Niache Nteseke
JF-Expert Member
- Apr 29, 2020
- 2,162
- 2,616
Wakuu habari zenu.
Nimepita kwenye status moja ya mdada nikakutana na hiyo clip ya Royal Tour kukiwa na maongezi kati ya Rais Samia na huyo mzungu.
Kuna kipande Rais Samia anamwambia huyo mzungu kuwa THIS IS BEGINNING OF BEAUTIFUL FRIENDSHIP. Nimejiuliza mara 2 kuhusu hiko Kiingereza je kipo sawa au?
Lakini pia, nnavyojua mimi kwenye ku-shoot movie/documentary/tamthilia kuna actions huwa zinarudiwa kurekodiwa mpaka scene husika inakaa sawa, sasa nnachojiuliza ni kuwa, katika kutengeneza hii Royal Tour hakukuwa na wasaidizi wake au watu wengine pembeni wakati Mh. Rais anaongea?
Lakini pia, wakati wana-edit hawakuskia hiko kipande, kwa sababu sauti nyingine zinaweza kuingizwa hata ukiwa studio, kwani wasingeweza kurekebisha hiko kipande?
Kwa kuwa nilisoma shule za Kata St. Kayumba nikasema niulize wadau kuhusu hiyo sentensi inatakiwa kuwa hivyo ilivyo (THIS IS BEGINNING) au kuna namna ilitakiwa kuwa wakuu?
NAWASILISHA.