Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Tarehe 09 Desemba 1961 ni siku ambayo bendera ya Tanzania (Tanganyika) ilipandishwa kuashiria nchi huru yenye kujitawala na kujiamulia mambo yake bila kuingiliwa na taifa lolote la nje.
Leo tunakaribia miaka 61 ya uhuru lakini bado wananachi wa Tanzania wanaishi kwa kudra za watawala. Bado uhuru wa Watanzania haujawa defined na kufikiwa katika uhalisia wa uhuru.
Elites wachache ndani ya nchi ndiyo ambao wanaishi kwa ule uhuru wenye maana ya uhuru. Tumefikia mahala ambqpo tunaficha majina yetu halisia ili kuweza kusema ya moyoni kwa sababu ukithubutu kusema lolote linalowakaza tabaka la wenye uhuru utaishia kuwekewa matanga ama utatengenezewa kesi ambazo utafungwa ushike adabu.
Katiba ya Nchi imeonesha kabisa kuwa haina mlinzi kwa sababu walioapa kuilinda ndiyo wanaoongoza kuipuuza. Kwa mfano
- Kuzuia makusanyiko halali ya kisiasa kwa vyama vya upinzani ni uamuzi wa HOVYO sana
- Kutunga sheria za kibaguzi na kuzitekeleza kama ilivyo sheria ya pensheni, sheria ya kuadhibu wanaowakosoa viongozi, sheria inayounda Bodi za Mazao zinazodhibiti soko dhidi ya wakulima na sheria nyinginezo zinazofanania ubaguzi ni wazi nchi si ya wananchi
- Tumeona askari wetu wakitumikia siasa wakiwa kazini na wakiwa wamestaafu ambapo Katiba imezuia hilo. Maana yake ni kwamba nchi inaendeshwa na waliohuru dhidi ya wananchi wanaoishi kwa kudra ya wamiliki wa Uhuru
- Miaka 61 ya Uhuru bado maji, umeme, elimu, afya na mengine muhimu ni mambo magumu na ya kufikirika kwa wananchi waliowengi
- Katiba mpya ambayo ni hitqji la msingi kwa mazingira ya sasa ya siasa za vyama vingi, inasubiri kudra ya walio HURU maana inaonekana inatishia uhuru wa wenye kumiliki Uhuru wa nchi hii
- Sheria inayohusu misafara ya viongozi inawapuuza wananchi ambao kimsingi ndiyo wanaokamuliwa kodi zao ili kuiendesha nchi
- Kitengo cha maafa kinapokea bajeti miaka yote lakini hakijawahi kuwa effective hadi leo.
- Serikali inanunua zana na silaha kali kwa minajili ya kuwatishia, kuwapiga, kuwaumiza na kuwashughulikia wananchi ambao wanaohoji wamiliki wa uhuru.
- Wananchi wanalimwa kodi kubwa kubwa na tozo mbalimbali ambazo wanaambiwa ni kwa minajili ya maenedeleo yao lakini taifa linaambiwa na wenye Uhuru kuwa hela hizo zinatolewa na Rais ambaye kimsingi halipi kodi.
- Serikali imewekeza kwenye kusimika mitambo imara kiteknolojia inayowafuatilia na kuwadukua wananchi wake wanaohoji mwwnendo na haiba za wqliojimilikisha uhuru wa nchi.
Hebu tuelimishane hapa, hii nchi ni nani haswa anapaswa kuitwa mwenye nchi, kwa nini tumefikia hapa?