Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Habari za Sabato Wakuu!

Wiki nzima hii nilikuwa huku Mbweni, ninakijiplot changu. Sasa kwa hali niliyoikuta nimejikuta ninakata tamaa.

Aiseeh! Hawa majirani zangu sio Pouwa. Hii mijengo walioidondosha na wanaoidondosha sio Pouwa! Unaweza ukadhani upo kwenye filamu za kinaijeria.

Hapa nashauriwa niuze hiki kiwanja kwa sababu pesa ya kujenga vyuma kama vile haiwezekaniki bila kuwa aidha mwekezaji, Fisadi, muuza madawa, mfanyabiashara wa madini, Mwanasiasa mlafi, mzee wa dili haramu na katili, mzee wa kuzamisha wavuni mipira iliyokufa na Watu wa aina hiyo.

Magari yanayopita huku ni magari mazito, Chris Lukosi huita madungu jeshi.

Hivi kweli hawa wanaojenga huku Mbweni ni Watanzania kweli? Maana umaskini wa nchi yetu na hizi nyumba huku ni mbingu na ardhi.

Santeni
Bila picha hainogi...

Maisha yako ni dira yako wasikupangie cha kufanya
 
images (34).jpeg
images (31).jpeg
images (33).jpeg
 
Unatakiwa kufurahi kuwa plot yako ipo kwenye eneo zuri, kama huna uwezo wa kuijenga iweke for Sale, utauza pesa ndefu sana na kuweza kupata plot sehemu ya kawaida ukajenge nyumba nzuri.

Unaweza kuuza hata 500m, wenye hela wanaangalia mazingira tu. Wewe nenda sehemu nzuri ukanunue eneo zuri na kubwa ufanye maisha.

Usijifosi kuishi mazingira huwezi kumudu(huendani nayo)
Mbweni JKT kwa ukubwa huo hahizidi 80m kule kwa Mama viwanja vikubwa ndio 200m
 
Nipo Mdogo wangu...Nilichukua break kidogo humu nimerudi...

Umenikumbusha Kuna sehemu pia Goba huko kunaitwa Goba Maghorofani...Hakuna nyumba ya chini hata moja....nyumba huko ni Maghofa tu.
Oohh okay usipotee sana jamani

Yeah maeneo mengi dar yako hivyo ukikuta sehemu ni ushuani ni ushuani kweli na ukikuta ni uswahilini ni uswahilini kweli yani

Sema ndio hivyo uchumi unavyozidi kukuwa watu wanazidi kujenga nyumba standard kwahiyo miaka ya mbeleni slums zitaisha
 
Habari za Sabato Wakuu!

Wiki nzima hii nilikuwa huku Mbweni, ninakijiplot changu. Sasa kwa hali niliyoikuta nimejikuta ninakata tamaa.

Aiseeh! Hawa majirani zangu sio Pouwa. Hii mijengo walioidondosha na wanaoidondosha sio Pouwa! Unaweza ukadhani upo kwenye filamu za kinaijeria.

Hapa nashauriwa niuze hiki kiwanja kwa sababu pesa ya kujenga vyuma kama vile haiwezekaniki bila kuwa aidha mwekezaji, Fisadi, muuza madawa, mfanyabiashara wa madini, Mwanasiasa mlafi, mzee wa dili haramu na katili, mzee wa kuzamisha wavuni mipira iliyokufa na Watu wa aina hiyo.

Magari yanayopita huku ni magari mazito, Chris Lukosi huita madungu jeshi.

Hivi kweli hawa wanaojenga huku Mbweni ni Watanzania kweli? Maana umaskini wa nchi yetu na hizi nyumba huku ni mbingu na ardhi.

Santeni
Hata Mama Samia Private residence yake ni hukohuko Mbweni.
 
Ni juhudi za serikali ya awamu ya sita hizo. Kule wanaendesha ndinga number plate E series wote.
 
Kuna jamaa angu anajilaumu hadi leo hii kushindwa kununua Kiwanja Kariakoo miaka ya 98, anasema alipata mtu anataka kumuuzia bei nzuri lakini alikataa.

Leo hii 2024 huwezi kumudu gharama ya Kiwanja Kariakoo 🙌
Kakudanganya huyo, hata mchikichini kwenye skwata huwa wanajiona wapo kariakoo.

Au alitaka kuuziwa jangwani chini kwenye mafuriko napo NI kariakoo pia Kwa Jina.
 
kuna siku mtu ali request saa 7 za usiku alikuwa anaelekea huko mitaa ya jkt kwa mbele.

kwa jinsi palivyo jengeka walahi nilijiona nipo dunia nyingine hadi hofu ikaanza kuniingia. uko watu wamejenga zile story za nchi ya majini ukiisikiliza harafu uende huko usiku unaweza ukasema story za majini zina uhalisia...!

mbele ya JKT kuna yale tuseme mabwawa ambayo barabara ipo katikati ya hayo mabwawa🤣 kwa mgeni harafu iwe usiku lazima uogope​
 
Back
Top Bottom