Hivi huyu rafiki yangu anaweza kuwa mtu wa aina gani?

Hivi huyu rafiki yangu anaweza kuwa mtu wa aina gani?

Sawa Lakini hebu niambie ungekuwa jobless kama huyu jamaa yangu niliyekusimulia hapo juu je kuishe namna hii uishio wewe ingefaa kweli ??
Hapana hapo inabidi utoke ujichanganye. Kwa mimi kujichanganya naweza sana ila sipendelei.
 
Uzoefu alionao katika jamii ndio chanzo Cha baadhi ya watu kubadilika na kuwa watu wasiopenda kujichanganya mfano,Unaweza Kuta watu wanaomzunguka hawathamini mawazo yake Hali kama hii inaweza kumbadilisha mtu akawa siyo mtu wa kuchanganyikana na watu.
Uko sahihi sana
 
Nadhani hii inamuadhiri zaidi mtu anayataka mawazo yake yawe yanakubalika tu kila mara, mimi uwa napenda kuwa free pale tunapojadili mada furani yani kama ntatoa mchango wangu na watu wakaukataa ni sawa, kama ntakuwa na ushahidi juu ya kile nikiongeacho basi ntawaonesha wakikataa tena sina muda wakuendelea kubishana nao na maisha yanaendelea siwezi kaa mbali na watu kisa wanapinga mitazamo yangu
 
Katika mambo ya imani upo sahihi , ila kumbuka huyu ni mwanaume maisha ya kukaa kaka ndani awaachie wanawake , lakn pia katika mambo ya imani huko huko hakuna jambo (jaribu ) ambalo mwanadamu anakutana nalo likawa nje ya uwezo wake hivyo basi elewa hata hivi vishawishi vyote ulivyovisema au q
uvionavyo vipo ndani ya uwezo wetu katika kuvikwepa .
Ni vigumu lakini kumbadirisha mtu aliyezoea huo utaratibu.

Mwenyewe pia huwa sipendi kutoka kama sina sababu maalumu. Kama ni mpira basi utaona nimelipia Ving'amuzi vyote kuangalia mechi zote pasipo kutoka nyumbani.

Kama ni Vinywaji, utakuta kila aina ya Vinywaji kwenye Friji kwahiyo kama ni mpenzi wa moja baridi moto utaipata nyumbani.

Inaweza kuwa ni vigumu kwa wengine lakini binafsi naona kawaida as nimeshazoea.

Na ikitokea nimetoka na marafiki basi kufikia saa 4 usiku nitakuwa nimesharudi nyumbani.
Kama itakuwa zaidi ya saa 4 basi iwe kuna biashara au mchongo wa hela nausikilizia 😅

Hakuna mahali pazuri na salama kama Nyumbani.
 
Mimi binafsi napenda kukaa sana ndani kama nipo off, nitashinda nyumbani siku nzima, sipendi kelele, sipendi mziki, napenda sehemu tulivu

Sipendi mazingira mapya napenda kwenda maeneo ninayoyafahamu.
Sioni tatizo na watu ambao tayari mna namna ya kuishi , tatizo ni pale huna maisha hujui pesa utapata vipi afu unajifungia ndani lakin tisa kumi unasingiliza wimbo huo huo tuuu hii maana yake nn ?
 
Wakati mwingine ni vizuri kujipumzisha ndani kuliko kutoka kisha ukajikuta una tenda dhambi kwa kutazama hivyo vya Nje.

Imagine kumtazama Mwanamke kwa kumtamani umeshazini naye, kumbuka hapo Mjini Wadada wasivyopenda kuvaa nguo za ndani si utajikuta umezini na Dsm yote[emoji12]

Ndiyo maana jamaa ana epuka dhambi ndogo nndogo kwa kushinda ndani tu
MTU hajavaaa chupi nikimtamani zambi sio zangu ni zake yeye aliyeamua kututamanisha.

Ili usipate zambi hapa mjini uishi Kama zombie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo naye ana watu wanaopenda watu wa hivyo, kwa hiyo kwenye kuoa, anaweza kupatana na mtu anayependa watu wa hivyo.

Hapo ni kama ataamua kuoa, maana anaweza kukataa kuoa, na hiyo ni haki yake pia.
Kukataa kuoa ni Haki Ila sio sahihi kabisa. Wengi huishia uzinzi na punyeto ambayo ni mambo ya hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MTU hajavaaa chupi nikimtamani zambi sio zangu ni zake yeye aliyeamua kututamanisha.

