Hivi humu JF hamna wachawi?

Kuna thread moja nimeona inadai JF sasa tuko 195,958!hivi humu wanakosekana wachawi?hebu waniroge nijue kama wapo!
JINSI MCHAWI ANAVYOMWITA JINI NA KUMTUMIA~1


NJIA YA UANGALIZI



Hii pia ni miongoni mwa njia wanazotumia wachawi hawa katika kumuita kafiri mwenzao wa kijijini na kumtumia katika shugli zao za kiuchawi na kuwasababishia matatizo binadamu wenzao au hata wanyama mbalimbali wa kufugwa bila sababu yoyote ya msingi.

katika njia hii mchawi ambaye anataka kumuita jinni huyu aliyehasi amri za mola wake ni lazima avizie iwe usiku sana nyakati za giza, hutafuta sehemu nzuri ambayo ataweza kuziona nyota angani kisha hukaa hapo huku akiangalia nyota fulani na kuisubiri itokeze angani.

Ikishatokeza nyota hii huinuka mchawi huyu na huanza kuiomba kwa visomo na maneno ya kichawi halafu anaanza kusoma tarasimu yenye maneno mazito ya kichawi na kuwaita majini waje kumtumikia,hakika maneno haya wanayoyasema ni mazito mno yasiyoweza kuandikika au kusemwa hadharani na mtu mwenye kumuogopa muumba wake.

Baada ya hapo anafanya harakati fulani kwa kupeleka mikono yake juu na kuishusha chini[kama anavuta kitu]mwenyewe anadai anateremsha pepo wa nyota iyo lakini kwa hakika hii ni ibada anayoifanya kuiabudu nyota hii badala ya mungu hata kama mchawi huyo alipofundishwa njia hiyo hakuambiwa hayo.

Basi kinachofuata hapo ni kuwa Mashetani yanaitikia amri ya mchawi huyu aliyelaaniwa baada ya kuona na kupenda harakati zake anazozifanya kumkufuru mungu na kuliongezea idadi jeshi la Ibilisi,na wanamfanyia kile kitu chake alichotia nia kukifanya huku yeye anaamini kuwa ile nyota ndiyo iliyomsaidia.



Nyota hii ambayo imesingiziwa uongo huu maskini huwa haijui kitu chochote kinachoendelea hapo bali ni maujanja tuu ya shetani katika kumzuga binadamu na kumtia dhambini.

Wachawi wenyewe wanaamini kuwa ukiwa umerogwa uchawi anaotumiwa jini wa namna hii,hauwezi kupona mpaka uaguliwe ndani ya siku ambayo nyota hiyo itaonekana tena na kuna nyota ambazo zenyewe kwa mwaka hutokea mara moja tuu,yaani uisubiri ile nyota tena na ikitokeza uiombe ikufungulie uchawi uliorogwa kwa kutumia jini wa njia hii.

Lakini ukweli ni kwamba hakika wayafanyayo wachawi ni vitimbi tuu mbele ya mkuu na mmiliki wa viumbe vyote, kwani kwa wale ambao tunatibu kwa kutumia kurani tunaibatilisha na kumtibu mtu mwenye matatizo haya mara moja Inshaa Allah. Tutaendelea baadae nina logg off...

Ukiwa na Shida yoyote ile Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169

 
Safi sana mkuu, je? Kuna kisomo cha rukya cha halali Na cha batili? Inasemekana kunawengine wanasoma rukya huku wakimshirikisha muumba kwa njia isiyo halali
 
Safi sana mkuu, je? Kuna kisomo cha rukya cha halali Na cha batili? Inasemekana kunawengine wanasoma rukya huku wakimshirikisha muumba kwa njia isiyo halali
Ukiwa sio mcha Mungu ukisoma kisomo cha Rukya Jini au Shetani hawezi kuondoka katika mwili wa Binadamu kwani hicho kisomo cha Rukya kina masharti yake Maalum.

Sharti za Mtabibu
1.Anatakiwa awe anaswali swala tano kila siku.
2.Aache kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
3Asiwe mchawi.
4.Awe anafunga suna siku za Jumatatu na Alkhamis pamoja na masiku meupe.
5.Awe anapenda kusimama usiku katika ibada ya swala za usiku kama tahajjud.
6.Awe anafanya uradi kila siku na kuleta dua za kumuomba Mwenyezi Mungu ampe nguvu za kupambana na majini
 
JINSI MCHAWI ANAVYOMWITA JINI NA KUMTUMIA~2

NJIA YA KIGANJA CHA MTOTO

Njia hii ya kumuita jini muovu aliyehasi na kumtumia kwa kutumia kiganja cha mtoto mdogo ambaye hajabalehe ni njia inayofahamika sana na wachawi sababu ni miongoni mwa njia wanazozipenda sana kutokana na urahisi wake na wepesi wa kuleta majibu kwa kuhudhuria kwa jini husika anayeitwa eneo hilo.
Katika njia hii ya kutumia kiganja cha mkono wa mtoto mdogo anachokifanya mchawi wakati ameshakusudia kutaka kumroga fulani bin fulani au kuafnya kitu chochote kile humchukua mtoto huyo ambaye ni lazima awe hajabalehe na awe hayupo msafi wa mwili na mavazi yaani awe amejikojolea,amejinyea,au apakwe kinyesi,mkojo,damu ya hedhi au chochote kile ili mradi hatakiwi awe ni msafi.
Mtoto huwekwa chini na kisha mchawi akachukua kiganja cha mtoto huyu na huchora mraba[pembenne]na kando ya huu mchoro anaandika maneno ya kichawi na mara nyingi huandika maneno mazito ya kufru na kumtukana mungu pamoja na kuwatukuza majini wao,maneno hayo wanaandika pande zote4 za mraba.
Kisha pale katikati ya mraba huu anaweka maua ya alizeti na maua ya rangi ya blue au maua ya alizeti na wino rangi ya blue hapo kwenye mraba uliochorwa katikati ya kiganja cha mtoto huyo asiyejua chochote kinachoendelea maskini.
tibazetu.com
Kisha anaandika tarasimu fulani kwa herufi mojamoja juu ya karatasi ndefu ya pembe nne,halafu karatasi hii inawekwa juu ya uso wa mtoto na anavalishwa kofia halafu anaambiwa atazame kiganja chake na kama ataona chochote aseme,hapo sasa mchawi huyu aliyelaaniwa anaanza kusoma matarasimu na maazima yake mazito ya kichawi kutokana na jini husika anayemwita kuja kumtumia.
Ghafla yule mtoto ataanza kuhisi mwangaza unatokea kwenye kiganja chake na huanza kuziona picha zinachezacheza kwenyenye kiganja chake na hapo mchawi huyu atamuuliza mtoto ”unaona nini?” mtoto atasema ”naona sura ya mtu ananitazama”basi mchawi huyu anasema ”mwambie waambiwa na mwenye matarasimu haya ufanye kadhaa wa kadhaa..na picha ile itaashiria kukubali kulingana na amri ile na kuitekeleza…
Basi hii ndiyo njia mjawapo katika njia nyingi wanazotumia wachawi, laana za Mwenyez mungu ziwe juu yao,katika kumuita mshirika mwenzao shetani wa kijini na kufanya uharibifu kwa watu wengine..MWISHO



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…