Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Bora kelele ya m2 unayempnda kuliko kelele 100% kwa watu usiowapnda inaumzaaaa
 
Tatizo ulimbukeni wa maisha! Kama mwanamke inakupasa kua na kifua cha kutunza baahdi ya mambo sio kila kitu uijuze kadamnasi ambayo haitokusaidia zaidi ya kukudharau.

Sent from my SM-T715Y using JamiiForums mobile app
 
Ninyi huwafanya wake wetu kutuona hatuna upendo kwa maigizo yenu ya mitandaoni, LEO MUNGU AMEKUUMBUA???
Ok, anza kuishi KIUALISIA uone raha yake, KARIBU MGENI!!!

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Waliosema kosea kote ila usikosee kwenye suala zima la kuoa,waliona mbali aisee.
 
Jamaa aliingia chaka mbaya, lakini ilibidi ajiulize kwanza kwa nini aliachana na mme wa kwanza!! Mwanamke ropo ropo kama huyu ni hatari kwa ustawi wa ndoa
 
kumbuka huyu ni mkewe na wana watoto. hapo watoto ukute wakirudishwa ada,hakuna chakula home ,umeme umeisha etc usihukumu mkuu? je kuna mume hapo?
Hakuna mke wala mume hapo...yan dada huyo alipokosea ni kuja tu kuyaanika hayo mambo yake..dah wazungu hawa wanatuua katika nyanja yani
 
Huyu mwanamke anakosea kuyaanika haya. Je vipi huyu anaeng'ang'ania mali za familia wakati watoto wanahitaji kuishi?
Kuna wanaume wanaachana na wake zao wanaacha magorofa for the sake of the kids.


Kwa tabia za wasichana wa kichagga na kipare, usikute tayari huyu Joyce analiwa na rafiki wa kamanda na ndiye anayempa hela za mtaji wake. Na pengine kamanda naye kagundua hivi na ndiyo maana anafanya anayoyafanya ili kumkomesha binti.
 
Nimependa pale KAMANDA KOMAA...yani akomae kumyonya bintbwa watu fala kweli huyu kileo na ni bwege kweli tena baradhuli yani mse nge...yani mwana hizaya mavi ya kuku kamanda gani unang'ang'ania vya mwanamke ambacho kinasaidia watt wako
 
Joyce bhana daaah

Akina joyce wote wanalostisha tu mcheki na yule joyce waziri mlostishaji tu

Be carefull na akina joyce

Huyu dada anampenda kileo nasemaje kilewo endelea kukaza kamanda hadi heshjma adabu na utii vije then utaachia au sio

Huyu hawezi kukimbia ni wako tu .halafu we usijibu kitu tulia tulia huo ndio uanaume
 
Jamaa kauzu balaa na mapigo yote ya upande wa pili hajajibu chochote tu?
Na aendelee hivyo hivyo kukausha wala asijibu ni hadhi yake kiume itakapo kuja

Huyu joyce atabweka sana ila atarudi kwenye mstari hana ujanja tena ni nani atakayekubali kuwa nae akiachana na jamaa kwa haya mambo yankauanika mambo.yake ya ndani hadharani.

Ni usichana bado anao akikomaa kiakili atajiona alikuwa mjinga sana.
 
Pole sana mama, hata kujianika mtandaoni inatosha kujua udhaifu uko wapi.
 
Hapo hata akiachika hakuna Mwanaume wa kumuoa....nani aje akubali kuanikwa hivi pindi ikitokea kutoelewana...
 
Mhh!mbombo ngafu!Ila Joyce hizo ni siri za ndani na familia yako kwa ujumla hukupaswa kupost huko Insta.Suala kama hili ulipaswa mlimalize kifamilia,je hamna wazazi?ndugu jamaa na marafiki? Unachokifanya ni kujianika kwenye public ambayo kimsingi haina msaada kwenu zaidi ya kukucheka na kukuhurumia kinafiki.
Mumeo hata kama amekosea hukupaswa kuja kulalamika insta,kila mtu akileta matatizo yake insta ndoa nyingi zisingekuwepo.Kama unaona imefika mwisho ni bora uachane naye ,ingekuja tu stori Joyce kaachana na Kileo basi but kwa unachokifanya unajidhalilisha wewe mwenyewe na mumeo!
But pole kwa yote magumu unayopitia tafuta njia sahihi za kumaliza tatizo lenu na sio Instagram.
Dah hakika umeongea vyema sana, na hio anachofanya ni ulimbukeni tu

Sent from my SM-A520F using JamiiForums mobile app
 
Hawa wanawake wengine ni shida, ya ndani analeta hapa mtandaoni kweli dah. somenihapo chini (instagram)

View attachment 688048

  • joycekiriasuperwoman
    Kilewo baba Watoto wangu, yaliyotokea ilibidi yatokee ili kila Mmoja aanze upya safari ya Maisha Yake. Wakati tunaanza huu mwaka nilikuambia huenda mwaka huu tukaachana! Unakumbuka? Well, Lakini jambo moja nakusisitiza hapa, Nimekuomba sana uniachie biashara zangu nisimamie, ili na wewe usinamie biashara zako kutokana na Changamoto zetu hasa za kiuchumi. Wewe Pesa zako unazopata kwenye biashara zako hutaki kushea, Ila Pesa zinazotoka kwenye biashara zangu unataka tushee. Najua ni ujinga wangu wa kukupenda sana ndo umeniponza. Labda ningetenganisha Mapenzi na biashara tusingeishia huku.

