Hivi hiki kitu kinaitwa sleeping paralysis ni cha kweli au ni wachawi wanafanya yao

Kuna kipindi hiyo hali ilikua inanitokea sana, mara ilikua inanitokea napokua nimelala eneo ambalo hua silalagi mara zote na mara chache ilinitokea nikiwa home
 
Elezea kinagaubaga
 
Inabidi uiwahi either ujitikise au lah lasivyo wahuni watakukaba ufee😅😅
 
Siku nyingine ukipata sleeping paralysis kunja kidole cha mkononi au mguuni utaamka hapo hapo. Binadamu sio nafsi huru kama tunavyofikiria.
 
Huku uswahilini utaambiwa umenigwa na majinamizi.
 
Haina ishu NI ganzi Tu upande wa kichwa sema me siiogopi siku hizi ila sipendi vile kupumua kunakuwa kama kwa shida hivi NI kama unakata roho
acha uongo wako kwa kuitetea sayansi,nina uzoefu na hiki kitu kwa miaka mingi,na ilifikia kipindi watu nikawa nawaona kabisa ila ndo hivyo sikuwa na la kufanya
 
acha uongo wako kwa kuitetea sayansi,nina uzoefu na hiki kitu kwa miaka mingi,na ilifikia kipindi watu nikawa nawaona kabisa ila ndo hivyo sikuwa na la kufanya
Naungana na wewe mkuu,yale ni manguvu ya giza kabisa,inashangaza eti hiyo sleeping paralysis inachagua siku za kukukamata wakati kila siku unalala vilevile
 
Nililala guest house moja apo morogoro asee nilipigwa mnigo wa ajabu niliamka huohuo usiku kutafuta sehemu nyingine daah
 
Halafu hii makitu ina mida yake 7 mpaka saa 9 hakuna sleeping paralysis sijui ya 4 usiku hata kama umelala fofofo
 
Bahati mbaya hili jambo linakutanisha makundi mawili mahasim.
Kundi la IMANI NA SAYANSI.
Sawa na DINI NA SIASA.
Hakunaga mshindi katika hawa ispokuwa itategemea na uelewa wa mtu mmoja umeota mizizi katika upande gani.

Nilitaka niweke uzoefu wangu katika hili jambo ila naona mabishano tu ya imani ya shiriki na Sayansi.
 
mimi kila ikinikuta hiyo, bila kupiga ayatul kursiyyu kimoyomoyo sichomoki. kwahio mimi naamini ni suala la kiroho sio la kisayansi.

Na pia nikichomoka then nikalala hapohapo inarudi tena, mpaka nisome ayatul kursiyyu kiganjani halafu nitemee mate mara tatu puh puh puh kiganjani, then najipaka mwili mzima ndo nilale. nikilala hapo haiji tena.

NB; PUH PUH PUH sio mimate tele..hahahha upepo wa vimatevimate.
 
acha uongo wako kwa kuitetea sayansi,nina uzoefu na hiki kitu kwa miaka mingi,na ilifikia kipindi watu nikawa nawaona kabisa ila ndo hivyo sikuwa na la kufanya
Unawaona watu kivip mkuu?
 
Waache hao wanaodai ni science waendelee kuamini hivyo hivyo siku wakikuta ute ute makalioni ndio watajua sio science ni wachawi na majini
 
Waache hao wanaodai ni science waendelee kuamini hivyo hivyo siku wakikuta ute ute makalioni ndio watajua sio science ni wachawi na majini
Kwani ulishawahi experience hiyo kitu kukuta uteute mkuu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…