Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Bila picha hainogi...

Maisha yako ni dira yako wasikupangie cha kufanya
 
Mbweni JKT kwa ukubwa huo hahizidi 80m kule kwa Mama viwanja vikubwa ndio 200m
 
Nipo Mdogo wangu...Nilichukua break kidogo humu nimerudi...

Umenikumbusha Kuna sehemu pia Goba huko kunaitwa Goba Maghorofani...Hakuna nyumba ya chini hata moja....nyumba huko ni Maghofa tu.
Oohh okay usipotee sana jamani

Yeah maeneo mengi dar yako hivyo ukikuta sehemu ni ushuani ni ushuani kweli na ukikuta ni uswahilini ni uswahilini kweli yani

Sema ndio hivyo uchumi unavyozidi kukuwa watu wanazidi kujenga nyumba standard kwahiyo miaka ya mbeleni slums zitaisha
 
Hata Mama Samia Private residence yake ni hukohuko Mbweni.
 
Ni juhudi za serikali ya awamu ya sita hizo. Kule wanaendesha ndinga number plate E series wote.
 
Kuna jamaa angu anajilaumu hadi leo hii kushindwa kununua Kiwanja Kariakoo miaka ya 98, anasema alipata mtu anataka kumuuzia bei nzuri lakini alikataa.

Leo hii 2024 huwezi kumudu gharama ya Kiwanja Kariakoo 🙌
Kakudanganya huyo, hata mchikichini kwenye skwata huwa wanajiona wapo kariakoo.

Au alitaka kuuziwa jangwani chini kwenye mafuriko napo NI kariakoo pia Kwa Jina.
 
kuna siku mtu ali request saa 7 za usiku alikuwa anaelekea huko mitaa ya jkt kwa mbele.

kwa jinsi palivyo jengeka walahi nilijiona nipo dunia nyingine hadi hofu ikaanza kuniingia. uko watu wamejenga zile story za nchi ya majini ukiisikiliza harafu uende huko usiku unaweza ukasema story za majini zina uhalisia...!

mbele ya JKT kuna yale tuseme mabwawa ambayo barabara ipo katikati ya hayo mabwawa🤣 kwa mgeni harafu iwe usiku lazima uogope​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…