    Wakati mimi nasajili Kampuni Yangu nilikuweka kwenye kampuni bila shida yoyote na wakati nafungua akaunti za bank nilikuweka pia. umekuwa ukijua kila ela inayoingia pamoja na matumizi yote kwa sababu lazima tusaini Wote na ndiyo Raha ya Mapenzi.

    Wewe ulipofungua Kampuni yako uliweka pia jina langu kitu ambacho nilipenda sana, lakini ulipokwenda kufungua akaunti ya bank HUKUNIWEKA. Kiukweli SIKUPENDA, mbaya zaidi ukataka kuwa unasaini Pesa zako kivyako.

    Japo nilianza kuona mashaka Lakini nilijipa Moyo, labda ukipata utanishirikisha pia kama Mimi nilivyoamua kukushirikisha kila kitu changu. PESA MWANAHARAMU buana, pale tuu ulipoanza kazi na kampuni yako Ndipo SHIIIDA ilipoanzia, hukutaka kushea hata senti Nyumbani wakati biashara zangu kwa Kipindi chote cha Miaka NANE zimeendesha familia yetu bila tatizo.
    Kuna Miradi mbalimbali ambayo ulikuwa ukionyesha NIA ya kuifanya lakini yote ilifeli. Hivyo haikuwa rahisi KUKUJUA kwa upande wa KIUCHUMI sura yako ikoje... Ulijaribu biashara hizo kwa mtaji wa Familia bila kuona matokeo chanya, Pesa zikawa hazirudi lakini tukajipa Moyo biashara ndivyo zilivyo. Mwisho nikakushauri mtaji wa biashara tukope Bank labda utakuwa na nidhamu zaidi ya Pesa ya Mkopo kuliko kutoa ela Nyumbani. Hukupenda huo Ushauri, ukaona nakubania.

    Sasa MWAKA huu 2018 tuliongea mengi pale Bahari beach, juu ya mahusiano Yetu na Changamoto zake! Pamoja na yote tuliyoongea nikakuomba kila mtu asimamie biashara zake, kisha tukubaliane kwenye MAJUKUMU ya Familia kwamba nani atafanya Kipi. Lakini pia nikakuambia kwamba Niko radhi kuendelea kutimiza hayo majukumu. [HASHTAG]#SIR[/HASHTAG]
Nilifikia uamuzi huo baada ya kuona unaficha PESA zako. Ile Siku niliyokubamba unatoa Ela kwenye akauti yako kwa Siri na hapo tulikuwa hatuna ela kabisa NILIUMIA kuliko hata ningekufumania. Yaani nilikuona huna NIA na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI. Najua Kazi ulizofanya hata kama NI Ndogo hukukosa hata mkate au sukari ya kuleta Nyumbani. Lakini ukaamua kula bata, hutoki na Mimi, Mara nyingi ukiwa na ela unatoka peke yako unarudi mpaka asubuhi... ukijua kuna punda wako hapa nyumbani atafanya kila kitu.

Kilewo najua Haya siyo mageni kwako, tumeyaongea kwa muda mrefu sana. Tumewashirikisha watu wa karibu. Pamoja na hayo yote Kilichonishangaza sasa ni wewe kukataa kuniachia biashara zangu wakati wewe una za kwako. Tena unasaini akaunti yako peke yako halafu akaunti Yangu nimekuweka tunasaini Wote.

Kilewo kwa staili hiyo ya maisha nilianza kukosa Furaha sana na wewe kwa kuona unanitumia wala huna NIA Njema na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI, huku Ndani MAPENZI YAKAPOTEA KABISA. Mpaka juzi birthday yako sikuwa najiskia kukuwish. Lakini kwa ajili ya Watoto nikajilazimisha. Ngoja niishie hapa.

KILEWO baba Watoto wangu, Dunia inajua NINAVYOKUPENDA. Tatizo langu kubwa na wewe unajua fika siyo wewe kutokuwa na Pesa, BALI KUTUSHIRIKISHA KWA KIDOGO UNACHOPATA wewe kama BABA wa Familia. kwa Sasa nina tatizo kubwa na wewe la kunipiga baada ya kuamua 2018 nitakuwa natoka peke yangu kujipa raha. Unajua sehemu ninazokuwaga nikiwa nimetoka na ndo sababu ulikuja ukanikuta, lakini uliamua kunipiga. Kesi ipo Dawati.

Kilewo ningekuwa na NIA mbaya nisingekuweka kwenye biashara Yangu, nimenunua Viwanja Goba na Bagamoyo, bila uwepo wako, lakini nilikuja kukushirikisha na wewe ukaenda kuongeza majina yako. Sikuwahi kulalamika maana NAKUPENDA na wewe ndo Baba Watoto wangu. Nimetamani kuzaa mtoto wa Tatu lakini kwa ambushi zako nimeogopa. Mambo ya KOMAA KAMANDA hapana. Nikasema Wawili wanatosha.

Kilewo wangu nakuomba tena na tena uniachie biashara zangu niweze kuendelea kutunza hawa Watoto wetu. Toka unipige umeondoka siwezi kutoa ela, hatuna Chakula nyumbani, Madeni ya wafanyakazi, Nyumba nadaiwa n.k
[HASHTAG]#SIRIZANDANI[/HASHTAG]
Hamna mke hapo aisee, kwa huo upupu.

Sent from my SM-A520F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom