Watu hatufanani mkuu Kuna watu tunapenda kua peke yetu haitusumbui Ila Mara nyingi inawasumbua wanaotuzunguka nakumbuka nikiwa primary Sina hili Wala like mama akaja akaniuliza eti una shida gani? Nikamwambia sina shida yoyote akaniambia mwalimu Fulani kaja kamuambia nitakua na tatizo la kisaikolojia kwa sababu ni mkimya Sana na sishirikiani na wenzangu kwa hiyo wanipeleke kwa mtaalam wa saikolojia nilishangaa maana Mimi nilikua najiona naongea tu vizuri na nacheza na wenzangu vizuri, hatukuongelea Tena Hilo suala mpaka nilivyojua mkubwa Ila mpaka Sasa hivi kila hatua ya maisha niliyopita comment huwa Ni zile zile utasikia we mpole,. we mkimya, mwingine anakuuliza hivi huwa unaongea kweli? Mbona unapenda kujifungia fungia, Kuna siku kazini mtu aliniambia watu wa aina yako ndio huwa wanajinyonga bila taarifa nikashangaa Sana maana sijawahi kwa na mawazo hayo hata.
Inabidi watu mjifunze kua binadamu hatufanani kitabia na Mara nyingi huwa mnaproject hisia zenu yaani Kama wewe ukikaa ndani muda mwingi unakua na stress unahisi kila anayekaa ndani ana stress hapana sio wote wako hivyo.
Yaani Kuna kipindi nikiwa chuo nilianza Hadi kujifunza tabia ambazo Sina ili tu nisiambiwe mpole sijui mkimya sijui nini baadae nikashindwa nikajua tu this is who I am kwa hiyo siku hizi naishi tu Kama mimi.Mtu alikiniuliza mbona mkimya Sana , mbona huongei namwambia naongea sana hujanifahamu tu vizuri.
Kwa watu tunaopenda kusoma mtu kukaa ndani peke yako si ajabu.
We are comfortable in our own company, maybe with a book to engage our minds.
Nakumbuka darasa la nne niliazimwa kitabu cha Willy Gamba cha Njama.
Sasa mtaani kwetu watu walikuwa wanaoenda dana kusoma riwaya za Aristablus Elvis Musiba za jasusi Willy Gamba, halafu vitabu vichache vinatembea nyumba hadi nyumba.
Basi niliazimwa kitabu nikaambiwa nikisome kwa siku moja tu nikirudishe.
Aliyeniazima alijua siku moja maana yake kaniazima leo asubuhi nitamrudishia kesho.
Nilikisoma kile kitabu siku ile kuanzia asubuhi mpaka jioni, jioni yake nikamrudishia nishamaliza kusoma.
Jamaa hakuamini speed yangu ya kusoma.
Sasa mtu hapa napiga piano, hapa naangalia movie, hapa nina games, hapa nina gym ina mazagazaga yote, hapa nina computer network with servers, laptops, desktops, including a Plex server, movies za Netflix na Prime just to mention a few, hapa nina library ina vitabu zaidi ya 10,000, hapa nina bar ina vinywaji vya kila aina, hapa nina music systems ambazo zinatosha kufungua nightclubs kadhaa, complete with DJ sets, all tye way to the garage, hapo natoka nje kufanya nini bila mpango maalum?
Na hata nikiamua kutoka nje natoka nyuma kwenye kwenye deck nina grill nyama choma ninavyotaka, nikitaka kuongea na watu nina simu ina unlimited internet, ambayo hata siitumii kwa sababu nina Wifi, hapo natoka kwenda wapi bila shughuli maalum?