Hivi ili nawe umeliona? Nyumba za makazi Marekani na Ulaya kutokuwa na fensi ndefu

Hivi ili nawe umeliona? Nyumba za makazi Marekani na Ulaya kutokuwa na fensi ndefu

Sa 7 mchana

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
5,214
Reaction score
10,276
Siku ya jana hiki kitu kili-pop out kwenye akili yangu nikaona ni zooooooom kwa ukaribu zaidi kudhibitisha ukweli wa hiki kitu.

Nili-google picha za nyumba za makazi za wenzetu kwa kweli sikuona fensi ndefu zote fupifupi.
Nikajaribu ku-recall picha za movies, nikawasha Tv kuangalia taarifa ya habari za nje kwa kweli muonekana wa fensi niendelea kuuona kuwa ni ule ule.

Hata kwa baadhi zilikua ndefu bado kulikua na uwazi ambao mtu aliepo nje anaweza kuona ndani fensi kunanini.

Sitaki kuamini kuwa maeneo yote yapo hivyo ila hii kitu inaweza kuwa na fashion au ni matakwa ya mamlaka.

Huku kwetu sasa, fundi anajenga mpaka tofali zitakapo ishia na wenye uwezo wanaongezea electric wire yani ni vurugu.

Kwenu sasa Wataalam wa nyumba na makazi bila kuwasahau Diasporas na wengine wote wenye kufahamu ukweli wa ilijambo.

Screenshot_20220411-174717_1.jpg
 
Mim nadhan huku kwetu swala na ulinzi bado ni kiwango kidogo sana wenzetu wameendelea kidogo kulingana na sisi.

Kule wana camera security mitaan na barabaran ukiwa unavamia tu ukibonyeza 199 polisi hawa sekunde hawana sababu ya kuta kama viwanda ni matumiz mabov ya pesa.

Ila huku kwetu ni security aiseee
 
HUKO KWA WENZETU WANAHAKIKISHIWA USALAMA!!! Huku kwetu usalama hakuna hivi tu watu wamejenga fence lakini vibaka wanaruka!!!

Ukijenga ukuta mfupi hakikisha umeweka matangazo kuwa nyumba inalindwa na mbwa wakali na silaha za moto pengine wataogopa!!!
 
Mim nadhan huku kwetu swala na ulinzi bado ni kiwango kidogo sana wenzetu wameendelea kidogo kulingana na sisi...
dream house yangu ni kwamba haitokua na fensi alafu kutambili za mbele sitting nataka ziwe vioo vitupu yani juu mpaka chini kwenye malumalu.

Kwenye upande wa ulinzi naweza kwama.
 
HUKO KWA WENZETU WANAHAKIKISHIWA USALAMA!!! Huku kwetu usalama hakuna hivi tu watu wamejenga fence lakini vibaka wanaruka!!!

Ukijenga ukuta mfupi hakikisha umeweka matangazo kuwa nyumba inalindwa na mbwa wakali na silaha za moto pengine wataogopa!!!
ama kweli bongo nyoso
 
Usalama na maadili na sheria pia zinachangia kwa wenzetu
Hujajiuliza Mbona nyumba zao milango ya nyuma ni vioo?
Fensi inaweza kuwa mpaka urefu wa mtu mzima na hizo fupi ni kwa mbele ila kwa nyuma baina ya nyumba na nyumba kuna fensi pia ambayo ni ndefu kwa urefu wa mtu
Hii ni sababu ya privacy ya watu na pia hata kama wana wanyama kama mbwa wasibughudhi Jirani
 
Back
Top Bottom