Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hivi kweli unamuamini huyu mama anachosema kuwa Kilewo anakatazia hela isitoke kuwalisha watoto wake na kulipa pango? Huyu mama si angekwishafukuzwa ndani ya nyumba kama pango halipi?

Kuna matobo mengi sana katika hii tamthilia anayotulisha huyu mama huko Insta.
Mwenyewe nimedoubt sana, nadhani anataka talaka tu.
Kilewo sio mpmbavu kiasi cha kutelekeza familia
 
Nakubali aisee..mimi ni mchaga ila hawa dada zetu hapana.
Kuna dada wa kichaga nilikua nioe alininyoosha mnyoosho mmoja sina hamu naoo aiseee...
Saivi namnyemelea muiraki
KAribu sana Mbulu, Dongobesh, Tumati, Daudi usisite kuwasiliana na mimi!
 
Wewe dada naona una tatizo la uelewa au unajitowa akili tu.

Unaelewa maana ya joint account? Hakuna mwenye share zaidi ya mwenzake, kama mnaona hili ni jambo rahisi kwa sababu mwanaume ameamuwa kukaa kimya basi mshaurini Joyce afuate mafundisho ya biblia ya samehe saba mara sabini, na mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia, na mtu akikunyang'anya kanzu basi mpe na joho kabisa, sasa mshaurini Joyce ajitowe kwenye hiyo account amuachie Kileo maana mnaropoka ujinga tu mtadhani mna uhakika wa mnachoaminishwa.

Mkumbuke yule mama aliyelia mbele ya Magufuli anadhurumiwa mirathi ameshindwa kesi mahakamani.
Nyooooooo......

Akalishe makalio mwenzie atafute halafu amuachie kirahisi

Huo ni wizi wa kuaminika

Na dume zima kung'ang'ania akaunti ya mwanamke ni upuuzi.....ila wanaume wa miaka hii ni matatizo

Unaanzaje kulishwa na mkeo?(ilhali huna tatizo lolote) na chakula anakula kinashuka hajui kilipotoka....

Akaunti anazui hajui hata pesa zikupotafutwa kisa tu mkewe alimwamini akamfanya kuwa signatory????

Na yeye kilewo alivyoficha akaunti zake ni sawa?

Pamoja na matatizo ya joyce lakini Ubinafsi na uslope wa mwanaume umechangia matatizo katika hii ndoa

Halafu huko aliko yupp comfortable hajui hata wanae wanaishie...mfyuuuu
 
Ni biashara zipi alizozikalia naomba unielimishe hapa nashindwa kuelewa.
Duh..kama umesoma vizuri ukaelewa ni kwamba Jamaa kawekwa kama partner kwenye biashara ya mwanamke ingawa ana zake..akaunti wanasaini wote ili watoe pesa..Jamaa kapotea, kaacha familia..mwanamke hawezi kutoa pesa bila Jamaa..kama anataka kuondoka ajitoe kuwa signatory ili mama aendelee na kulea familia..akili za viongozi wa chadema zina shida hasa unapokuja kwenye masuala ya familia..
Tundulissu hakuwa na mahusiano mazuri na mkewe kabla hajavunjwa kiuno, mbowe na mkewe Dr Lilian mtei nao ni shida hadi zitto aliwahi kumchana hadharani, haya mwingine huyo, kina sugu hata hawaeleweki nae na mzazi mwenzie walishaachana..lema baada ya kutikiswa sana kisiasa ndio kaamua kutulia na mkewe..
 
Nyooooooo......

Akalishe makalio mwenzie atafute halafu amuachie kirahisi

Huo ni wizi wa kuaminika

Na dume zima kung'ang'ania akaunti ya mwanamke ni upuuzi.....ila wanaume wa miaka hii ni matatizo

Unaanzaje kulishwa na mkeo?(ilhali huna tatizo lolote) na chakula anakula kinashuka hajui kilipotoka....

Akaunti anazui hajui hata pesa zikupotafutwa kisa tu mkewe alimwamini akamfanya kuwa signatory????

Na yeye kilewo alivyoficha akaunti zake ni sawa?

Pamoja na matatizo ya joyce lakini Ubinafsi na uslope wa mwanaume umechangia matatizo katika hii ndoa

Halafu huko aliko yupp comfortable hajui hata wanae wanaishie...mfyuuuu
Sasa huyu Kileo amepata wapi wakati tumeambiwa yeye ni marioo hana lolote?

Hivi huwa mnashirikisha ubongo wenu kabla hamjarishwa taarifa za kusadikika?

Ni kwa nini haendi mahakamani? Umeshajipa muda wa kujiuliza swali hili?

Kwa sababu kimsingi hapo hakuna ndoa tena, ile misingi inayofanya watu muwe wanandoa ikifa na ndoa imekufa, je ni kwa nini Joyce haendi mahakamani?

