Hivi hii misimamo na mahaba ya namna hii huwa mnayatoa wapi?

Hivi hii misimamo na mahaba ya namna hii huwa mnayatoa wapi?

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,994
Reaction score
4,446
Katika ukuaji wangu Kuna Imani na misimamo nikimuona nayo mtu nabaki namshangaa kabisa

Kwa mfano;
Hivi inawezekanaje kuwa chawa wa mtu kiasi Cha kushindwa kuona mabaya take?🤔

Hivi mtu unawezaje kujidhuru kwa ajiri ya mapenzi ?🤔

Hivi kipi kinacho Mfanya mtu anashindwa kumuamini Mungu au Maandiko yake matakatifu lakini mtu huyo huyo anajenga Iman yake juu ya binadamu mwenzake ?🤔

Kuwa mrahibu wa kitu fulan mf mpira yaani mtu anakosa amani furaha na utulivu wa akili kisa tu timu fulani imefungwa?🤔

Ebu nielezen ndugu huwa mnafanya Nini Hadi kufikia hatua ya kuwa na Iman za namna hyo
Kwasababu Mimi binafsi katika maisha yangu siwezi kuendeshwa na kitu kimoja

Never
 
Kuna nafasi huwa haijazwi na chochote zaidi ya mapenzi ya mtu kwa kitu au vitu Fulani.

Mapenzi haya yakizidi yanazima Mtandao na hapa ndipo utapata mtu anayechukia Nguruwe bila sababu au kumuona adui asiyekuwa upande wake

Mapenzi unafki sugu.
 
N umaskini tuu.
Umaskini wa Kipesa na akili.

Sasa kama unamtu wa kumsujudia then anakutoa kwenye huo umaskini wako Kwann usijifanye mpumbavu ili uneemeke.
Mm nawaunga mkono, hawana namna 😂
 
Hakuna kitu kinachoitwa Mungu ndiyo maana nashindwa kumwamini.

Si lazima mtu asipomwamini mungu (ambaye hayupo) anamwamini mtu kama unavyodai.
Ni sawa ulisemalo unaweza husimuamini Mungu yule wa Isaka na Jacob lakini ukawa na mungu wako labda aitwaye mwamarundi, kazobha kanyamuhanga,kipembe nk lkn je vipi kuhusu kuwekeza Iman yako kwa mtu anayeonekana kiasi kwamba hasipotamka jambo juu yako ww huwez kuamua chochote juu ya maisha yako?
 
Hapana Mkuu ata sijahi kuwaza kujaribu
Mimi nilishajaribu aisee ina uraibu mbaya Sana,Yaani hulali usiku kwa Amani kama mechi zako hazijachezwa,unaweza kuamka usiku WA manane ukaanza kusuka mkeka😀😀😀😀😀
Uko zako kanisani Tu kolea tunacheza mechi zao asubuh asubuh ukitoka Tu mlango WA kanisa cha kwanza kuwasha data uchungulie mkeka kama unapumua 😀😀😀😀😀
 
Ni sawa ulisemalo unaweza husimuamini Mungu yule wa Isaka na Jacob lakini ukawa na mungu wako labda aitwaye mwamarundi, kazobha kanyamuhanga,kipembe nk lkn je vipi kuhusu kuwekeza Iman yako kwa mtu anayeonekana kiasi kwamba hasipotamka jambo juu yako ww huwez kuamua chochote juu ya maisha yako?
Sasa hapo ni jinsi mtu alivyotune akili yake mkuu.

Kumbuka kuwa mtu asiyependa kufikiria kivyake huamini chochote aambiwacho na yule (mtu) amwaminiye.

Ndiyo maana kwenye matangazo ya kibiashara watu maarafu mathalani wasanii, wachezaji n.k hutumiwa kunadi bidhaa Ili watu wanaowashabikia hao watu maarufu wanunue bidhaa hizo.

Binadamu wengi hawatumii akili zao ndo maana ni rahisi kutekwa na wale wajanja wachache e wanaotumia akili zao vizuri.

Zumaridi na Mwamposa endeleeni kuwanyoosha wabongo 🔥.
 
Sasa huo si ndo uzwazwa wenyewe
 
Back
Top Bottom