Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

kupata mtu ambae mna lengo moja nayo changamoto mkuu.kuna watu wabinafsi sana . hv mtu unakuwaje mchoyo hadi kwa damu yako eti.japo tunamuona joyce mbaya ila na huyu kamanda sio kabisa aaah
Unajua ukipata nafasi ya kuwa mwanaume u will not judge..

Mwanaume ndio dira ya familia.. Na sio Leo tu for many years imekuwa hivyo. Tinafikiria tofauti sana.. Mwanaume ni kuwa ma uwezo kuwa kuthubutu..

Nahapo ndio usiri lazima uje.. Maana wanawake wanapenda assurance.. Kunapokuwa na tabu..baba anaondoka kwenda kutafuta nchi ya mbali sio kwamba hawapendi watoto..ila akibakia mtakula nn?!

Njaa ya siku moja haiui familia.. Na watoto watakula nn wakati huu baba anahangaika kutengeneza kikubwa cha baadae ..mama anakuwa mbunifu.. Ndio maana tuliwahi kunywa uji usiku tukiwa wadogo.. Kuvaa nguo za kaka yako siku ya sikukuu.. Maana hamfi kwa kukosa soseji Sikh mbili.. Mtafurahia sana kama matibabu na ada za chuo kikuu zitakuwepo pindi zinahitajika..

Familia itakuwa na raha zaidi kama wakati wa kuanza maisha watoto wazazi watakuwa financially stable wasiwasumbue watoto kutimiza ndoto zao.. Yote haya yanakuja na sacrifice.. Na hapo ndio kizazi chetu kinapokwama.. Hatujui kujitoa..we only live today!

Kwa kesi ya hawa wawili..kuna makando.kando mengi has a kwa huyu Dada.. She is entitled.. Na kwa watu Wa namna hiyo kaa nao mbali...wanaomini lazima wapate things their way..
 
Usimlaumu yeye ni mwanamke na anajielewa sana ila fikilieni nje ya box kwann ameweka maisha yake katika mitandao? Hilo ni swali gumu sana jibu analo mwenyewe....

Jambo lingine kumbuka yeye n kioo cha jamii anafuatiliwa na wanawake wengi sana hapa tz hivyo kwa ww mwanaume na isitoshe unaweza kuwa huna familia na mpaka leo una miaka 29 bado unaishi kwa baba unajifanya una mkosoa kwa alichokifanya, fikilia kwanza ana nia gani?...


Jambo la mwisho pia kumbuka ni mfanyabiashara, mwanamke mchapakazi, hivyo hujui ana nia gani au ana mipango gani katika mwaka huu dhidi ya biashara zake nina imani hii ni moja ya mipango yake ya mwaka2018 hakika atafanikiwa
 
KILEWO atakuwa amebanwa na kazaramo kamoja ka mbagala rangi tatu ni mauno kwenda mbele.Ugali dagaa na mchicha na amani ya roho.Stress ya nini na vijisenti vya masimango hela unatoa kwa MUSHI unaleta tutumie na mimi nikitaka kwenda kula na Zainabu unanitangaza!!! Ngoja nibaki na Zainabu wangu nikiwa na amani na hata instagram hajui na hajasoma hata meseji zenu
 
Wahaya wanawezana wenyewe kwa wenyewe maana kwa ngono hawajambo.Hata akiwa profesa tabia zake kwenye hio sekta hua ni zile zile kama za ambae hajasoma.

Endeleeni kuoana tu nyie kwa nyie mkuu.
Ni bora kuoa mpenda ngono kuliko mjing
 
Ila Kilewo anajuwa kuwaweza ...nyie mnampost mnamtukana ila yeye kimya tu....alafu uyu Joyce kilia mbona anaganga njaa wakat anajiipa super woman.....watoto wawili mbn it's very easy kuwalea ...tena vizuri tu ....kwa mtu anayejiita super woman ...awez kukosa..kulea watoto wawili...by the way hapo Amna...Cha sisi kujadiri...maana mapenz niyawawili...tu.
 
  1. copied
  • KANUNI 30 KWA WANAWAKE NDANI YA NDOA 1). Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima. 2). Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako. 3). Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha. 4). Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka. 5). Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo. 6). Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako. 7). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe. 8). Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na kumshajiisha. 9). Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo. 10). Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu. 11). Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake. 12). Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitajio namba moja la mwanaume ni heshima. 13). Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo. 14). Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani. 15). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo. 16). Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridhawa. 17). Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu. 18). Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo licha ya kwamba unapata pesa zaidi yake. 19). Usisahau kuwa mume anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha. 20). Iwapo mawazo yako yamefanikisha jambo kuliko mawazo yake, usijilinganishe naye. Bali ishini na mfanye kazi kama timu. 21). Usiwe msumbufu kwa mumeo. Hakuna mume anayependa mke msumbufu. 22). Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi. 23). Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula. 24). Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake. 25). Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli. 26). Usisuhubiane na wanawake wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa. 27). Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa. 28). Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri. 29). Umri usiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa. 30). Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako. Ninakutakia ndoa njema. Usisahau ku share na wenzako kusambaza ujumbe huu muhimu kwako na kwa wengine wapenda maendeleo
 
1. Anataka awe mwanaume wa familia.
2. Anataka awe anashililia miradi yote ya familia.
2. Brain washing kwamba bado anampenda mumewe.
 
Kioo cha jamii gani? Hiyo jamii anaifunza nn kwa huu upuuzi anaouandika? Jamii ya matabulalasa pekee inaweza kujifunza kupitia huyu mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…