Hivi, huwa ukiongea peke yako unaongea na nani?

Huwa ninaongea alone, nafeel amani kabisa, na huwa najishushua endapo negative thought ikipop in, nikiwa nimetulia huwa yaani as if nimekaa na mtu pembeni mnapiga stori I feel kabisaaa there is someone ila ninakua mwenyewe. Hii kitu bana.... Nilidhani ni peke yangu kumbe ni watu wote nikawa nashindwa simulia kuhofia kuonekana mwehu.
 
Zamani nilikuwa kama wewe niliogopa mno kuandika habari za kiroho na ushirikina...niliona kabisa nitaonekana wa ajabu au mwendawazimu kabisa...nikawa audanganyifu 1amwingi naandikia MMU NA PHOTOS
Baadae nikaona nitoe woga niandike! liwalo na liwe , basi nikaanza ila haikuwa rahisi kihivyo kueleweka
Kilichotokea kidogo niache kuandika changamoto zikawa kubwa mno..wakajitokeza watu wenye mawazo mgando hawa kazi yao ilikuwa ni kutoa kejeli na kashfa na matusi....inahitaji roho ngumu mno kuweza kudili na watu wa jinsi hiyo...lakini hatimaye taratibu walianza kuyeyuka mmoja baada ya mwingine, siku hizi jukwaa limetulia lakini pia nadhani hata moderators wa sasa wamefanya kazi yao
 
duh! hii kali mfano nikiota nimekufa je?
 
Mwanzo ni mgumu siku zote, na wengi wapiga kelele huwa ukiwapa nafasi hawana wanachojua zaidi ya kuponda as if they were born to be critics [emoji16] [emoji16] akili yao haifikirii nje ya chumba. Pole saana ila najua kupitia wao umejifunza mengi na jinsi ya kuishi na watu wa namna hiyo, wamekufanya uwe strong zaidi. Mi nakupa big up sana.
 
Niliwasemehe tu kwakuwa nilikuwa na hakika hawajui kuwa mimepitia wapi na kujifunza nini
 
Mimi huwa naona vitu vingi via ndoto, na ndoto hizo nisipoelewa huwa zinajirudia mpaka nielewe au nizifanyie kazi. Nikizifanyia kazi zinapotea, juzi kati kuna nyumba nilikuwa nataka kuhamia. Mara nikaiota kabla sijapelekwa na nilipopelekwa nikaikuta ni ile ile niliyoiota.

Kuna ndoto inanijia kila mara ila bado sijaing'amua ni nini natakiwa kufanya. Naona nataka kupigwa risasi lakini yule anayetaka kunipiga either anazuiwa au ananisamehe... Sijaielewa natakiwa kufanya nini...

Nyingine kuna mahali natakiwa kwenda yaan kusafiri, sasa nimeiona hiyo safari kwamba nilipofika huko tukaambatana na ndugu zangu wengine. Njiani kukawa na mtaro wa maji kama vile mto lakini pamezibwa kwa miti. Nikawaambia ndugu zangu kuwa mimi naweza kupita juu ya hiyo miti wakanikataza nikaacha. Ghafla akapita mtu mwingine mpita njia tu akajaribu kupita juu ya ile miti akazama kwenye maji.

Mimi ndiye nikawa wa kwanza kumsaidia kutoka na kumpa huduma ya kwanza kwa mtu aliyedumbukia kwenye maji kisha nikampeleka kwao. Ndoto ikaishia hapo sikuona mwisho wa ile safari yangu na ndugu zangu. Labda kadri siku zinavyokwenda nitaiona...

Samahani kutoka nje ya mada. Je una uelewa wa hizo ndoto mkuu mshana jr??
 
Nimeipenda hii Mada bw.mshana,embu endelea kidogo kuna kitu nataka kukisikia kuhusu self knowing
 
duh! hii kali mfano nikiota nimekufa je?
Ukiota umakufa. Inamaana wamekuua ktk ulimwengu wa kiroho

Lakin kama nilivyosema hapo juu .tumepewa mamlaka ya kubatilisha na kutangua.

