Kuna kipindi hapo kati ilichanganya sana.
Maybe ilifika 500k. na huwa inategemea umbali.
DRC, Zambia au Malawi bei zinatofautiana sana.
Then kipindi hicho tulikuwa tunaruhusiwa kubeba vichwa.
Hiyo ya kubeba vichwa ilikuwa hatari hukuogopa??
Kuna dereva mmoja wa IT alinisimuliaga alivyopakiza abiria wanne hatari.!!
Ilikuwa hivi, yule dereva alikuwa anapeleka gari Zambia alivyofika Mbezi akapata abiria akawashusha Moro, wakapanda abiria wengine wawili wanaenda Iringa, mmoja kakaa mbele mwingine kakaa nyuma.!!
Kufika Doma akapata abiria wengine wawili wakakaa nyuma, jumla wakawa abiria wanne na dereva watano.!!
Anasema walivyofika zile kona za Iyovi mbele mbele akashangaa yule abiria wa mbele katoa panga limenolewa kote anamwambia paki gari pembeni, yule mwenzie wa nyuma naye kawadhibiti wale abiria wenzie wawili naye ana panga.!! Dereva ikabidi awe mpole akaona gari la watu linaondoka na cha kuwafanya hana.!!
Sasa dereva akaangalia kwenye mirror akaona mmoja wa abiria aliyedhibitiwa anampa ishara “Paki gari” dereva akapaki.!
Kabla hawajashuka wakashangaa chuma cha baridi “SMG” kimemgusa yule jamaa wa mbele mwenye panga, anaambiwa awe mpole lasivyo anamwagwa ubongo.!! Ebanaeeh.!! Dereva anakwambia aliona mikojo inatoka.!!
Wale jamaa wa mapanga wakashushwa, dereva akaulizwa anawadai shingapi akataja wakaambiwa walipe nauli zao.! Hakuna kelele hapo wametulizwa na mapanga yao, wamekuwa wapole.! 😹😹
Dereva akalipwa pesa yake wazee wa kazi wakamwambia dereva “suka amsha” wale jamaa wa mapanga wakaanza kuomba yaishe wapewe hata lift pale pabaya usiku wanaweza kutekwa 😂
(wamejisahulisha km wao wangefanikiwa wangewaacha wenzao)
Wale majambazi wakawaambia nyie wajinga aliyewaambia gari linaporwa kwa mapanga nani??
Wakaondoka huku dereva kichwa kimepata moto anawaza sawa wale wa mapanga wameshindwa vipi kuhusu hawa majambazi og nawafanyaje?? 😂😂😂
Walivyofika kitonga wakamuuliza dereva unadai shingapi? Sisi hatuna shida na gari tunataka cash, kumbe kuna mtu wao walikuwa wanamuwahi wamchukuie pesa.!!
Dereva akashusha pumzi hakuamini akasema, msinilipe chochote nyie nendeni wakuu.!!
Wale majambazi wakampa pesa kinguvu wakashuka, yule dereva anasema toka pale hakupakia abiria yoyote njiani mpk amefika kwa boss wake Zambia 😂😂😂