Mimi huwa naona vitu vingi via ndoto, na ndoto hizo nisipoelewa huwa zinajirudia mpaka nielewe au nizifanyie kazi. Nikizifanyia kazi zinapotea, juzi kati kuna nyumba nilikuwa nataka kuhamia. Mara nikaiota kabla sijapelekwa na nilipopelekwa nikaikuta ni ile ile niliyoiota.
Kuna ndoto inanijia kila mara ila bado sijaing'amua ni nini natakiwa kufanya. Naona nataka kupigwa risasi lakini yule anayetaka kunipiga either anazuiwa au ananisamehe... Sijaielewa natakiwa kufanya nini...
Nyingine kuna mahali natakiwa kwenda yaan kusafiri, sasa nimeiona hiyo safari kwamba nilipofika huko tukaambatana na ndugu zangu wengine. Njiani kukawa na mtaro wa maji kama vile mto lakini pamezibwa kwa miti. Nikawaambia ndugu zangu kuwa mimi naweza kupita juu ya hiyo miti wakanikataza nikaacha. Ghafla akapita mtu mwingine mpita njia tu akajaribu kupita juu ya ile miti akazama kwenye maji.
Mimi ndiye nikawa wa kwanza kumsaidia kutoka na kumpa huduma ya kwanza kwa mtu aliyedumbukia kwenye maji kisha nikampeleka kwao. Ndoto ikaishia hapo sikuona mwisho wa ile safari yangu na ndugu zangu. Labda kadri siku zinavyokwenda nitaiona...
Samahani kutoka nje ya mada. Je una uelewa wa hizo ndoto mkuu
mshana jr??
Naomba nianze kujibu kipande kimoja kimoja;
Tukianza na hicho cha safari.
Hiyo ndoto ipo waz kabisa na inaelweka.
Upo kwa ajili ya kusaidia watu; kingine unatakiwa ufike ngazi fulan sijajua kwa upande upi ila bado hujafikia.
Muombe Mungu akuvushe akufikishe safari aliyo indaa yan ngaz unayotakiwa kufika muombe Mungu akufikishe.
Njian kuna vikwazo muombe Mungu avitoe.
Tuje kwenye hiyo kupigwa risasi;
Muombe Mungu aingilie kati.
Yawezekana una kosa au kuna kosa lilifanyika huko nyuma.
Rud kule juu kuna mtu kuna mtu nili muelezea jins ya kuomba toba; ( toba una ruhusu Mungu akusaidie aingilie kati)
Muombe Muombe Mungu aingilie kati.
Ukiiachia hiyo ndoto huyo mtu akikupiga risas ata deposit vitu kama ni sumu au kitu kibaya;
Sababu ndoto ni mlango pia ambao Mungu anautumia na shetan anatumia.
Ndoto ikijirudia ujue ni ya kuifuatilia; ina maana.
Na kama umeota huelew una haki ya kuomba kwa Mungu kujua nn fasir ya ndoto au omba Mungu airudishe tena kwa uwaz ili ujue nn maana yake.
Huko kuomba fasir na ufahamu wa ndoto si ombi la siku moja ni kila cku
Muombe Mungu.
Bt hiyo ya kupigwa risas si ndoto nzur inaweza ikakuharibia ktk real life.
Muombe Mungu aingilie kati.
Sijajua if nimekujibu vizur cz kufasir ndoto bado sijafikia huko vzr nafahamu kidogo sana.
Rudi juu kule kusoma nilichoandika kuhusu yule mtu aliyeota amekufa kuna some hints utapata