Ukiamka tu anza kusali au kama ni usiku umeamka anza kusali na kubatilisha hicho kifo jinenene maneno ukifuatisha maneno katika Neno la Mungu.

Ila kikubwa kumbuka kuanza na toba; sababu unaingia ktk ulimwengu wa roho kimaombi

Ukitaka kuingia ktk ulimwengu wa roho kuna sheria lazima ujitakase kwa damu ya Yesu lazima uombe toba ktk huo mlango ambao shetani kautumia

Inawezekana kabisa alikua ana haki ya kukumaliza sababu huwez jua nan kafungua huo mlango huko nyuma yaan wale walio tutangulia.

Takasa hilo lango la afya yako ( uhai) kwa damu ya Yesu ( ile damu ya pasaka ya Kristo sababu pasaka wetu amekwisha tolewa. Ukisoma
1corintho 5:7F kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka yaan Kristo.


Kumbuka kambi ya shetani wanatumia damu wanatoa kama sadaka ili kuwasiliana wao wao ktk ulimwengu wa kiroho . damu za watu na wanyama.

Na sisi ni hivyo hivyo tunatumia damu tofaut yetu sisi tuna Damu ya Yesu ambaye alitolewa kuwa sadaka hatuna haja ya kuchinja vingine. Ni Damu yenye nguvu sana ukiitamka amini kuwa inafanya kazi( AMINI)

Hata kama usipo shuhudia katika macho yako ya rohon yakupasa uamin.

Sasa beba hiyo Damu ( kwa imani ) inyunyize katk lango lako la afya ama uhai waki ktk ulimwengu wa roho .

Mwambie Mungu naomba toba kwaajil yangu na kwaajili ya familia yangu tutakase kwa Damu ya Yesu.
Hata kama shetan kapata uhalali wa kuniua nami nakuja kwako kwa damu ya Yesu takasa hilo langu la uhai wangu na afya yangu kwa damu ya Yesu

Nami nanyunyiza damu ya Yesu katika miimo na vizingiti vya malango.

Navunja maagano yote yaliyofanyika soma

kutoka 12:22 Nanyi twaeni tawi la hisopu; mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini; na kukipiga kizingiti cha juu; na miimo miwil ya mlango; kwa hiyo damu iliyo bakulini.......

23 Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao wamisri; na hapo atakapo poiona hiyo damu katika kizingiti cha juu; na katika ile miimo miwili; Bwana atapita juu ya mlango; wala hata mwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.

*Ukisoma vizuri hapo juu utaona wana wa Isreal walitumia damu ya mnyama na Mungu hakurusu mwenye kuharibu aingie awaharibu wao.

Sasa hiv sis tuna damu ya Yesu ambayo ni damu yenye agano bora kuliko vyote. Tuje ktk Damu ya Yesu sasa wewe paka damu ya Yesu ktk miimo miwil na kizingit cha juu ya lango lako ktk ulimwengu wa roho lango la uhai wako na afya. Kwa Imani .

Funga mlango ambao shetan ameutumia kuku ua ( funga kwa Damu ya Yesu)

Fungua mlango wa uhai ( afya ) kwa Damu ya Yesu mkabidhi Mungu hilo lango.

Hapo utaona kuwa Mungu rud juu kusoma hapo mstar wa 23 Bwana atawapiga wamisri ( wamisri maana yake hao waliokuua walio kunenea mabaya; wanao kunenea laana; na kila aina ya uchafu walio kuitikia) mwambie Mungu shughulika nao hao watesi

Mwambie Mungu wahukumu hao watu ( kwa Mungu kuna viti vingi kimojawapo ni cha hukumu)

Mwambie Mungu naleta hii kesi madhabahun kwako hukumu mwenyew. Nifanyie haki( kwa kuwa Mungu ni Mungu wa haki pia)

Baada ya hapo waweza batilisha hayo maneno au hicho kifo walicho kunenea tangua. Na wafute hao mashahid walio kuona umekufa ktk ndoto

Wafute kabisa kwa Damu Ya yesu
Karibisha shahid Roho Mtakatifu na malaika washuhudie uhai wako sasa kwa Kuwa Mungu amerejeza uhai wako.

