Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hapo hakukuwa na mapenzi kabisa.hapo ni pesa tu zinazoleta dhahama ya yote Haya
 
Huyu mama anapoandika hayo mtandaoni hajui watoto wake wanakua na wataona alivyokuwa anatoa siri za ndani... Japo mzee anaweza kuwa na makosa lakini mama hakutakiwa kuanika siri namna hiyo. Mitandao hasa kwa sasa ni kumbukumbu tosha.
 
Sifurahii haya ya Joyce na Kileo ila kama kweli Kileo ndiyo alivyo kifamilia Mimi ningeondoka mapema mno na wala Watoto nisingezaa naye. Wanaume kupe wa Mlima Kitonga ni shida mno. Ni kuwakimbia kama ukoma.
 
Hivi huyu mwanamke kakosa njia nyingine za kufix hili tatizo zaidi ya kuendelea kuanika kwenye mitandao? Is marriage conflicts and misunderstanding solved this way?
 
Mimi kama nimemuelewa tofauti Joyce anisamehe. Lakini akili yangu inanituma kuamini kuwa baada ya Joyce kuanika sakata hili kwenye media na shutuma alizopata toka kwa wachangiaji, sasa ameamua kuja na episode 2 ili watu wajue chanzo cha ugomvi wao ni ubahili/ubinafsi Wa mumewe na hii anadhani itamsaidia ku atract public sympathy. Lakini ukisoma vizuri maelezo yake unamwonea huruma kwa sababu between lines ameficha tabia yake na anachotaka kiuhalisia toka kwa mumewe. Lakini pia angalau ameeleza chanzo cha kupigwa kwake kuwa ni yeye kwenda "kujirusha" peke yake kama anavyofanya mumewe ili ngoma iwe droo, na anataka jamii ione kuwa kipigo toka kwa mumewe hakikuwa sahihi kwa vile alimkuta sehemu anayoifahamu na hakuwa akifanya zinaa kama yalivyokuwa mawazo ya mumewe. Tatizo la pili la Joyce ni kutofanywa Second signatory kwenye akaunti za mumewe wakati yeye amemfanya signatory kwenye akaunti zake. Katika hili Hoja ya Joy ni ya msingi lakini siyo nzito. Anakiri wakati hili linafanyika hakuona tatizo kwa sababu alikuwa na mapenzi thabiti kwa mumewe. Kwa maana nyingine kinachomfanya ahoji sasa hivi ni kupungua kwa hayo mapenzi thabiti ya awali. Sasa ni kipi kimeyapunguza hayo mapenzi? Ni pale Kilewo alipoacha kumjali na kumthamini, yaani kutoka out peke yake bila mkewe.
Je, haya ni ya kuanika hadharani hata kama kweli yapo? Jibu rahisi ni no, tena big NO! Kinachofanya ayaanike haya kwa sasa ni dhamira yake anayosema alimwambia mumewe tangu mwanzoni mwa mwaka huu, hajataja ni lini, kuwa "MWAKA HUU 2018 NI MWAKA WA KUACHANA".
Huwezi kudumu katika mahusiano kama akili yako umeshaiset kuachana. Ukilala unaota kuachana, ukiamka unawaza kuachana. Siku zote mawazo yanaumba dhamira na mwisho wa siku "UTEKELEZAJI". Joyce unatekekeza ulichokiwaza siku nyingi na sababu ulizotoa ni catalyst. Yaani ulitegesha kama wimbo mmoja Wa Mrisho Mpoto anaposema; "UKINIKANYAGA TU.....!"
Lakini Joy hujachelewa, la kwanza nakusihi acha kutumia njia hii ya kishamba kumdhalilisha mwanaume unayemuita baba Wa watoto wako, na sehemu nyingine umemuita "KILEWO WANGU". Tafuta wenye busara wakusaidie ama KUACHIKA kwa amani au KUREJESHA ndoa yako katika line.
Wasalaam;
Bila bin Bila!!

Hongera umemsoma vizuri, mimi nilipoambiwa tu kuwa huyu elimu yake ni darasa la saba na alikuwa house girl (ingawa si darasa la saba na house girls wote wako hivyo), sikutaka hata kuhangaika.Mwenzako hapo yeye anaona sifa kwamba ataongeza followers, yaani kifupi huyu mwanamke ni mjinga na jamaa kama ana akili akimbie mbali sana, huyu atamdhalilisha mpaka siku anaingia kaburini. Kwa upeo wake mdogo hachagui cha kuongea na aongee wapi. Nina mfano hai kama huu, mpaka mume aliingia kaburini kwa mateso ya mke wa namna hii jamaa akiwa msomi mkubwa.
 
Dadangu Ndoa ni swala pana sana, kiukweli huwezi muanika MUme wako ivi tena Mwanaume Aliyekuzalisha!
Swala siyo mume aliyekuzalisha, akisha kuwa mume wako huyo ni mwandani wako. Hata kama ana tabia za aina gani huwezi muanika hivi, iwe ni kwa ndugu au marafiki sembuse kny mitandao.
 
Mwanamke akitakata jina kwa namna yoyote ile akajulikana, akashika pesa, akwa adicted ktk mitandao ya kijamii, akawa anakutana na makundi ya watu wenye chapaa makundi tofauti tofauti ni nadra mno familia kubaki salama hasa baba, unaweza kulishwa sumu ukafilia mbali zilipendwa wewe, mwanamke sio ndugu ni rafiki basi.
 
Hivi huyu kilewo hajafanya jambo lolote jema kwa Dada yetu au maisha yao yote amekuwa mkaidi..

Wanawake ni watu wabaya sana hawakumbukagi wema wanachopenda kusema ni mabaya ya mwanaume tu...

Hapo sasa anataka tuamini kwenye hiyo ndoa yeye alikuwa right muda wote wa mahusiano ila jamaa ndio mzinguaji
 
Watu wengi wanacomment in one side ya kuona Mwanamke kakosea ila yapaswa kujua chanzo cha ugomvi mpaka Mwanamke kufikia uku..katika ndoa kila MTU ana wajibu wake kwa mwenzake jambo lolote linapotokea
 
Mapenzi yamegawanyika katika sehemu kuu 2
Sehemu ya kwanza ni Faraja kicheko pamoja na Furaha...... Utadhani Dunia hii ndugu yote ni yako
Sehemu ya Pili ni kasheshe ugomvi pamoja na chuki..... Polisi mahakamani watu kufikishana...
" wimbo huu wana ndoa tuusikilize sana.....ukistaajabu ya DJ Nelly utakutana na ya Kilewoo" Asante Joyce unaendelea kuwaandikia watoto wako historia ambayo wataikuta na kuiishi
 
watoto huyo kilewo amewatelekeza bila chakula
Sio kweli pesa za kujilusha awe nazo za chakula cha watoto zisiwepo kisha mambo haya hawaelewi yanawaathiri watoto kwa kiasi gani shule wanaathirika sana kisaikolojia shule wangeacha ugonvi uwe wao usihusishe watoto
 
Back
Top Bottom