Hivi hili tatizo la njaa Afrika hatuwezi kulimaliza sisi wenyewe?

Hivi hili tatizo la njaa Afrika hatuwezi kulimaliza sisi wenyewe?

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Mara nyingi tunaona nchi kama
  • Sudan
  • South Sudan
  • Chad
  • Somalia
  • Burundi
  • Madagascar

And some parts of
  • Nigeria
  • Kenya
  • Ethiopia

Kila mwaka lazima usikie kutoka hizi nchi kuwa millions wanaface hunger. Kwa nini AU wasijadili jinsi ya kumaliza hili tatizo?

Mfano Tanzania huku huwezi kusikia mamilioni wanaface njaa mwaka wowote, tuna ardhi yenye rutuba, mvua za kutosha, sehemu kubwa ambayo haijatumika kwa kilimo, Je ardhi hii hatuwezi kutumia some of it kulima chakula na kusaidia maeneo ya ukanda huu ambayo yanakumbana na njaa unapofika msimu wa njaa?

Sijui solution ila hata kuwakodisha ardhi labda tuseme serikali ya South Sudan, wawekeze hela kwenye ardhi sehemu fulani Tanzania, walime chakula ili utakapofika msimu wa njaa chakula kisafirishwe kuelekea regions zenye janga la njaa specifically. Yani kiwe chakula special kwa ajili ya maeneo yanayokumbwa na njaa tu

Nimefikiria naona inanikera sana kila mwaka mamilioni ya Waafrika wanateseka na njaa mpaka wasaidiwe na wazungu, nk

Sio lazima kifanyike nilichokisema lakini itafutwe tu njia ya kumaliza tatizo la njaa, Africa na sisi wenyewe bila kutegemea wazungu. Ifike tu hatua, njaa isisikike kona yoyote ya Africa
 
Nchi ulizozitaja (kama Sudan, Somalia, na Chad) tatizo lao kubwa siyo ukosefu wa chakula bali ni kukosekana kwa amani.

Hata Tanzania itoe ardhi na kulima tani milioni, chakula hakiwezi kuwafikia walengwa kama kuna vita au barabara hazipitiki, bila utulivu wa kisiasa hata tukilima bara zima, njaa haitaisha.
 
Nchi ulizozitaja (kama Sudan, Somalia, na Chad) tatizo lao kubwa siyo ukosefu wa chakula bali ni kukosekana kwa amani.

Hata Tanzania itoe ardhi na kulima tani milioni, chakula hakiwezi kuwafikia walengwa kama kuna vita au barabara hazipitiki, bila utulivu wa kisiasa hata tukilima bara zima, njaa haitaisha.
Vipi Madagascar, Burundi na Kenya?


More than two million people face hunger as drought grips Kenya | Climate News | Al Jazeera Photos: More than two million people face hunger as drought grips Kenya
 
Akili zitatukaa sawa tutamaliza kuuza na kugawa rasilimali zote na kubaki na majangwa (barren land)
Kuliko kuuzia wazungu rasilimali ni bora zitumike kusaidia waafrika
We have so much unused fertile land that could be made useful
Na hii sio kuuza rasilimali wala nini kwa sababu control inabaki Tanzania na inaweza kusitisha uzalishaji kama ikitaka
 
Policies.

Mataifa yenye nguvu na yaliyoingia ubia wa "Resources Sharing over Loans" kwa hizo nchi na nyingi Africa hata ya kwetu ikiwemo ni kuhakikisha umaskini hauishi ila unapunguzwq kwa speed ndogo sana ili serikali ziweze kutengeneza thamani ya uhitaji.
 
Mtoto akilelewa kwenye familia anayopewa kila kitu na wazazi wake na hafanyi kazi yeyote ile hata kujishughulisha kido tu hakuna, siku hao wazazi wakifa ndo hua wanauza mirathi yote, wanafuja mali, wanaanza kulia njaa.. eventualy wanakufa masikini tena kwa kifo cha aibu sana. Namaanisha ninacho kisema.
 
Siongelei kaya mojamoja
Naongelea njaa ya collective group of people "Kama watu milioni 2 kuface njaa kwa wakati mmoja katika eneo moja"
Sasa utatatua vipi njaa ya watu million mbili wakati watu wako wachache umeshindwa kuwapa chakula?

Halafu hapa nchini idadi ni kubwa sema tu veggies hawako serious na maisha ya wananchi wanawaza kupiga propaganda..!!

Hizo sehemu ulizozitaja zote zina ukosefu wa amani, sasa muda wa kulima watautoa wapi?
 
Sasa utatatua vipi njaa ya watu million mbili wakati watu wako wachache umeshindwa kuwapa chakula?

Halafu hapa nchini idadi ni kubwa sema tu veggies hawako serious na maisha ya wananchi wanawaza kupiga propaganda..!!

Hizo sehemu ulizozitaja zote zina ukosefu wa amani, sasa muda wa kulima watautoa wapi?
Umena vema sana.
 
Kenya, Madagascar, Burundi????
Zina ukosefu wa amani??
Blaza, kwanini tupeleke maji ya kuoga kwa yakobo wakati kwa bakari kunawaka moto?? Tungetumia kuvu na rasilimali kumsaidia bakari kuzima moto kwanza then tukae pamoja tuanze kutatua matatizo yanayo wakali.

Hata hivo unaangalia kwa majirani akati baadhi ya watoto wako hawana hata nguvu za kwenda chooni, maana wakienda huko wana jumber tu hakuna kinachotoka.

Nadhani tungeanza kumfafanulia Lamomy kuhusu hayo, kuliko kuanza kuuliza kama kenya wanakosa amani. Hatuwezi kuzika kama ndugu tunagombana msibani mkuu.
 
Kenya, Madagascar, Burundi????
Zina ukosefu wa amani??
Sio sehemu zote katika hizo nchi kuna njaa, hao wanasumbuliwa na ukame wa baadhi ya maeneo kama Tanzania.

Wao wanapaswa wajisaidie wenyewe kwa kupanda mazao ambayo yanakubali kwa jiografia ya eneo husika..!!

Ni kama Dar mpunga haukubali lakini Mbeya unakubali, hivyo watu wa Mbeya wawauzie wa Dar.

Singida kame mazao ya chakula hayakubali lakini wana alizeti na vitunguu vinakubali.
 
hata tanzagiza kuna njaa, njaa ziko aina nyingi, njaa ni umaskini, kuna watanzagiza wengi tu hasa watoto wanakwenda kulala bila ya kula chochote, watoto wenginre wanatoroka shuleni sababu ya njaa ...
 
Umena vema sana.
Huyo kuna kitu haelewi, mfano Zambia mahindi kwao yanakubali lakini kuna kipindi mvua zikiwa chache yanagoma Tanzania tunawauzia. Hivyo hivyo kuna kipindi mvua zilisumbua Tanzania tukawa tunanunua mahindi Zambia pamoja na wakenya…!!

Hao hao wazambia mchele wanaokula wanautoa Tanzania lakini mbona hawalalamiki njaa?
 
Back
Top Bottom