kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Naangalia taarifa ya habari ITV sasa hivi, nimestaajabu kumuona CEO wa TANESCO Maharage akisema umeme wa grid ndio uko asilimia 47 kuelekea Kigoma. Mimi labda siko Tanzania au sielewi.
Nakumbuka kwa masikio yangu nimesikia tena sio mara moja kwamba umeme wa grid ulishafika Kigoma miezi kadhaa sasa imepita. Tena kukawa na maelezo kuhusu kuokolewa gharama kubwa kutokana na kuacha kutumika mafuta mazito.
Leo nashangaa eti kumbe bado umeme wa grid kufika Kigoma. Hebu anayejua vizuri hii issue atujuze labda mimi hizi taarifa nilikuwa naota ndoto.