duka langu la mkopo......! Kwendraaaaa.....nenda microfinance huko uone nako kama watakutimuia!

Tunataka wateja siyo wachawi
 
Back
Top Bottom