Tuko wengi.Mwenyewe alishaongea Hadi basi.Kuna muda hata kama nipo nyumbani anaamua Tu kupiga kwenye kasimu Ka nyumbani kwa sababu muda wote yenyewe inakua sebleni.Yangu kuna muda naikuta kwenye vyombo jikoni."Utaskia dada em nipib"
Kingine, pesa ya matumizi usitoe usiku, toa asubuhi unapokua unaondoka na usimpe mkeo chumbani.
Wasikilize wanafamilia yako wote, mmoja baada ya mwingine, kisha kama ni shida unayoweza kutatua hapo hapo unatatua(kama mtoto labda anataka daftari unazama mfukoni unatoa.)
Hakikisha mama yao pia unampa pesa ya matumizi mbele yao, yaani mfanye mama yao nae kama hao watoto.
Tuvumilie tu mi wa kwangu ashakubaliana na hali,nami kuna mda ananikera unapiga mara nne zote kwani kuna taarifa ya msiba?mi kwanza sipendi kuongea na simu
Aisee hii kitu inaudhi jamani, mama yangu sikuhizi simpigii simu yake kabisa, nikitaka kuongea nae nampigia mzee tu namwambia ampe mke wak simu😅😅, maana mama unaweza kupiga hata mara 10 kumbe simu ipo kwenye banda la kuku yeye yupo sijui wapi dah!