Hivi hili la bandari nalo likipita kwa ushwari uliolengwa na mamlaka, je ni kitu gani au jambo gani tena la kutuingiza barabarani kama nguvu ya umma?

Hivi hili la bandari nalo likipita kwa ushwari uliolengwa na mamlaka, je ni kitu gani au jambo gani tena la kutuingiza barabarani kama nguvu ya umma?

staloni

Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
41
Reaction score
53
Kama kuna jambo ambalo limeamsha hisia na vuguvugu za kizalendo kwa kipindi kirefu kilichopita, na kupata sapoti ya wanazuoni wanaoheshimika ndani na nje ya nchi ni hili la bandari.

Pamoja na kuwa wazi kabisa kwamba kuna kila dalili ya kuja kulilia huko mbele ya safari kuwa viongozi wetu wametuingiza chaka, lakini ni dhahiri shairi kabisa kuwa umma hauna ujasiri wa kuamua kinyume na watawala walivyokusudia.

Hii ni tofauti kabisa na jirani zetu flani na sijui ni kwa nini hatujifunzi kutoka kwao.

Hivi ndo kusema kwamba hii Tanganyika ndo nchi nyepesi sana kuitawala au tusubiri kizazi kingine kitakachokuwa na uwezo wa kufanya jambo ili kiheshimiwe na watawala?

Na je hao tutakaoamua kuwasubiri watajifunzia wapi kama hawakuwahi kuona nguvu ya umma ya kizazi kilichokua mbele yao kikifanya jambo likawa jambo?...TAFAKARI KWA KINA.
 
Wakitaka kututoboa macho labda...
Na kwa hilo huenda tukakaa kimya, sisi ndio wabongo, hatupendi tabu.
 
Tumeuwa kizazi cha kuhoji na kuzalisha kizazi cha machawa hakuna chochote kitachoingiza watu barabarani

Wenyewe wanasema sisiemu mbele kwa mbele
 
Back
Top Bottom