FourTwoNet
JF-Expert Member
- Aug 4, 2022
- 1,236
- 2,512
Sipati picha kama JF wangekuwa wameandika jina lao kama "Jamii Folums" ingekuaje.
Au jukwaa hili jina lingeandikwa "Habali na Hoja mchanganyiko sijui ingekaaje hiyo.
Inaeleweka kwamba kila mmoja ametoka maeneo tofauti, hivyo lugha zetu za mama zinaweza kuchangia namna tunavyoweza kutamka na kuongea lugha nyingine, hilo linaeleweka.
Tafrani inakuja kwenye swala zima la kuandika. Kutamka ni rukhsa kukosea, lakini kwenye kuandika, hilo halina mjadala.
Tusipokosoana, matokeo yake hata waandishi wetu wa magazeti na vyombo vya habari na watunzi wa riwaya wataendekeza kosa hili na kupoteza ladha ya lugha.
Utakuta mtu kaandika maneno mengine kwa kuweka hizi herufi vizuri na kwenye sentensi hiyo hiyo kachemsha maneno mengine, hii inamaana amezoea kuona mtu anaandika neno flani kwa kukosea, kwa hiyo anaona ni sawa. Ndio maana shuleni kulikuwa na zoezi la imla.
Siku hizi hata walimu wamezoeshwa na waliokuwa walimu wao, hivyo kupelekea kutokuona hili katika kusahihisha wanafunzi.
Binafsi, nitakuwa nikiingia humu halafu nikute umelipua L na R....sikuachi.
Tukiendekeza tabia hii, hata hichi kiswahili tunachojivunia tutakipoteza.