Hivi huyu mtu anayejiita Mfalme Zumaridi anatuchukuliaje?

Hivi huyu mtu anayejiita Mfalme Zumaridi anatuchukuliaje?

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Nimetizama mahojiano ya huyu anayejiita mfalme Zumaridi na Mtangazaji wa Clouds, Millard Ayo na nimebaki na maswali mengi sana lakini kubwa ni kwamba ANATUCHUKULIAJE WATANZANIA?

Zumaridi anasema akiwa darasa la 3 alitokewa na Mungu akiwa na umbo la jua lakini usiku, kwa hiyo yeye aliweza kuangalia jua tena lililotokea Usiku.

Anasema yeye ameshaenda Mbinguni mara nyingi sana na mbinguni kuna nyumba za ghorofa na alipoenda motoni alikuta watu wanamlilia awaokoe wengine wanaongea kisukuma.

Zaidi anasema ameshakutana na Ibrahimu ambaye alimtambulisha kwa Eliya na Yakobo, na eti aliingia kwenye ofisi ya Mungu. Ningehoji Wasukuma mnatukuliaje sisi lakini nitaonekana mkabila, naacha tu.

Mwenye muda akatazame kwa Millard.

Screenshot 2023-03-13 at 21.08.00.png
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hii dunia ina machizi mengi sanambona wengi tu wanasema wameongea na Mungu. Msamehe bure tu kuna kitufe cha mawasiliano kichwani kwake kilinyofoka[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Walimuonea bure thus walikosa ushahidi, ajiweke karibu na walamba asali kama wafanyavyo wenzake, hata wakiua watu hamna kesi, na sio vi askari vidogo tu vinamtupa selo mwaka kwa kesi za ukomozi zisizo ushahidi, eti human trafficking wanaijua human trafficking kweli hao.
 
Back
Top Bottom