Hivi hizi R na L zimetukosea nini?

Ingekuaje ❌ Ingekuwaje ✅
Swala zima ❌ Suala zima ✅
Hata hichi ❌ hata hiki✅

Anza wewe kujifunza uandishi kwanza.
Mtoa mada kwa akili yake anafikiri makosa ya kiuandishi yapo kwenye R na L tu! Ona sasa na yeye mwenyewe alichokifanya.

"Lugha zetu za mama......."✖️

Lugha mama ✔️
 
Wanaochanganya L na R wengi ni vichwa vizito katika kufikiri na kuelewa. Waangalie wengi wenye hilo tatizo utagundua hata uwezo wao kujenga hoja na kuongea ishu zenye mantiki ni mdogo sana.
Nagongea msumari.
 
Kujirekebisha ni muhimu, na kukosolewa pia mkuu. Naungama na kutubu dhambi zangu.
 
Ingekuaje ❌ Ingekuwaje ✅
Swala zima ❌ Suala zima ✅
Hata hichi ❌ hata hiki✅

Anza wewe kujifunza uandishi kwanza.
Hii imekuwa kama jadi yetu watanzania. Kupenda kubisha tunaposahihishwa. Mwanzisha thread ana point nzuri sana. Haya maneno uliyosahihisha mara nyingi yanaweza kuvumilika lakini siyo hili kosa la R na L.
 
Mtoa mada kwa akili yake anafikiri makosa ya kiuandishi yapo kwenye R na L tu! Ona sasa na yeye mwenyewe alichokifanya.
Tuanzie kwanza hapo kwenye R na L. Nimekubali na nimeelewa maelekezo. Ntakuwa makini.
 
Hii imekuwa kama jadi yetu watanzania. Kupenda kubisha tunaposahihishwa. Mwanzisha thread ana point nzuri sana. Haya maneno uliyosahihisha mara nyingi yanaweza kuvumilika lakini siyo hili kosa la R na L.
Ahsante sana mkuu.
 
Ajabu hata baadhi ya watangazaji wa vituo vya runinga na redio ni waathirika wa kuchanganya R na L.
 
Mkuu una hoja ya msingi kabisa japo kuna watu wanataka (kama kawaida ya wabongo) kupindisha mada kwa kuleta ubishi wa kijinga kabisa. Makosa kwenye kutumia R na L ni janga la nchi. Kama mtu atakosea kwenye matamshi nitaelewa lakini siyo kuandika ambako tunaanza kufundishwa tangu chekechea.
 
Tuanzie kwanza hapo kwenye R na L. Nimekubali na nimeelewa maelekezo. Ntakuwa makini.
Mara nyingi hizo R na L husababishwa na asili ya watu! Mfano watu wa Kanda ya Ziwa, kimsingi hawana L! Badala yake wana R tu!! Niretee ugari, Niretee Gwajima, nk.

Ukienda Dodoma, Iringa, nk huko hawana R! Badala yake wana L tu! Badala ya kutamka Iringa , wenyeji hutamka Ilinga! Dodoma nako kila neno lenye R, hugeuzwa na kuwa L! 'Napeleka malejesho', nk.

Mifano ni mingi, muda ni mchache.
 
Hii imekuwa kama jadi yetu watanzania. Kupenda kubisha tunaposahihishwa. Mwanzisha thread ana point nzuri sana. Haya maneno uliyosahihisha mara nyingi yanaweza kuvumilika lakini siyo hili kosa la R na L.
Makosa ni makosa tu hata kama kwako yanavumilika, tunatofautiana kiwango cha kuyavumilia….. kama kwako sio tatizo haimaanishi yapo sahihi.

Jenga utamaduni wa kukosoana kama tulivyo sisi akili kubwa, hata muuaji anapofiwa hulia machozi.
 
Matumizi ya lugha na ufasaha wake ni shida kwa watu wengi Sana ndio maana Kuna muda tunashauriwa kuangalia mantiki ya kile alicho andika kuliko kuzingatia matumizi ya lugha kwa usahihi wake.

NB :siungi mkono matumizi yasiyo sahihi ya lugha

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Unapokosea wakati wa kukosoa wenzako kubali na wewe kukosolewa ili tujenge uelewa wa pamoja, sijaelewa kwa nini unataka makosa yake yapite bila kupingwa kisa tu kaleta hoja unayoiita janga la kitaifa…. huu utakuwa ubishi kama sio ujuaji wa kipumbavu.

“Usini-diss kwa kiswahili kama hujui hata kukitamka”.
 
Kushindwa kuitamka herufi fulani kwa sababu ya athari ya lugha mama ni jambo linaloeleweka na liko kwa jamii nyingi ila kuchanganya herufi ni jambo lingine kabisa.
Ni kweli baadhi ya watu wa Kanda ya ziwa hawana L, kwa maana hutegemi kumsikia akisema UgoLo badala UgoRo.

Pia unaweza kuwa na shida ya kutamka ila ikifika hadi kuandika mtu bado anachanganya huyo ni kilaza tu.
 
Ni watangazi vihiyo, na wanapaswa kuondolewa kwenye hivyo vyombo vya habari kabisa kwa sababu wanakuza ukubwa wa hilo tatizo.
Ajabu hata baadhi ya watangazaji wa vituo vya runinga na redio ni waathirika wa kuchanganya R na L.
 
Makosa ni makosa tu hata kama kwako yanavumilika, tunatofautiana kiwango cha kuyavumilia….. kama kwako sio tatizo haimaanishi yapo sahihi.

Jenga utamaduni wa kukosoana kama tulivyo sisi akili kubwa, hata muuaji anapofiwa hulia machozi.
Yapo makosa yanayovumika kwenye kiswahili. Hivi unajua Zanzibar wanaandika ''mwengine'' na sisi tunaandika ''mwingine''?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…