Huu ujinga wake anajuwa kuna wajinga wenzake humu mitandaoni ndio mtamuelewa lakini siyo kwenye court of law.
 
bado na stick na 90% ya wanaume waliojibu upupu wako katika troubled relationship.
MWANAUME RIJALI MWENYE AKILI TIMAMU NARUDIA TENA MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KUSAPOTI HILI SWALA LA JOYCE
 
Hiy

Hiyo ni old fashion wengine hatuendekezi huu ujinga hutaki kuchangangia akae nyumbani alee watoto


Ukienda kwa hoja hii kua mwanamke achangie gharama za nyumbani utaishia ugomvi tu....

Wanaume tumeumbiwa mizigo,hua tunabeba bila kuongea kitu,ndio uanaume!

Hii concept ya kumtega mke eti aanze kuchangia 50% ya nyumba unakaribisha maneno...atatoa 10% ila ataongea nchi nzima wajue anahudumia familia 100% mwanaume uonekane kiazi tu.Unawajua wanawake mkuu au unawasikia?

Hizi propaganda za Joyce unaziona za nini?Wanawake waache kabisa,sio wenzetu kiivyo unavyodhani mzee!

Acha kabisa!
 
Nimeanza na kusema 'huyu mwanamke anakosea'.......sasa hapa ndio inabidi mwanaume aoneshe tofauti yake na huyu mwanamke. Wagawane mali gani na huyo alikuwa analelewa tu. Mali za huyo dada mropokaji. Ukikubali kulelewa kuwa mpole.
Biashara zilianzishwa kwa majina yao mawili wakati wako kwenye ndoa.

Sheria inataka wagawane nusu kwa nusu huku kiasi kikubwa kikitengwa kwa watoto.

Hapa hela za benki, viwanja vya nyumba, na miradi mingine?
NUSU bin NUSU.

Hivi ndivyo wanavyofanyiwa wanaume sasa afanyiwe Joyce nae. Mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu, eh?

Mali za huyu mama zitapona tu kama Kilewo alisaini PRENUPTUAL AGREEMENT. Lakini yule mama alivyompenda Kilewo wakati anaolewa sidhani kama alikumbuka hilo la prenap.
 
Ila Joyce bwana nawe hueleweki kipindi alikuwa anagombea ubunge ulikuwa unaropoka mitandaoni unaonekana kabisa pesa mbele angeshinda ubunge sijui kama yangetokea haya. By the way pole sana kwa yanayoendelea kukupata huenda ndio kidogo unapunguza stress yatoe yote usijekupata stroke bure
 
Pande mbili

[HASHTAG]#WANAUME[/HASHTAG]
Anayosema ni kweli na ni aibu kwa wanaume!!
[HASHTAG]#WANAWAKE[/HASHTAG]
Anavyoropoka kjwenye public ni aibu kwa wanawake!!
 
Hawa wanawake wengine ni shida, ya ndani analeta hapa mtandaoni kweli dah. somenihapo chini (instagram)

View attachment 688048

  • joycekiriasuperwoman
    Kilewo baba Watoto wangu, yaliyotokea ilibidi yatokee ili kila Mmoja aanze upya safari ya Maisha Yake. Wakati tunaanza huu mwaka nilikuambia huenda mwaka huu tukaachana! Unakumbuka? Well, Lakini jambo moja nakusisitiza hapa, Nimekuomba sana uniachie biashara zangu nisimamie, ili na wewe usinamie biashara zako kutokana na Changamoto zetu hasa za kiuchumi. Wewe Pesa zako unazopata kwenye biashara zako hutaki kushea, Ila Pesa zinazotoka kwenye biashara zangu unataka tushee. Najua ni ujinga wangu wa kukupenda sana ndo umeniponza. Labda ningetenganisha Mapenzi na biashara tusingeishia huku.

    Wakati mimi nasajili Kampuni Yangu nilikuweka kwenye kampuni bila shida yoyote na wakati nafungua akaunti za bank nilikuweka pia. umekuwa ukijua kila ela inayoingia pamoja na matumizi yote kwa sababu lazima tusaini Wote na ndiyo Raha ya Mapenzi.

    Wewe ulipofungua Kampuni yako uliweka pia jina langu kitu ambacho nilipenda sana, lakini ulipokwenda kufungua akaunti ya bank HUKUNIWEKA. Kiukweli SIKUPENDA, mbaya zaidi ukataka kuwa unasaini Pesa zako kivyako.

