Habarini wana jamvi...
Moja kwa moja kwenye mada husika.... Nilikuwa naperuzi kwenye mtandao mmoja maarufu na kukutana na habari ya kugunduliwa kwa mijusi (Dinosaurs) huko lindi ambao wanakadiriwa kuwepo miaka million 150 iliyopita...
Sasa kizaa zaa kikaanzia hapo watu kushangaa hio miaka eti sasa hivi ndio kwanza mwaka
2021, wanahoji hayo mamilioni ya miaka yametoka wapi?
Nimeishiwa na pozi kabisa yaani......
Kwa sisi tunao somea Geology (Jiolojia) hatubabaishwi kabisa na hizo data kwani dunia inakadiriwa kuwa na miaka bilioni 4.5..... So ndani ya huo muda vingi vimefanyika na kutokea
Nawasilisha
View attachment 1962274
View attachment 1962275
View attachment 1962276
View attachment 1962277