Hivi huyu mtu anayejiita Mfalme Zumaridi anatuchukuliaje?

Hivi huyu mtu anayejiita Mfalme Zumaridi anatuchukuliaje?

Nimetizama mahojiano ya huyu anayejiita mfalme Zumaridi na Mtangazaji wa Clouds, Millard Ayo na nimebaki na maswali mengi sana lakini kubwa ni kwamba ANATUCHUKULIAJE WATANZANIA?

Zumaridi anasema akiwa darasa la 3 alitokewa na Mungu akiwa na umbo la jua lakini usiku, kwa hiyo yeye aliweza kuangalia jua tena lililotokea Usiku.

Anasema yeye ameshaenda Mbinguni mara nyingi sana na mbinguni kuna nyumba za ghorofa na alipoenda motoni alikuta watu wanamlilia awaokoe wengine wanaongea kisukuma.

Zaidi anasema ameshakutana na Ibrahimu ambaye alimtambulisha kwa Eliya na Yakobo, na eti aliingia kwenye ofisi ya Mungu. Ningehoji Wasukuma mnatukuliaje sisi lakini nitaonekana mkabila, naacha tu.

Mwenye muda akatazame kwa Millard.

View attachment 2549515[/B]
Millard ayo nae vipi!??
 
shwaini na nusu hizi dini tukifanya mchezo ndizo zitatupeleka motoni
najutia kwa serikali ilimuweka ndani pale ndipo alipopata credit ona sasa waandishi wa habari kila uchao wanamfutatilia
NB ;Binadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa
 
Back
Top Bottom