Hivi huyo Magoti, mshauri wa Rais kuhusu siasa, alikuwa na uzoefu upi wa mambo ya siasa? Mbona CCM ina manguli wa siasa jamani?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nimeshangaa kusikia Magoti ndiye alikuwa anamshauri Rais kuhusu siasa. Nikimuangalia ni kama ana umri wa miaka thelasini hivi, yaani mtoto tu, na ndio maana mwanzo nilidhani ni mhudumu au afisa wa kawaida tu pale ikulu.

Hivi katika "msitu" wa wazee waliokomaa kisiasa kama Steven Wasira, Mizengo Pinda, Sumaye, Mzee Makamba, Paul Kimiti na wengine wengi kweli Rais anachaguliwa Magoti ambaye hajawahi kugombea hata uenyekiti wa mtaa au kijiji ili akaifahamu siasa kuanzia saiti?

Rais Samia awe anawakataa wasaidizi wengine, asikae nao kwa sababu ya hali zao na huruma tu. Hawa akina Magoti ndio wale wanageuka kuwa madalali wa kumkutanisha Rais na watu.

Nilisikia hata muuza madafu anasema alilipwa na Magoti fedha nyingi ambazo hajawahi kuziona kwa kuuza baskeli chache tu za madafu, sasa hizo nyingi ni nfapi, na kwa nini muuza madafu azione nyingi kuliko mzigo aliouza, na wangapi wanalipwa nyingi, na kwa nini.

Kwa hesabu zozote zile, Magoti is too juniour kumshauri Rais kuhusu siasa, badala yake Rais ndiye anaweza kumshauri Magoti kuhusu siasa. Samia ameogelea katika bahari kuu ya siasa na anagajua mapapa na nyangumi yanayoishi latika bahari kuu ya siasa.

Mh. Rais, usiishie kwa Magoti tu, piga chini wengine wengi ambao "hawajaiva" kumshauri Rais
 
Sidhani kama wewe ni mfatiliaji mzury wa haya mambo magoti si wa Leo au Jana pale ikulu ni WA MDA mrefu pia amefanya kazi na mwanakwenda , kiufupi tunaitaji watu tofauti kuleta na kuchochea mambo tofauti tofauti na siasa Ina mambo mengine hujui alikuwa ana mshauri katika eneo gani mkuu kuwa kiongozi katika eneo flani haitegemei hapo awali ulikuwa na cheo gani kama ulivyo sema hakuna ana mwenyekiti wa shina nk
 
Nchi yetu ina maajabu mengi sana ndugù yangu.

Tumeachana kabisa na meritocracy tumehamia kwenye sijui uchawa + kujipendekeza + kujuana na huruma

No wonder tupo hapa na tutaendelea kuwa hapa kwa muda mrefu sana kimaendeleo.

Kuna watu wengi sana wenye uwezo, experience ya kutosha na weredi mkubwa sana ila hawateuliwi nafasi hizo kwa sababu mfumo wa nchi yetu ejiondoa kabisa kwenye meritocracy
 
Sasa mzee makamba atashauri nini kuhusu siasa za Sasa?
 
Tatizo viongozi wengi wa Afrika ni weupe kichwani, kwahiyo huwa wanapenda kufanya kazi na watu wabovu kichwani.

Mama alipopewa tu urais akajawa na hofu kufanya kazi na watu smart kama Lukuvi, Kabudi, Bashiru na Polepole. Akawafyekelea mbali, akabakiza akina Magoti. Magoti akili ipo magotini kweli.
 
Usimdharau mtu kwa hali yake Mungu huweza kukupa majibu muda wowote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…