Hivi huyu rafiki yangu anaweza kuwa mtu wa aina gani?

Hivi huyu rafiki yangu anaweza kuwa mtu wa aina gani?

Uyo jamaa wako yuko kama mimi tu.

Mie kuzulula sjui kijiweni siwezi. Me nikitok job ni nyumbani na I work from home. Siwez kutoka kuzulula tu bila sababu ya msingi.

Na kama natoka basi nakua na lengo maalum, mfano naenda sehemu fulani kufanya kitu fulani then narudi zangu home immediately. Weekend nakua home na siku zozote siendi job nashinda home hata siku kadhaa fresh tu

Mimi ni mpenzi wa Volleyball so jioni saa 11 mpaka sa 1 nakua kucheza Volleyball. Mida unaobaki (ukiondoa job) nakua zangu home na mama chanja wangu.

Kuhusu nyimbo mie nina nyimbo zangu chache kila siku lazima nisiskilize
  • iyo by diamond
  • enemy solo by awilo x p square
  • sifa - by light bearers
  • upendo by light bearers

Hizi nyimbo nafuatisha kwa kuimba kabisa, naeza kaa kimya nyimbo zote ili zikfika hizo lazima niimbe na nafurahia sana.

So kwa upande wangu sioni shida ya jamaa.
 
Hii tabia wakati mwingine inachangiwa na malezi kwa kiasi kikubwa, kuna wazazi wasiopenda kabisa watoto wao wakacheze mbali na nyumbani, hawa muda mwingi wa makuzi yao wanakuwa kwenye mazingira ya nyumbani pekee.

Hivyo hawa hata wakikua, wakaanza kujitegemea, kwasababu walishazoea mazingira ya nyumbani, kutokwenda mbali, kuzungukwa na waliowazoea kila siku, inakuwa ngumu kwao kuja ku adopt ukubwani, japo baada ya muda wengine huanza kubadilika taratibu.

Wengi aina hii mara nyingi hata confidence huwa hawana, wanakuwa wenye aibu, wasioweza hata kukaa mbele ya wengine, mara nyingi hupenda palipo na wengi, wao wawe nyuma tena ikibidi hata uwepo wao usitambulike, pia huwa na maneno machache waliotawaliwa na tabasamu la muda mfupi wakiongea vichache vyao.
Huyu ni mie kabisa. [emoji23][emoji23]
 
Wewe kama Watanzania wengi huwezi kunielewa kwa sababu hata serikali yako inakupa haki ya kupigiwa kura uchaguliwe kuwa mbunge au rais kuongoza nchi, halafu inakuwekea vikwazo kwenye kuitumia haki hiyo kwa kukuambia huwezi kuitumia mpaka uwe mwanachama wa chama cha siasa.

Yani kuanzia kwenye serikali ushalelewa kutoelewa maana ya haki yako.

Siwezi kushangaa mimi nikikueleza habari za haki usiponielewa ukaona naitumia vibaya, tena unasema kimkato hata bila kueleza naitumia vibaya vipi nikuelewe.

Kwa sababu huna point ya kunielewesha naitumiaje haki vibaya.
[emoji625][emoji625]
 
Dah nkajua unaniongelea
Kumbe sio mimi
Mimi napenda mpira ila ni yanga tu!
Mipira ya nje napenda matokeo tu hasa ya match ngumu zenye kuongeleka
2 nkiipend nyimbo moja nta play hiyo hadi ikome
Wakati mwingine utakuta ni ya zamani sana
Mfano now nipo na ya darasa ft sani boy sogea 🔥
 
Inatokea tu mkuu coz me binafsi kama cna kinachoweza nitoa nje ya Nyumba bas nitakaa ndani ninashinda na boxer, Milango sifungui na hata chakula napigia boda alete mtaani yaani ni kuangalia latest movies na series na nikichoka nitacheza Ps5 na game ninayopenda kucheza sana ni Ghost of Tsushima... So hapo ni mpaka night na next day ikiwa haielewek basi ni the same routine na sichoki
 
Huyo ni mtu anayependa routine.

Anapenda mazingira anayoyajua, hapendi mapya.

Ndiyo maana hata muziki akipata anaopenda anakaa nao huo huo anaupiga mara nyingi.

Ndiyo maana anapenda kukaa ndani alipopazoea tu.

