Hivi hizi taa za kuongozea magari zinazofungwa sasa hapa Dar zimefanyiwa Tathmini au ni Upigaji?

Hivi hizi taa za kuongozea magari zinazofungwa sasa hapa Dar zimefanyiwa Tathmini au ni Upigaji?

Weeeh!! Tena IT ndio mna visa sijaona aisee.!!
Hapa nimetamani kuongea kwa voice note nikucharule 😹😹😹

Kuna siku nilikuwa nampeleka dogo shule mkoa, nilikuwa mdogo mdogo.!
Mbele si nikaona IT imeniuzia kicheche nilimind, nikapotezea.
Nikaja kukutana naye mbele nikamuovertake si akafanya ligi akanichomekea tena.!!
Nikasema manyoko wewe usintanie gari yenyewe ya boss unaipeleka Congo huko ngoja nikuonyeshe.!! Nikapaki pembeni nikamwambia dogo hamia seat ya nyuma nimuonyeshe kibuyu huyu ananizoea.!!
Nilinyoosha goti na mimi nikamchomekea aliyumba nikaona anapeleka gari kichakani kuchimba dawa 😂😂😂
Akajitahidi akachomoka akarudi road nikamsubiri mbele akanipita kwa speed na honi za kukubali yaishe nikacheka sana’a nikaona kajifunza hataki ugomvi huyu.!!

Nilichofanya na mimi nikamuovertake kwa speed nikashusha kioo nikampa middle finger alishangaa kuona ni demu akacheka akanipa salute mi huyo nikamuachia manyoya.!! 😹
Tukaja kukutana tena check point waliponisimamisha kwa muda wananiuliza unaenda wapi mbona unaendesha gari km limeibiwa? Halafu ni mdada?
Wakanikagua yule jamaa anacheka, anasema niwaambie ulichokifanya?? Nikamkata jicho la “mwana ukome” walivyoona niko na mwanafunzi wakaniruhusu.!!
Yule jamaa wa IT akaniita “Oyaah road trip Queen nisubiri” nikamsonya nikamwaga moto hatujaonana tena mpk naingia Mbeya.!!
IST huwa inakimbia sana
 
Kuna kipindi hapo kati ilichanganya sana.
Maybe ilifika 500k. na huwa inategemea umbali.
DRC, Zambia au Malawi bei zinatofautiana sana.

Then kipindi hicho tulikuwa tunaruhusiwa kubeba vichwa.
Hiyo ya kubeba vichwa ilikuwa hatari hukuogopa??
Kuna dereva mmoja wa IT alinisimuliaga alivyopakiza abiria wanne hatari.!!
Ilikuwa hivi, yule dereva alikuwa anapeleka gari Zambia alivyofika Mbezi akapata abiria akawashusha Moro, wakapanda abiria wengine wawili wanaenda Iringa, mmoja kakaa mbele mwingine kakaa nyuma.!!
Kufika Doma akapata abiria wengine wawili wakakaa nyuma, jumla wakawa abiria wanne na dereva watano.!!

Anasema walivyofika zile kona za Iyovi mbele mbele akashangaa yule abiria wa mbele katoa panga limenolewa kote anamwambia paki gari pembeni, yule mwenzie wa nyuma naye kawadhibiti wale abiria wenzie wawili naye ana panga.!! Dereva ikabidi awe mpole akaona gari la watu linaondoka na cha kuwafanya hana.!!

Sasa dereva akaangalia kwenye mirror akaona mmoja wa abiria aliyedhibitiwa anampa ishara “Paki gari” dereva akapaki.!
Kabla hawajashuka wakashangaa chuma cha baridi “SMG” kimemgusa yule jamaa wa mbele mwenye panga, anaambiwa awe mpole lasivyo anamwagwa ubongo.!! Ebanaeeh.!! Dereva anakwambia aliona mikojo inatoka.!!
Wale jamaa wa mapanga wakashushwa, dereva akaulizwa anawadai shingapi akataja wakaambiwa walipe nauli zao.! Hakuna kelele hapo wametulizwa na mapanga yao, wamekuwa wapole.! 😹😹

Dereva akalipwa pesa yake wazee wa kazi wakamwambia dereva “suka amsha” wale jamaa wa mapanga wakaanza kuomba yaishe wapewe hata lift pale pabaya usiku wanaweza kutekwa 😂
(wamejisahulisha km wao wangefanikiwa wangewaacha wenzao)
Wale majambazi wakawaambia nyie wajinga aliyewaambia gari linaporwa kwa mapanga nani??

