Hivi idara ya usalama wa taifa wa Tanzania inahusika na kila kitu hadi uuzaji wa nyanya na vitunguu magengeni?

Niulize mara ngapi sasa? Au hujui kusoma na kukielewa ulichokisoma?
 
Usalama wa Taifa kwa TZ kwanza ni wachache sana.

Halafu Muundo wao wa kikazi ni kwa summary unaweza kusema umekaa KIUMBEYA na KICHAWA na umeunganishwa kwa RAIS.

Kwa lugha rahisi, usalama wapo ofisi ya Rais kumsaidia Rais kwenye mambo yake na ikitokea Rais Hana mda na nchi na wao wanakuwa hivyo hivyo.


Ngazi ya Wilaya, wanasimamiwa na DSO ambao unakuta ofisini ni wachache. Kazi yao ni umbeya kutoka ofisi ya DC na Halmashauri kwenda juu hasa RSO.

Na umbeya Mara nyingi siyo wa kusaidia nchi, ni umbeya wa Mfanyakazi fulani hakuungi mkono,anakukosoa sana, mtu gani anasumbua, tajiri gani anafadhili watu wanaopinga utawala wake, au nani hayumo team yako ya uchaguzi.

Ni Ujinga ujinga tu
 
Aliyeleta mada alikuwa sawa ila aishindwa namna ya kuiwasilisha. FYI usalama wa nchi sio kuipigajia ccm ibaki madarakani (kama ilivo kwa sasa). Usalama wa nchi ni lidude lipana hivi? Mfano ukosefu wa fedha za kigeni unaweza sema ni ishu ya kiuchumi tu ila ni purely usalama na mfano wa pili upungufu wa chakula ni usalama wa taifa.
Usalama wetu ni more of political intelligence. Unawezaje kujenda reli kwa kuagiza chuma urusi ukaacha chuma Liganga hapo.

Hawa jamaa waweke kitengo cha Economic intelligence (na wasiwe UVCC watumie knowlegeable personel).

Fikiria mtu aingize mbegu za nyanya zisizoota na kwa fitina akazuia mbegu zingine zote. Nini kitatokea? Inshort hawa jamaa wanatakiwa kuwa wanafikiria mbele sio kuwa driven na matukio ya sasa.
 
Vitengo vya usalama vipo vingi..ila TISS ndio wenye hiyo kazi ya kudhibi watu wajanjawajanja kwenye kila sekta.

KUFIRISI MTU hatakama ni tajili kiasigani..ila kama utajili wako hauleweki vyanzo vyako au vyanzo vyako ni vya magumashi.

KUMSHUSHA MTU hatakama ni maalufu kiasi gani, kama umaalufu wako niwakuumiza watu, au umaalufu unaofikia kuleta madhala hadi kwenye utawala.

KWENYE MPIRA , utavurugwa endapo tu, uwekezaji wako kwenye mpira ni kama kivuri cha kujipatia faida binafsi au kufanya Biashara zingine ukijificha kwenye mpira.

Yoote haya hameasisiwa kwaajili ya watu kuishi kiumoja, amani, ushirikiano, na kuwaelekeza watu kutafuta mali halali na kujipatia kipato halali.

Uzuri chochote unachofanya kwenye uwekezaji MEMO LANDAM inaelekeza kisheria. Hasa eneo unalowekeza, kitu unachozalisha, ushirikiano na watu waliokalibu na eneo lako unalowekeza.

Hivyo ukijifanya mjanja kazi ya kukuminya inakua nyepesi kwao.na utashugulikiwa na watu wengine kabisa kama vile POLICE au TRA, nk
 
Tunaishi kwenye jamii ambayo haiwezi kuhoji kuanzia ngazi ya familia , ngazi ya kitaifa tunaambiwa tuhoji kwa staha aliyeiba pesa nyingi aitwe fisadi .Kwakifupi ukimfundisha mtu kitu leo kesho yake hakijui ukimuliza anakwambia mwalimu hujatufundisha ukimwambie afungue daftari lake anakishangaa amekiandika mwenyewe .Hata ukiwasikiliza wanaobishana mitaani hawabishani kwa hoja yaani uelewa wa watu wengi ni mdogo sana cha ajabu wanajiamini sana hata kama anachoongea ni pumba tupu
 
Mi najiuliza tuu hadi huu ubadhilifu unafanyika ngazi ya halimashauri wao ofisi ya DSO huwa ipo busy na majukumu gani?
Wanalima mpunga huko dakawa na ifakara kila siku tunakuta nao mashambani
 
Unafaham ujasusi wa kiuchumi??
 
