Hivi hii TANESCO ya Maharage si walisema umeme wa grid umeshafika Kigoma?

Hivi hii TANESCO ya Maharage si walisema umeme wa grid umeshafika Kigoma?

Naangalia taarifa ya habari ITV sasa hivi, nimestaajabu kumuona CEO wa TANESCO Maharage akisema umeme wa grid ndio uko asilimia 47 kuelekea Kigoma. Mimi labda siko Tanzania au sielewi.

Nakumbuka kwa masikio yangu nimesikia tena sio mara moja kwamba umeme wa grid ulishafika Kigoma miezi kadhaa sasa imepita. Tena kukawa na maelezo kuhusu kuokolewa gharama kubwa kutokana na kuacha kutumika mafuta mazito.

Leo nashangaa eti kumbe bado umeme wa grid kufika Kigoma. Hebu anayejua vizuri hii issue atujuze labda mimi hizi taarifa nilikuwa naota ndoto.
Huyo Muuza vifurushi vya Bongo movie Mstaafu wa DSTv(Mr Beans) na yule aliyesomea utatuzi wa migogoro ughaibuni(Bush Electrical Engineer Kipara) wanamuingiza chaka sana Mama Maridhiano![emoji1787]
 
Watu Hawana Aibu Kabisa Waliposema Umeme Kigoma Itabaki Historia Kumbe Waliwahadaa Waha
 
kigoma hakuna umene wa grid ya taifa hadi leo zile zilikuwa taarifa za kitapeli za uzinduzi mradi hewa hadi leo kigoma wanaisoma namba nilibahatika kupita huko niliona miundo mbinu ya barabara imetifuliwa sana kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kasulu shida kubwa wakandarasi wanalia sana hawana hela serikali inawapiga chenga ! waziri wa ujenzi makame mbarawa hakuna analolifanya kwa ujumla waha huko wametelekezwa.
 
Moja kati ya sifa kubwa za Magufuli ilikuwa ni UONGO.
mimba ya jpm itakutesa milele kumbuka huyo mwendazake aliacha amelipa makandarasi wa barabara baadhi ya fedha tangu malipo hayo kufanyika barabara zimebaki zimechimbwa bila kumalizika kutoka kibondo kasulu makandarasi wanalia hawana fedha na mbarawa yupo ofsini anakula kiyoyozi . serikali hii maigizo ni mengi kuliko vitendo maana hata ufatliaji wa karibu haupo kila kiongozi anafanya kazi kwa kuviziana siku ikiwa mbaya kwako wabakubebesha zigo ka kukufukuza kazi au kusimamishwa ndiyo serikali ya sasa.
 
Naangalia taarifa ya habari ITV sasa hivi, nimestaajabu kumuona CEO wa TANESCO Maharage akisema umeme wa grid ndio uko asilimia 47 kuelekea Kigoma. Mimi labda siko Tanzania au sielewi.

Nakumbuka kwa masikio yangu nimesikia tena sio mara moja kwamba umeme wa grid ulishafika Kigoma miezi kadhaa sasa imepita. Tena kukawa na maelezo kuhusu kuokolewa gharama kubwa kutokana na kuacha kutumika mafuta mazito.

Leo nashangaa eti kumbe bado umeme wa grid kufika Kigoma. Hebu anayejua vizuri hii issue atujuze labda mimi hizi taarifa nilikuwa naota ndoto.
Mkuu hivi hujui kuwa kila Mheshimiwa afanyapo ziara sehemu fulani mojawapo ya kazi zake ni kuzindua miradi iliyopo, iliyokuwepo na itakayokuja!?
 
Back
Top Bottom