Wakaondoka huku dereva kichwa kimepata moto anawaza sawa wale wa mapanga wameshindwa vipi kuhusu hawa majambazi og nawafanyaje?? 😂😂😂
Walivyofika kitonga wakamuuliza dereva unadai shingapi? Sisi hatuna shida na gari tunataka cash, kumbe kuna mtu wao walikuwa wanamuwahi wamchukuie pesa.!!
Dereva akashusha pumzi hakuamini akasema, msinilipe chochote nyie nendeni wakuu.!!
Wale majambazi wakampa pesa kinguvu wakashuka, yule dereva anasema toka pale hakupakia abiria yoyote njiani mpk amefika kwa boss wake Zambia 😂😂😂
 
No, kuna mambo mengine age factor inakubeba kuyafanya! wala sio shida.

Maybe naweza kukupa changamoto siku moja kama utataka lakini!!

Tufikie walau 220km/hr uone gari inavyoweza kukimbia. 🤣
Hiyo iko poa tuwasiliane mi napenda sana car racing 😂
 
Sema ulivyoniambia Subaru kidogo niseme nakufahamu.

I know one of my colleague ni Team Subaru, na huwa anaenda kwenye rally mara nyingi.

Anyway kama jina lako halisi linaanza na J.
Itakuwa ni wewe 🤣🤣🤣.
😹😹😹 Jay tenahh
Sio mimi bana, mimi Lamomy
 
Wadau ni balaa sasa,

Taa zinazofungwa kwa sasa kuanzia Barabara ya Gerezani, Sokoine Drive na Kilwa Road sio za kawaida.

Ni nyingi kupita maelezo, nauliza tu aliyefanya Tathmini ya kuweka hizi taa amelenga nini?

Kwa mfano ukitokea Gerezani kona ya Sokoine Drive Kuna msururu wa traffic light. Inaanza ya kivuko cha watembea kwa miguu, mbele mita 10 kuna taa za kuingia barabara ya gerezani mita 10 tena kuna taa za junction ya Sokoine na Gerezani.

Its look too much.

Anyway ngoja tuone zitafanya vipi kazi.

Ila ni kiashiria cha uharibifu wa rasilimali pesa.
Sina uhakika kwanini, inaweza kuwa zina malengo ya kupunguza msongamano.

Lakini waliodizaini watakuja kutueleza kwanini wamefanya hivyo.
 
Sina uhakika kwanini, inaweza kuwa zina malengo ya kupunguza msongamano.

Lakini waliodizaini watakuja kutueleza kwanini wamefanya hivyo.
Kesho nitapiga picha ili nieleweke
 
Hiyo ya kubeba vichwa ilikuwa hatari hukuogopa??
Kuna dereva mmoja wa IT alinisimuliaga alivyopakiza abiria wanne hatari.!!
Ilikuwa hivi, yule dereva alikuwa anapeleka gari Zambia alivyofika Mbezi akapata abiria akawashusha Moro, wakapanda abiria wengine wawili wanaenda Iringa, mmoja kakaa mbele mwingine kakaa nyuma.!!
Kufika Doma akapata abiria wengine wawili wakakaa nyuma, jumla wakawa abiria wanne na dereva watano.!!

Anasema walivyofika zile kona za Iyovi mbele mbele akashangaa yule abiria wa mbele katoa panga limenolewa kote anamwambia paki gari pembeni, yule mwenzie wa nyuma naye kawadhibiti wale abiria wenzie wawili naye ana panga.!! Dereva ikabidi awe mpole akaona gari la watu linaondoka na cha kuwafanya hana.!!

Sasa dereva akaangalia kwenye mirror akaona mmoja wa abiria aliyedhibitiwa anampa ishara “Paki gari” dereva akapaki.!
Kabla hawajashuka wakashangaa chuma cha baridi “SMG” kimemgusa yule jamaa wa mbele mwenye panga, anaambiwa awe mpole lasivyo anamwagwa ubongo.!! Ebanaeeh.!! Dereva anakwambia aliona mikojo inatoka.!!
Wale jamaa wa mapanga wakashushwa, dereva akaulizwa anawadai shingapi akataja wakaambiwa walipe nauli zao.! Hakuna kelele hapo wametulizwa na mapanga yao, wamekuwa wapole.! 😹😹

Dereva akalipwa pesa yake wazee wa kazi wakamwambia dereva “suka amsha” wale jamaa wa mapanga wakaanza kuomba yaishe wapewe hata lift pale pabaya usiku wanaweza kutekwa 😂
(wamejisahulisha km wao wangefanikiwa wangewaacha wenzao)
Wale majambazi wakawaambia nyie wajinga aliyewaambia gari linaporwa kwa mapanga nani??