Sidhani kama wanadhibiti kila sehemu ya maisha yangu.

Mnawapa sifa ambazo hawana.
Kwa kifupi ukiona taifa lolote linayumba ujue Idara ya usalama ipo hoi na ndiyo maana kazi ya kwanza ya Rais akiingia ofisini asubuhi anaanza na faili la TISS.
Ata Israel yupo pale Middle East kwasababu
ya uimara wa Mosad na USA wanatamba kwasababu ya uimara wa CIA.
Kwaiyo ata Tanzania, tatizo la kuwa na viongozi wa ovyo tatizo ni TISS maana wao ndiyo wanatakiwa wafanye vetting ya uhakika.Kama kuna bidhaa hafifu za Kenya kwenye soko la Tanzania pia tatizo ni wao TISS kuruhusu Rais kuteua Mkurugenzi Mkuu wa TBS asiye na sifa na Bodi dhaifu achilia mbali Waziri wa Biashara asiyejua Biashara na michezo yake ya kihuni.
Kwa mfano;kama TISS wangekuwa strong Mwigulu asingekuwa Waziri wa fedha na wala Kitila Mkumbo asingekuwa Waziri wa Mipango kwasababu hawana rekodi yoyote ya kuwai kufanya Biashara yoyote walau ata kuwa ata Business consultants.Unamuachaje mtu kama Dr Charles Kimei kwenye Cabinet na unawapa kipao mbele akina Kitila Mkumbo?
"Information is power"

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Hapana. Hayo mambo siyajui nimetoa tu maoni yangu. Huenda yasiwe sahihi,na mi ntajifunza kupitia comments za wengine
Yeriko Nyerere ameandika kitabu kwa ujasusi, labda hawajamsoma bado...
 
Mossad huwa wanadili na mambo ya nyanya na biringanya magengeni na unga na sukari kwenye maduka ya mangi?
 
Mkuu hujawai kusikia sukari au Mchele usiofaa kwa matumizi ya Binadamu umekamatwa?
Wewe un

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
We junya kweli!

Hiyo ni dhima ya TFDA.

What is the role of TFDA in Tanzania?


The objective of TFDA is to protect the health of consumers against hazards associated with food, drugs, herbal drugs, cosmetics and medical devices.

https://procedures.tic.go.tz › menu

Food and Drugs license from TFDA - Tanzania Investment Centre

 
Wao siyo kila kitu nchini.

Walio kila kitu nchini ni wananchi.

Bila wananchi, hakuna nchi.
Yaaani bro inasikitisha sana. Wanachi wa tz wanajiona mafala ndio maana huku JF kila mtu anataka kua usalama wa taifa
 
Asante Kwa kufafanua hili. Wabongo wengi hawawaelwi Hawa watu ndio maana wanaoana kama super heroes flani hivi ambao wapo Kwa ajili ya kuwasave wao na nchi.
 
Rwanda ina idara kamili sana ya usalama / ujasusi .
Kilicho nishangaza Zaid ni pale walivyo jipenyeza Hadi kuifanya Rwanda ndio iwe makao makuu ya AFL , Africa football league na Kisha ktk mabango ya mpira kila baada ya sekunde 10 neno " visit Rwanda linajitokeza


Wakaenda mbali Zaid ,club kongwe ya arsenal wameingia mkatba na rwanda kwa kuweka neno visit Rwanda katk bega la kushoto na matangazo kwenye mabango yapo kila second .

SASa jiulize Ni namna gani wanaweza mamb hayo wakt Tanzania tumewazidi rwanda kwa kila kitu

Lkn yote hayo Ni idara kamili ya ujasusi iliyo Bora ndani ya rwanda ndio maana kila eneo wanajipenyeza na kuchukuwa platform kubwa katka majukwaa ya kimataifa, sis bongo ujasusi wetu Ni kuiba tu Mali za nnchi na kufanya upopoyo na kuwa chawa kwa watawal



I wish I could be a president aise Kuna watu wangeteseka Sana snaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…