Hii inaweza kuwa dalili ya kuwa kwenye autism spectrum, au ni tabia yake tu.
Naungana na wewe mkuu
 
NWewe huyo sio rafik yako... Yeye anakujua ila wewe humjui... Yeye anakuelewa wewe humuelewi... Inshort achana na maisha yake fanya yako... Hana shida yoyote INTROVERT huyo
Ni kweli mkuu INTROVERT ni wepesi kuwasoma , na kuwajua watu
Kinyume chake ss kuwaelewa wao ,😁
 
Huyu Ana tabia Kama za wajomba zangu wawili wote Sasa ni marehemu Mungu azilaze roho zao mahali pema,na hiyo tabia wamemrithisha mtoto wa dada yangu kuanzia asubuhi mpaka jioni husikii sauti yake kimya anacheza game na kusikiliza music akitoka mazoez akirudi ndani kimya hila bwana juzi Kati nimegundua ni mvutaji mzur wa bangi baada ya kunyatia mlangoni kwake usiku wa manane na kukutana na harufu ya bangi Zaid ya Mara mbili
 
Watu hatufanani mkuu Kuna watu tunapenda kua peke yetu haitusumbui Ila Mara nyingi inawasumbua wanaotuzunguka nakumbuka nikiwa primary Sina hili Wala like mama akaja akaniuliza eti una shida gani? Nikamwambia sina shida yoyote akaniambia mwalimu Fulani kaja kamuambia nitakua na tatizo la kisaikolojia kwa sababu ni mkimya Sana na sishirikiani na wenzangu kwa hiyo wanipeleke kwa mtaalam wa saikolojia nilishangaa maana Mimi nilikua najiona naongea tu vizuri na nacheza na wenzangu vizuri, hatukuongelea Tena Hilo suala mpaka nilivyojua mkubwa Ila mpaka Sasa hivi kila hatua ya maisha niliyopita comment huwa Ni zile zile utasikia we mpole,. we mkimya, mwingine anakuuliza hivi huwa unaongea kweli? Mbona unapenda kujifungia fungia, Kuna siku kazini mtu aliniambia watu wa aina yako ndio huwa wanajinyonga bila taarifa nikashangaa Sana maana sijawahi kwa na mawazo hayo hata.
Inabidi watu mjifunze kua binadamu hatufanani kitabia na Mara nyingi huwa mnaproject hisia zenu yaani Kama wewe ukikaa ndani muda mwingi unakua na stress unahisi kila anayekaa ndani ana stress hapana sio wote wako hivyo.
Yaani Kuna kipindi nikiwa chuo nilianza Hadi kujifunza tabia ambazo Sina ili tu nisiambiwe mpole sijui mkimya sijui nini baadae nikashindwa nikajua tu this is who I am kwa hiyo siku hizi naishi tu Kama mimi.Mtu alikiniuliza mbona mkimya Sana , mbona huongei namwambia naongea sana hujanifahamu tu vizuri.
Exactly, kuna personality nying sana. Ila coz of societal norms watu wengi wameishia kudhoofishwa coz wana act tofauti na wengine. Mm binafs siwez jichanganya sana na watu, hua inashasha energy level zangu.

Watu watakulable kila aina ya uchafu wanaohisi unakufaa coz upo tofauti na wao. It's si insane
 
Hiyo tabia hata mimi naifahamu mkuu.
Faida zake ni nyingi kuliko hasara kwa sababu kufanya hivyo hujiepusha na mambo mengi na ushawishi mbalimbali.
Watu wa aina hiyo huwa hawapendi makelele kutoka kwa watu wengine kwani huwa inawapa interference.
Faida nyingine ya watu wa hivi huwa wanafocus sana future/long term plans na huwa zinakuja imagination za success kichwani mwao jinsi itakavyotokea in future so kujichanganya na watu huwa wanahisi itamdisturb kisha itamtoa nje ya reli ya mipango yake.
Kutokana na hilo ili kupunguza athari ya upweke alionao ndio anatafuta kitu cha mbadala cha kumliwaza kama mziki ila aupendao ambao utagusa hisia zake na si kila mziki utamfaa,ukimbadilishia mziki usiogusa hisia zake pia atachukizwa na kuhisi makelele.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Nimepigia mstari. Hii ndiyo fact kuu.
 
Back
Top Bottom