Kwa kifupi ukiona taifa lolote linayumba ujue Idara ya usalama ipo hoi na ndiyo maana kazi ya kwanza ya Rais akiingia ofisini asubuhi anaanza na faili la TISS.
Ata Israel yupo pale Middle East kwasababu
ya uimara wa Mosad na USA wanatamba kwasababu ya uimara wa CIA.
Kwaiyo ata Tanzania, tatizo la kuwa na viongozi wa ovyo tatizo ni TISS maana wao ndiyo wanatakiwa wafanye vetting ya uhakika.Kama kuna bidhaa hafifu za Kenya kwenye soko la Tanzania pia tatizo ni wao TISS kuruhusu Rais kuteua Mkurugenzi Mkuu wa TBS asiye na sifa na Bodi dhaifu achilia mbali Waziri wa Biashara asiyejua Biashara na michezo yake ya kihuni.
Kwa mfano;kama TISS wangekuwa strong Mwigulu asingekuwa Waziri wa fedha na wala Kitila Mkumbo asingekuwa Waziri wa Mipango kwasababu hawana rekodi yoyote ya kuwai kufanya Biashara yoyote walau ata kuwa ata Business consultants.Unamuachaje mtu kama Dr Charles Kimei kwenye Cabinet na unawapa kipao mbele akina Kitila Mkumbo?
"Information is power"
Sent from my V2111 using
JamiiForums mobile app