    Japo nilianza kuona mashaka Lakini nilijipa Moyo, labda ukipata utanishirikisha pia kama Mimi nilivyoamua kukushirikisha kila kitu changu. PESA MWANAHARAMU buana, pale tuu ulipoanza kazi na kampuni yako Ndipo SHIIIDA ilipoanzia, hukutaka kushea hata senti Nyumbani wakati biashara zangu kwa Kipindi chote cha Miaka NANE zimeendesha familia yetu bila tatizo.
    Kuna Miradi mbalimbali ambayo ulikuwa ukionyesha NIA ya kuifanya lakini yote ilifeli. Hivyo haikuwa rahisi KUKUJUA kwa upande wa KIUCHUMI sura yako ikoje... Ulijaribu biashara hizo kwa mtaji wa Familia bila kuona matokeo chanya, Pesa zikawa hazirudi lakini tukajipa Moyo biashara ndivyo zilivyo. Mwisho nikakushauri mtaji wa biashara tukope Bank labda utakuwa na nidhamu zaidi ya Pesa ya Mkopo kuliko kutoa ela Nyumbani. Hukupenda huo Ushauri, ukaona nakubania.

    Sasa MWAKA huu 2018 tuliongea mengi pale Bahari beach, juu ya mahusiano Yetu na Changamoto zake! Pamoja na yote tuliyoongea nikakuomba kila mtu asimamie biashara zake, kisha tukubaliane kwenye MAJUKUMU ya Familia kwamba nani atafanya Kipi. Lakini pia nikakuambia kwamba Niko radhi kuendelea kutimiza hayo majukumu. [HASHTAG]#SIR[/HASHTAG]
Nilifikia uamuzi huo baada ya kuona unaficha PESA zako. Ile Siku niliyokubamba unatoa Ela kwenye akauti yako kwa Siri na hapo tulikuwa hatuna ela kabisa NILIUMIA kuliko hata ningekufumania. Yaani nilikuona huna NIA na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI. Najua Kazi ulizofanya hata kama NI Ndogo hukukosa hata mkate au sukari ya kuleta Nyumbani. Lakini ukaamua kula bata, hutoki na Mimi, Mara nyingi ukiwa na ela unatoka peke yako unarudi mpaka asubuhi... ukijua kuna punda wako hapa nyumbani atafanya kila kitu.

Kilewo najua Haya siyo mageni kwako, tumeyaongea kwa muda mrefu sana. Tumewashirikisha watu wa karibu. Pamoja na hayo yote Kilichonishangaza sasa ni wewe kukataa kuniachia biashara zangu wakati wewe una za kwako. Tena unasaini akaunti yako peke yako halafu akaunti Yangu nimekuweka tunasaini Wote.

Kilewo kwa staili hiyo ya maisha nilianza kukosa Furaha sana na wewe kwa kuona unanitumia wala huna NIA Njema na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI, huku Ndani MAPENZI YAKAPOTEA KABISA. Mpaka juzi birthday yako sikuwa najiskia kukuwish. Lakini kwa ajili ya Watoto nikajilazimisha. Ngoja niishie hapa.

KILEWO baba Watoto wangu, Dunia inajua NINAVYOKUPENDA. Tatizo langu kubwa na wewe unajua fika siyo wewe kutokuwa na Pesa, BALI KUTUSHIRIKISHA KWA KIDOGO UNACHOPATA wewe kama BABA wa Familia. kwa Sasa nina tatizo kubwa na wewe la kunipiga baada ya kuamua 2018 nitakuwa natoka peke yangu kujipa raha. Unajua sehemu ninazokuwaga nikiwa nimetoka na ndo sababu ulikuja ukanikuta, lakini uliamua kunipiga. Kesi ipo Dawati.

Kilewo ningekuwa na NIA mbaya nisingekuweka kwenye biashara Yangu, nimenunua Viwanja Goba na Bagamoyo, bila uwepo wako, lakini nilikuja kukushirikisha na wewe ukaenda kuongeza majina yako. Sikuwahi kulalamika maana NAKUPENDA na wewe ndo Baba Watoto wangu. Nimetamani kuzaa mtoto wa Tatu lakini kwa ambushi zako nimeogopa. Mambo ya KOMAA KAMANDA hapana. Nikasema Wawili wanatosha.

Kilewo wangu nakuomba tena na tena uniachie biashara zangu niweze kuendelea kutunza hawa Watoto wetu. Toka unipige umeondoka siwezi kutoa ela, hatuna Chakula nyumbani, Madeni ya wafanyakazi, Nyumba nadaiwa n.k
[HASHTAG]#SIRIZANDANI[/HASHTAG]
Jocye kaaa kimya weka hakiba ya maneno,Kileo amekaa kimya sababu anajua wewe ni mama wa watoto wake,anakujali sana ndio maana amekaa kimya embu na wewe kaa kimya yamalizeni haya ndani ya familia.
 
Back
Top Bottom