Hivi hii ni hali ya kawaida? Miaka 27 sasa nakojoa kitandani

Umekojoa leo tu kitandani au mara Kwa mara???
 
Ukiona choo ndotoni usikojoe ni mtego huo, pia kuchoka sana na kazi unalala usingizi mzito. Mwisho kabisa jitahidi kutokunywa vinywaji hasa jioni na usiku na nenda chooni mara kwa mara. Kama unashindwa kuamka mwenyewe weka hata alarm kila baada ya muda fulani ikuamshe.

Nenda hoapitalu pia ukaangalie labda kuna shida ya kibofu.Pole kwa changamoto
 
Fanya mazoezi sana inasaidia kupunguza tatizo la afya ya akili ndio chanzo cha hayo yote.
Pia penda kunywa maji mengi itasaidia kukuweka active wakati wa usiku.
Kama unakunywa pombe acha kabisa kuna siku utahaibika vibaya sana.
 
Ushauri wa BICHWAKOMWE😁
 
Kitaalam inatwa nocturnal enuresis. Sema kwako umesha fikisha umri mkubwa huenda likawa tatizo la urology, hospital linatibika kwa vidonge

Ukiwafuata watalaam wa tiba ya asili nao wana tiba inayofanya kaz harak
 
Pole sana
Suala la kukijoa kitandani ni suala mtambuka. Suala hili huweza kuathiri mtu kwa jinsi anavyojitathimini na mahusiano na jamii/psychosocial interaction. Ili uweza kumsaidia mhusika kuna hatua nyingi za kupitia:

1: Mhusika anakojoa kitandani akilala usiku tu au pia mchana?

2: Mhusika aliweza kufanikiwa kudhibiti kukojoa kitandani wakati wa utoto wake na suala hili kurejea baadaye au la?

Huwezi kumsaidia mtu mwenye tatizo hili bila kujua msingi wake. Mfano: kuna watu wanakojoa kitandani sababu ya:
1: Kiasi cha usingizi wakilala
2: Tatizo la mishipa ya fahamu
3: Unene uliopititiza na kuathiri upumuaji wakati wa kusinzia/Apnea.
4: Kibofu kidigo
5: Magonjwa ya homoni.
6: Maambukizi njia ya mkojo
7: Nk.

Msingi wa tiba:
1: Kutatua tatizo la msingi lililogunduliwa kuwa kisababishi.
2: Ratiba ya kuamka na kwenda uani kwa kutumia stopwath au mtu kumwamsha muhusika.
3: Kupunguza kiasi cha vinywaji vinavyoweza kuongeza utengenezaji wa mkojo kama vile kahawa au maji wakati wa jioni vs usiku.
4: Positive feedback/pongezi kwa kuweza kuhimili kulala bila kukojoa kitandani.
5: Kuepusha lawama inapotokea sivyo.
6: Ushauri nasaha
7: Dawa husika

NB: Fika kwa wataalamu wa afya hasa kama ukiweza kumwona daktari bingwa wa njia ya mkojo/Urologist itakuwa vyema zaidi. Ingawa waweza kusaidika na watoa tiba wengine.
 
Ndo maana nakataza watu waache kutumia maji ya mchele
 
Shukuru kwa kila Jambo!
Kuna wengine hawakojoi mkojo wa kawaida wala sperm..))
 
Ni kazi ya shetani. Nenda ukaombewe kaka na pole.
 
Njia pekee hapo ni kubadili ID badala ya kujiita 'niite bazinkulu' jiite 'niite kikojozi'.

Tabia hiyo itaachana na wewe.
 
Kali sana hii! Mkeo anatakiwa awe msiri na asiwe mnywa pombe
 
Nitafute ninayo dawa ya kutibu kukojoa kitandani 06217970903
 
Umekojoa leo tu kitandani au mara Kwa mara???
Chemsha zile ndevu za mahindi mabichi...kunywa asubuhi na jioni wiki 1 ukiona bado unaendelea hata wiki 2 ila wiki tuu inatosha unaacha kabisaa.
 
Daaah mkuu umenikimbusha,nilikuwa Nina demu langu zuri hilo la kuitwa Pendorehema,daaah huyu demu alikuwaga mzuri na nusu,kasoro yake ilikuwa hiyo ya kukojoa kitandani!

Yaani nilikuwa nikimwangalia namna alivyo mzuri na anavyokojoa kitandani naishiwa pozi!
 
Chemsha zile ndevu za mahindi mabichi...kunywa asubuhi na jioni wiki 1 ukiona bado unaendelea hata wiki 2 ila wiki tuu inatosha unaacha kabisaa.
Kinachosababisha kukojoa ni Maji na ubaridi tumboni, hio nimefanyia tafiti ya muda mrefu kikojozi usiku asilale kwenye ubaridi lazima alimwage na wengi ambao ni vikojozi ni walala ovyo jitu linalala km limekufa unaweza ukalibeba ukaenda kulilaza nje na lisishtuke hata kidogo linakoroma tu, ushawahi kumuona mtu amelala km amekufa? Ndio hao vikojozi yaan akilala amelala na watu km hao hawatakiwi kua watu wa tungi maana vichwa vyao ni kipengele anaweza hata akashindwa kutimiza majukumu yake ya kikazi kwa kuendekeza usingizi, nna ndugu yangu yeye tangu mdogo mpaka sasa amekua ana mke na watoto ila ni kikojozi, mpaka unajiuliza yule Mwanamke anamvumiaje yule mtu na hali ile ya kujikojolea maana sasa anaukimbilia uzee na hajaacha kukojoa kitandani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…