Hivi huyu Joti huwa anawachekeshaje watu?

Hivi huyu Joti huwa anawachekeshaje watu?

Mimi naonaga tu ana maneno mengi lakini sioni uchekeshaji wowote. Yupo kama Kevin Hart, umachachari mwingi lakini content hamna.

Sasa hapa lengo lilikuwa kuchekesha, japo kazingua hapo kuingiza katiba lakini hata kuchekesha kwenyewe hakupo.

Huwa anawachekeshaje?


Nahisi shida yako hapa si joti, bali huyo aliyempaisha.....hapo ndo kwenye shida yako.
 
Kuchekesha watu ni kazi kubwa ya kuiba akili,nafsi na mawazo ya mtu ili umuhamishe utakavyo na afurahie utendalo au uongealo.Sasa,mtu anachezeshachezesha kope na kuvaa matambara makakioni ndiyo anataka ucheke!Ajabu hii!
Kwahiyo kuchekesha mpaka ujiite Nishai Mtombangile Kitwango Mikazo???
 
Hakuna Comedian Tanzania zaidi ya Mandonga tu.
 
Joti hachekeshi.
Yule Mzee wa mizengwe sijui anaitwa nani..nikimuona tu kabla hajaongea chochote nacheka
Kabisa, kabisa, anaitwa Sumaku. Ana maneno mengi kweli na anajua
 
Kuna watu joti aliwapoteza now ameshuka Sana , kwenye YouTube channel yake kuna jamaa anaitwa kipande , na Sopa na Madame kiukweli hawa walimweka juu Sana joti kipindi ametengana na original commedy , amewafukuza now kabaki mtupu kabisa
Una uhakika kawafukuza?
 
Sure mkuu

Kipande

Sopa

Mama dame

Afu nafkir maslahi ni madogo ...huyu jamaa ofis yake ilikua pale kinondoni studio ....nyumba moja pamoja na studio ya Man-water

Ilikua wakitoka location wanapika wanakula afu kila mtu anaenda kwake

Niliangalia ile lifestyle nka conclude kuwa alikua anawalipa hela ndogo pengine ndo maana wamekimbia

Sopa siku hz ana kisehemu pale sinza kwa remi anauza soup asubuh ...ukienda pale unamkuta jikoni anakimbiza

Vijana wameamua kujiongeza
Pia naona ana acc yake youtube anapost comedy
 
Nyonyoma kwa mbali, baadhi ya clips zake ni nzuri. Pia watu wa cheka tu huwa wanaotea punchlines hapa na pale. Ukweli ni kuwa sekta ya comedy bongo haina tofauti na wenzao wa bongo movie. Contents zao za kitoto sana.
Wanazidiwa hata na wakenya.
 
Mimi naonaga tu ana maneno mengi lakini sioni uchekeshaji wowote. Yupo kama Kevin Hart, umachachari mwingi lakini content hamna.

Sasa hapa lengo lilikuwa kuchekesha, japo kazingua hapo kuingiza katiba lakini hata kuchekesha kwenyewe hakupo.

Huwa anawachekeshaje?


bora joti kidogo unaweza kujikuta umecheka. kuna pimbi mmoja anaitwa mkojani, hata huwa sielewi wanaomuweka hadi kwenye video wana pesa ya kupoteza sana.
 
Nampenda sana joti,ni muigizaji mzuri sana,labda kama una personal conflict naye
 
Back
Top Bottom