Hivi huwa mnasomaje ili kufaulu Mitihani?

Hivi huwa mnasomaje ili kufaulu Mitihani?

Usinikumbushe mkaka mmoja olevel alikua na bidii vibaya mnooo
Kwenye makosa ya kuchelewa kukusanya kazi humkuti, kukimbia vipindi humkuti

Muda wote anasoma, anamuuliza mwalimu maswali ila matokeo yakija yeye ni wa mwisho.
Ubaya tulikua na mitihani kila wiki na kila wiki lazima achapwe.

Ilifika kipindi walimu wakawa hawamchapi tena sababu wanaona juhudi zake ila ndo hivyo kitabu kinamkataa.
Iko ndo kitu tunakimisi waafrika wengi,uenda huyo jamaa alikuwa na mashinikizo nyuma yake,alikuwq anafanya ambacho hajakipenda toka moyoni,bali anafanya kwa kutii shinikizo toka mahala,hivyo alipaswa kuelekezwa kwa kuojiwa kujua kipi anapenda,lkn hiyo yafaa ijulikane tangu uko awali (kindergarten),hapo ndipo walioendelea utuzidi sana tu,mifumo yetu ya elimu yafaa kubadilika sana tu,kwenda huko.
 
Nikieleza namna ya kucheza na nyota hutaamini kwa kuwa umejikita sana kwenye hizi dini za kigeni. Utaniona kama taahira.
 
Back
Top Bottom