Ili usipate zambi hapa mjini uishi Kama zombie

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha............yaani kuna dhambi nyingine ni kama zimewekwa ili kupunguza Idadi ya watu kuiona Pepo.

Imagine Kumwangalia kwa Kumtamani eti Utakuwa umeshalala naye🙆

Hii ingekuwa kuna nafasi ya Kubadirisha hiki kifungu kama Katiba tungeomba marekebisho aisee 😜
 
Watu waliosoma boarding school kuanzia form one mpaka form 6 ndio wanakuaga hvyo kuna dogo yaani home anaweza akajifungia ndani hata siku nzima ila nimekuja kugundua boarding school zinaharibu watoto.
 
Kwa nini unaona mtu kukaa ndani ni kuharibika?

Kuna watu ma genius wanakaa ndani wakifanya kazi zao zinazosaidia sana dunia.

Mfano, hii mitandao na mambo mengi ya computer yanatengenezwa na computer programmers ambao ni watu wa kukaa ndani sana wakifanya kazi zao za coding.

Na hao ndio wamekusaidia mpaka ukapata JF, Whatsapp, Facebook etc.

Ukaweza kutuma pesa kirahisi kwa miamala ya simu.

Sasa inakuwaje ukasema kirahisi kwamba kupenda kukaa ndani ni kitu kibaya?
 
Mimi nina mshkaji wangu ni mkimya sana, huyu anapenda kukaa peke yake tu.

Akiwa yupo free anavuta tu bangi kisha analala au ana sikiliza mziki basi.

Hata kwenye mishe mishe yupo hivi hivi hanaga story na watu yaan hata ndugu zake hana story nao.

Huyu mshkaji wangu tumekuwa wote toka wadogo yaan mimi tu ndo naweza kuongea nae sana, kwenye sehem ya watu wengi huwa haongei mpka umsemeshe ndo atachangia.

Ila nakumbuka zaman hakuwa hivi kuna muda nawazaga labda bangi inampeleka ila naona hamna yeye anasema tu hataki sana story na watu
 
Mimi naweza nikakaa ndani tuseme jumamosi yote na usijue kama nipo ndani,na sifa yangu napenda kuangalia vitu pasipo sauti hasa alja zeera,Discovered, ID extra.

Hivyo kila MTU na style yake
 
Watu hatufanani mkuu Kuna watu tunapenda kua peke yetu haitusumbui Ila Mara nyingi inawasumbua wanaotuzunguka nakumbuka nikiwa primary Sina hili Wala like mama akaja akaniuliza eti una shida gani? Nikamwambia sina shida yoyote akaniambia mwalimu Fulani kaja kamuambia nitakua na tatizo la kisaikolojia kwa sababu ni mkimya Sana na sishirikiani na wenzangu kwa hiyo wanipeleke kwa mtaalam wa saikolojia nilishangaa maana Mimi nilikua najiona naongea tu vizuri na nacheza na wenzangu vizuri, hatukuongelea Tena Hilo suala mpaka nilivyojua mkubwa Ila mpaka Sasa hivi kila hatua ya maisha niliyopita comment huwa Ni zile zile utasikia we mpole,. we mkimya, mwingine anakuuliza hivi huwa unaongea kweli? Mbona unapenda kujifungia fungia, Kuna siku kazini mtu aliniambia watu wa aina yako ndio huwa wanajinyonga bila taarifa nikashangaa Sana maana sijawahi kwa na mawazo hayo hata.
Inabidi watu mjifunze kua binadamu hatufanani kitabia na Mara nyingi huwa mnaproject hisia zenu yaani Kama wewe ukikaa ndani muda mwingi unakua na stress unahisi kila anayekaa ndani ana stress hapana sio wote wako hivyo.
Yaani Kuna kipindi nikiwa chuo nilianza Hadi kujifunza tabia ambazo Sina ili tu nisiambiwe mpole sijui mkimya sijui nini baadae nikashindwa nikajua tu this is who I am kwa hiyo siku hizi naishi tu Kama mimi.Mtu alikiniuliza mbona mkimya Sana , mbona huongei namwambia naongea sana hujanifahamu tu vizuri.
 
raha sana kuwa na self awareness nimependa
 
Back
Top Bottom