Wanawake bwana! Ukiona anakushirikisha kitu ambacho kwa kawaida huwa ni siri, ujue baadaye itakula kwako.
Ukiona Mwanamke anakwambia Mume wangu password ya simu yangu ni hii (akakuonesha) ujue kesho atakuganda kama sisimizi umuoneshe password yako. (kwa ajili ya nini wanafanya hivi sijui, Ila ni wivu tu wa mali).
Na ukiona Mwanaume amekususia mapato ya biashara flani (kwa mfano duka, au pango la nyumba) akakuambia hakuna shaka kwa kuwa unang'ang'ania. Alafu akakususia au akakuruhusu kila kitu kwenye mapato ya biashara nk, Kaa ujue eee mwanamke huyo mume wako ana nyumba au miradi mikubwa na mingi zaidi ya hicho alichokuachia.
Wanaume wengi wanatabia ya simba au chui Ni wakali sana katika umiliki wao, Lakini ukiwa mkali na ukadinda ktk level yao huondoka na kuhama kabisa kutafuta sehemu tulivu na yenye maslahi kwao.
Wanawake mtulie,
Ama mtahangaika sana na wanaume.