Ukirud huko juu mwanzo kabisa utakuta vifungu soma kwa imani na vitamke kwa Imani.

Ukiona nafsi inaogopa isemeshe nafsi yako kuwa kuna Tumaini kwa Mungu ni kuwa vita si vyako bali na vya Bwana .

Kutoka 23:20c ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako na mtesi wa hao wakutesao

Kutoka 14:14
Bwana atawapigania ninyi; nanyi mtanyamaza kimya

Kutoka 20:4
Kwa maana BWANA; Mungu wenu; ndiye awaandamaye na kwenda kuwapigania juu ya adui zenu; ili kuwaokoa ninyi.

2nyakati 20:15f.
BWANA akawaambia hivi; Msiogope;wala usifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu .


* haijalishi wapo wengi kias gani haijalishi kwani walio upande wako ni wengi kuliko walio katika upande wao


2falme6:16
Akamjibu; Usiogope; maana wallio pamoja nasi ni wengi kuliko walio pamoja nao.

* semesha nafsi yako itie nguvu ili uombe kwa iman na hakika yote.

Kumbuka kuwa wewe ni unaomba na mtendaji ni Mungu aliye hai.

Ushawahi waza kuwa unasema kitendeke hiki wewe umekaa tu na mtu anafanya kitu. ( assume una mtoto una mtuma)

Sasa leta akili yako ktk ulimwengu wa Roho sasa Mungu anataka tu useme kitu sababu amatupatia mamlaka ya kila kitu.

Sisi tuna full control ktk hii dunia sema bado hatujakaa sawa au hatujui nafas zetu ktk ulimwengu wa roho na mwil.

N:B. Kumbuka sio vyote uotavyo vinatokea na pia kuoata kuwa umekufa sio tu ni kufa inaweza kuwa kufa kiuchumi; afya; au kila ukifanyacho hakiendi

Kwa leo naishia hapa.

Mungu atulinde kwa damu Ya Yesu.
 
Tuendelee kumwamini na kumuomba zaidi kwani ndie tunaemtegemea.
 


AMEEEEEEEEEEN
 
Una ndoto za maono ila kwa nyongeza naomba nimwalike DIVINE yuko vizuri kipande hiki
 
Nimeipenda hii Mada bw.mshana,embu endelea kidogo kuna kitu nataka kukisikia kuhusu self knowing
Hii ya self knowing/self realization ni mada nyingine lakini ngumu sana niombee nipate wepesi wa kuiweka katika lugha inayoeleweka kwa urahisi , huku ikisimama katikati ya imani na maisha ya kawaida
 
Hii ya self knowing/self realization ni mada nyingine lakini ngumu sana niombee nipate wepesi wa kuiweka katika lugha inayoeleweka kwa urahisi , huku ikisimama katikati ya imani na maisha ya kawaida
Ukiinena kwa lugha za kusafiri ndio itakua pasua kichwa
 
Una ndoto za maono ila kwa nyongeza naomba nimwalike DIVINE yuko vizuri kipande hiki
Thnx bro naomba nimjibu kesho; cz nw nitashindwa andika vya kutosha; had nipekue Biblia yangu.

Nahitaji vifungu vya kutosha; bt it seems anaelewa vitu kutokana na sms yake sema anataka uhakika.

Nitamrudia kesho kumjibu
 
Thnx bro naomba nimjibu kesho; cz nw nitashindwa andika vya kutosha; had nipekue Biblia yangu.

Nahitaji vifungu vya kutosha; bt it seems anaelewa vitu kutokana na sms yake sema anataka uhakika.

Nitamrudia kesho kumjibu
Usisahau pia tuna mada yetu ya malango, panapo wepesi kesho tuiweke hewani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…