Wakaondoka huku dereva kichwa kimepata moto anawaza sawa wale wa mapanga wameshindwa vipi kuhusu hawa majambazi og nawafanyaje?? 😂😂😂
Walivyofika kitonga wakamuuliza dereva unadai shingapi? Sisi hatuna shida na gari tunataka cash, kumbe kuna mtu wao walikuwa wanamuwahi wamchukuie pesa.!!
Dereva akashusha pumzi hakuamini akasema, msinilipe chochote nyie nendeni wakuu.!!
Wale majambazi wakampa pesa kinguvu wakashuka, yule dereva anasema toka pale hakupakia abiria yoyote njiani mpk amefika kwa boss wake Zambia 😂😂😂
Aisee hatari sana.
Lakini ndio hivyo!!
Tulikuwa hatupakii hovyo hovyo.

Sijawahi kukutana na kisanga chochote zaidi ya kunusurika kwa mambio tu
 
Taa za karibu namna ulivyoelezea mara nyingi huwa zinafanya kazi pamoja, "Synchronized".

Usiwe na wasiwasi.
Asante kwa kunitia moyo.
Ubaya taa zipo hazifanyi kazi muda wote.
 
Asante kwa kunitia moyo.
Ubaya taa zipo hazifanyi kazi muda wote.
Nimewahi kuona sehemu, nje ya Tanzania, ina taa za karibu, nikaona zinafanya kazi kwa pamoja.

Pia zina sensor ya magari, kama upande wa kulikowaka nyekundu, kuna gari imekuja japo moja, baada ya muda zitajibadili na kuwasha nyekundu kwengine, na kuruhusu hii moja. Ikipita tu zinabadilika na kuendelea kupeleka magari yalipo.
 
Na hapo lazima sensor zitawekwa, kuzuia msongamano na usimamishaji wa magari bila ulazima.
 
Jadda inaonekana ww muoga sana.!!
Kuna siku nilikuwa nadrive night kali naenda mkoa, kuna sehemu inaitwa senjere kuna mlima lori lilikuwa mbele yangu.!!
Kila nikiliomba nipite linanigomea linacheza cheza babarabara nzima.!!
Ghafla likaniruhusu ila likawa halina utulivu, sijatulia likaanza kurudi reverse halafu linarudi zigzag weeehh.!! Nikasema hapa tayari dude lishabuma hili bila kutumia akili ya ziada naondoka.!!
Nikaanza kulivizia lilivyoingia kushoto nyingi nikanyoosha goti speed niliyotoka nayo haina kugeuka wala kuangalia pembeni.!!
Ile siku niliandika kwenye diary sikuamini km ningechomoka.!!

Njoo siku tutafute trip hata za chalinze tufanye fujo. Nimemiss vurugu za road trip siku nyingi sijagombana na trafic 😹😹
Hahaha huo siyo uoga ila ndio uhalisia ulioko huko highway yani ukishakuwa huko hakuna cha bmw wala cruiser, wote mnakuwa wapole mbele ya kina scania na yutong maana huko huwa ndio maeneo yao ya kujiachia kuliko yakiwa mjini, na kumbuka lori au basi likikuvaa mara nyingi hasara inakuwa kwako zaidi kuliko kwao

Mimi siyo muoga ila pia huwa sijiamini kiasi hicho nikiwa barabarani, maana si kila ajali anayopata mtu inasababishwa na mhusika nyingine ni za kusababishiwa kwahiyo huwa niko makini sana hata wewe mwenyewe si unaona namna ulivyoponea chupuchupu, yani wale jamaa wana utemi sana hata akiwa kwenye lane yako huna budi kuwa mpole na hata yeye anajua huwezi shindana naye utampisha tu

Anyway kumbe unapenda ligi za road trip kama mimi, basi inshaallah siku nikitulia tutafanya namna tukiwashe ila kwa sasa ratiba zinanibana, nina safari za mara kwa mara za kiofisi ambazo huwa situmii usafiri binafsi sana
 
bad enough usimikaji wa zile taa zimeingilia zile njia za kupitia walemavu na wheelchair zao.
 
Back
Top Bottom